Swali: Show za mieleka ni Kweli au Feki?

Swali: Show za mieleka ni Kweli au Feki?

Hiki kitu lazima kitatugawa makundi mawili.
Wale wapenzi sana wa mchezo huu lazima watasema ni kweli lakini kwa wale ambao sio wapenzi sana watasema ni act au hawajui.

Lakini kuna maswali kadhaa ambayo sijapata majibu yake ya uhakina:
1. Ikiwa huu mchezo sio fake kwa nini hauonyshwi live.
2. Ikiwa sip fake kwanini haupo kwenye mashindano rasmi kama Olympics, Jumuiya ya madola nk.
3. Ikiwa sio fake kwanini mshindi anapangwa kabla ya mchezo kuanza-nini mantiki ya championship?
4. Kuna michezo mingi ya hatari zaidi ya huu, kama vile Bull Ridding, kwanini tunaambiwa DONT TRY THIS AT HOME.wanahofia nini?

Lakini kwa upande mwingine huu ni miongoni mwa michezo inayolipa sana kwa sasa, inawezekana vipi ukawa fake?
Kwenye uwanja kunakuwa na mashabiki kibao, kama ni fake lazima wao ndio wanaolipwa kiingilio, lakini kama ni kweli lazima watakuwa wanalipa kingilio. Swali unawezaje kulipia mchezo ambao kanuni zake zinajulikana kabisa kwamba mshindi anapatikana hata kabla ya mchezo, na ni lazima wanapokuwa wanaingia watakuwa wameishajulishwa mshindi wa siku hiyo?
 
Hii michezo ya freemason kaazi kwelikweli
 
Kuumia wakati wa mchezo hakumaanishi kuwa hawa act, hata wacheza film wanaumia au hata kufa wakati wana act movies
Pia watu kulipa kiingilio na kujaa ukumbini sio issue kwani hata maigizo nk watu wanaingia pia.
Sidhani kama inahitaji akili ya ziada kujua kuwa hii kitu haina uhalisia ule unao onyeshwa.
Na usitegemee kamwe wahusika kukwambia ukweli as long as kwao ni faida zaidi kama watu wakijua hii kitu ni real
 
Uongo mtupu huo,mwanadamu hapigani vile,ukipigwa unakuwa kama zezeta unasubiri upigwe tena ndipo uanze na wewe,hii michezo ni ya kutengeneza tu
 
wabongo sisi sio wafatiliaji mieleka ni fake na tena sio siri wwe wenyewe wanasema kua ni fake, ingia website yao angalia terms zao.
 
labda watu tunashindwa kuelewana hapa juu ya huku kuwa real au fake ki vipi...yaani real kwa maana ipi kwli hii michezo au feki kwamba ni ni kitu cha kutengenezwa tu..!! tunaposema ni real ina maana ni vitu ambavyo kweli watu wanafanya (fake maana yake ni pale watu wanapochukuliwa tu picha zao na matukio yoote kuchezeshwa na computer...kitu ambach si kweli)..ndo maana tunasema ni real sababu yale yoote yanayofanywa ni kweli watu wanafanya ISIPOKUWA ni kwasababu ule ni mchezo kwa ajili ya kufurahisha tu (kama muvies/maigizo mengine) na kinachofanyika jukwaani ni kitu ambacho kimeshapangwa na waandaaji wenyewe na yoote yanayotokea yanakuwa yameshapangwa...kul kupigana, kurukiana ni vitu ambavyo wachezaji woote wanajua kabla ya kuingia jukwaani (ndo maana wanasema ni HIGHLY TRAINED) ili watu wasijaribu!! na wakati mwingine mambo huenda mrama (kama ilivyo katika michezo mingine yoyote watu wanavyoumia bahati mbaya) na kujikuta msanii anaumia kutokana na makosa madogo yanayojitokeza (ndo maana huwa wanaedit kabla ya kurusha)...ila kwenye swala la uhalisia ni kitu halisi kabisa watu wanapigana na kuumia (ila ndo kama nilivyosema ni kwa kupitia mafunzo/maelekezo maalum)..
 
zipo sehem ambazo si fake,kama kuruka kutoka juu,na baadhi ya mambo,
so ni kama nusu fake,nusu si fake
 
Kwenye mieleka mshindi anapangwa,mechi inavyoisha inapangwa ila wanavyopigana kwenye ring kuna risk eg.moves zingine kama tombstone ya undertaker ni hatari mtu kashawahi kuvunjwa shingo. Wanavyosema usitry at home wanamaanisha kuwa wanavyopigana wanatake preventive measures. Halafu mechi zinaonyeshwa live USA ,UK na MEXICO kama unapata setanta unaweza kuangalia tna live. Kuhusu mashabiki wa nje wote wanajua kuwa ni scripted. MI NI MSHABIKI MKUBWA WA MIELEKA NA NIPO OBSSED NAYO.
 
