Swali shirikishi kwa watanzania

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,476
2,651
Wasalaam, wote tumeshuhudia ziara za makonda akizunguka nchi zima na kutoa maagizo yasiotekelezeka ambayo kimsingi maagizo yalipaswa kutolewa na rais au waziri mkuu.

Swali langu ni kwamba je bajeti ya pesa anazotumia bwana huyu ni kodi za watanzania au ni pesa za ccm? maana kama CCM waliweza kuchukua viwanja vya umma vya michezo na kujimilikisha pasipo huruma watashindwaje kutumia pesa za umma kwa kurubuni wananchi.
 
Mimi langu ni hili
JamiiForums-1216034906.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti anatoa maagizo yasiyo tekelezeka!, na hapo hapo tena eti yalipashwa yatolewe na mhe rais au waziri mkuu, yaani inabidi uwe mjinga wa kiwango cha degree kukubaliana na hawa watu.
 
Hata angekuwa waziri asiye na wizara maalum, bado anakuwa na mipaka ya kiutendaji.
Jukumu lake ni kueneza itikadi za chama. Aite vyombo vya habari amalizane nao, siyo kuwasimami watumishi wa serikali.
 
Hata angekuwa waziri asiye na wizara maalum, bado anakuwa na mipaka ya kiutendaji.
Jukumu lake ni kueneza itikadi za chama. Aite vyombo vya habari amalizane nao, siyo kuwasimami watumishi wa serikali.
Na shida iko hapo, hajui mipaka yake ya kazi, katibu au makamu mwenyekiti wala hawatoi MAIGIZO kama hayo.
 
Sijui kama niko sahihi!
Nafikiri huenda ni ruzuku! CCM inachukua asilimia kubwa ya ruzuku kuliko vyama vingine!
Na hiyo ni pesa ya serikali tu!
 
Na shida iko hapo, hajui mipaka yake ya kazi, katibu au makamu mwenyekiti wala hawatoi MAIGIZO kama hayo.
Anatafuta ulaji kwa nguvu, na uongozi hawezi, anatafuta madaraka na mamlaka, kunyanyasa watendaji.
Aachiwe serikali yote aiendeshe yeye mjuaji.

Dar es Salaam aliikuta na kuicha kama alivyoikuta, anajidai anaajua kutetea na kuondoa uovu, wakati kila kitu ni ujinga mtupu.

Aende kwenye vikao vya ndani vya kila kata, wilaya na mikoa yote na aongoze vikao vyote na atoe maagizo yeye, na afuatilie utekelezaji yeye.

Maana yake sijui awe rais yeye au katibu mkuu kiongozi? waziri asiye na wizara maalum?

Kama anataku kuwa rais, asubiri agombee.
 
Back
Top Bottom