Kuumia wakati wa mchezo hakumaanishi kuwa hawa act, hata wacheza film wanaumia au hata kufa wakati wana act movies
Pia watu kulipa kiingilio na kujaa ukumbini sio issue kwani hata maigizo nk watu wanaingia pia.
Sidhani kama inahitaji akili ya ziada kujua kuwa hii kitu haina uhalisia ule unao onyeshwa.
Na usitegemee kamwe wahusika kukwambia ukweli as long as kwao ni faida zaidi kama watu wakijua hii kitu ni real

kila mtu anajua kuwa ni fake huko nje na bado inaingiza millions of us dollars.
 
ile kitu ni kweli,hata kama ni editing hufanywa kuondoa sehemu zinzoweza kumuudhi mtazamaji kama vile kuvuja damu,lugha kali ya matusi n.k. Miili ile ni 'panya wa maabara' I meana jamaa wanakula steroids na strong antipains kama soda vile,njemba zina madaktari wao. Niliwahi kusikia eti wale kuadhimisha 45th birthday huwa ni majaliwa.

steroid zimepigwa marufuku siku hizi.
 
Mie nimpenzi wa mieleka 100%. Ule mchezo ni kweli na sio acting. Kuhusu vyuo vya Wrestling kuwa ni vipo ila sivijuhi kwa majina ila ukisoma historia za wachezaji utaona kapitia huko au kapata training kutoka kwa kocha fulan wa mieleka. Kuhusu kutokuwa live ni kwasababu Show zile ni Pay-per-view ila zikipita caseti yake ambayo ni recoded uuzwa nafuu zaidi. Kingine watu wengi wa USA ndo wanaona live pitia chanel zao Kama Usa net. Kuhusu kwanin hauchezwi Afrika ni kwamba ule mchezo ni gharama hasa kwenye medical attention pia kulipa wachezaji afrika ule mchezo utasanda wakianzisha mfano SA walijarib ila wakashindwa. Lakin tunao wafrika wawil ambao wanacheza WWE nao ni Justin Gabriel kutoka SA na kingstone kutoka Ghana. Kuhusu kwanin wanaandika dont try this at home ni kwa sababu wapenz weng wa ule mchezo ni Watoto ndo mana wanasisitiza sana watoto wasiige wawapo nyumbani au shuleni Embu fikilia watoto wako wakapigana RKO kwenye cement home lazima utaingia gharama ya kumalizia mtoto wako ng'oa kipande cha jino kilicho bakia.
 
Mieleka ni Maigizo, we huoni hadi imekuwa kama tamthilia, ukitaka ngumi za ukweli angalia Boxing au Kick boxing.
 
Mie nimpenzi wa mieleka 100%. Ule mchezo ni kweli na sio acting. Kuhusu vyuo vya Wrestling kuwa ni vipo ila sivijuhi kwa majina ila ukisoma historia za wachezaji utaona kapitia huko au kapata training kutoka kwa kocha fulan wa mieleka. Kuhusu kutokuwa live ni kwasababu Show zile ni Pay-per-view ila zikipita caseti yake ambayo ni recoded uuzwa nafuu zaidi. Kingine watu wengi wa USA ndo wanaona live pitia chanel zao Kama Usa net. Kuhusu kwanin hauchezwi Afrika ni kwamba ule mchezo ni gharama hasa kwenye medical attention pia kulipa wachezaji afrika ule mchezo utasanda wakianzisha mfano SA walijarib ila wakashindwa. Lakin tunao wafrika wawil ambao wanacheza WWE nao ni Justin Gabriel kutoka SA na kingstone kutoka Ghana. Kuhusu kwanin wanaandika dont try this at home ni kwa sababu wapenz weng wa ule mchezo ni Watoto ndo mana wanasisitiza sana watoto wasiige wawapo nyumbani au shuleni Embu fikilia watoto wako wakapigana RKO kwenye cement home lazima utaingia gharama ya kumalizia mtoto wako ng'oa kipande cha jino kilicho bakia.

Mkuu kuna link zimetolewa hapo juu zinazoonyesha kwamba huu mchezo ni maigizo kama zilivyo sinema zingine. Binafsi nimependa ufafanuzi wako, ila ingekuwa vizuri kama ungeweka hapa japo link moja inayothibitisha kuwa mchezo huu sio maigizo. Na pengine ukatuambia ni kwanini hauko kwenye orodha ya mashindano michezo rasmi kama vile olympics.
 
...ukipigwa unakuwa kama zezeta unasubiri upigwe tena ndipo uanze na wewe,hii michezo ni ya kutengeneza tu...

That is Exactly the point!!. Mimi nashidwa kuelewa kwanini wanaopenda wrestling hawaoni hiyo simple fact. Yani mwenzako anapanda kamba ya ulingo kisha anajiweka vizuri ili akuangukie nawewe umakaa tuu chini unasubiri uumizwe. Narefarii anaruhusu mtu atoke ulingoni kutafuta kiti chakumpiga. Kisha refarii anaruhuru vifaa vya hatari kama vile ngazi, meza, and vyuma viingizwe ulingoni ??? That is crazy if people believe this is not preplanned.

Najaribu kutafuta which I think was a USA congressional hearing (mkutano wa bunge la Marekani) ambalo liliilazimisha watu wa Wrestling kukubali kwamba wanachofanya sio sports bali ni entertainment. I believe the issue nikuwa Marekani - The federal government have a different taxation between sports and entertainment. Basically, congress ilikuwa inataka Wrestling programs zilipe kodi zaidi kama entertainment, na sio kama sports ambayo kodi ni chini. Hii ilikuwa miaka ya 1996-98, I cannot remember, I will try to google the hearing....or if someone remember this hearing.

Someone once said "wrestling is to men what soap-opera is to women".
Kama unataka kuona mapambano ya ukweli angalia Boxing or UFC.
 
Ile kitu ni real wakuu watu wako well trained ndo maana wanasema dont try this at home,lkn vie vile unaambiwa it takes years to practise and to do safely,kama kuna mtu ana access ya ten sports aangalie kipindi kinaitwa TOUGH ENOUGH Kinaonyesha watu wanavyotrainiwa mieleka na walimu wao ni Stone Cold na King Bourker.Ingekuwa mambo ya kupanga kila mcheza mieleka angepata ubingwa lkn kuna wengine hata mikanda midogo km USA champion na Tag team hawajawahi pata.
 
Mkuu kuna link zimetolewa hapo juu zinazoonyesha kwamba huu mchezo ni maigizo kama zilivyo sinema zingine. Binafsi nimependa ufafanuzi wako, ila ingekuwa vizuri kama ungeweka hapa japo link moja inayothibitisha kuwa mchezo huu sio maigizo. Na pengine ukatuambia ni kwanini hauko kwenye orodha ya mashindano michezo rasmi kama vile olympics.

Kuhusu kuweka link nadhan usome tu page yao ya wwe.com au usome wikipedia za mchezaji mmoja utaona. Kuhusu kwanin mchezo haupo kweny list sina jib kamili ila kuna watu kama Kurt Angle alishawahi shinda Medali olympic ya 96. Kuna Bob Lashley yeye ameshinda medali za ndani USA. Just google hayo majina utapata maelezo yao kweny wikipedia.
 
Ni fake make kila kitu hupangwa kabla . Hata hivyo wachezaji lazima wawe well trained kuepuka madhara kama kuvuja damu nyingi na kuvunjika. Angalia mshindi inapobidi apatikane mara nyingine anaepigwa hujifanya ndondocha kama haoni pigo laja ilhali watu wengine wote twaliona. Ulishaona wapi kitu kama hicho kwenye boxing? Vipi umpige adui yako, aanguke chini akiwa hoi, wewe unaanza kushangilia dakika kadhaa mpaka anajivuta ,anasimama na kukupa pigo la ushindi bila wewe kuona? Hapo ina maana wewe ni taahira. Tuache ushabiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom