Swali la weekend kwa wanafamilia...

Swali la weekend kwa wanafamilia...

Kwanza hiyo laki tano umeshaiona au??
Kama umeiona basi ni laki saba lakini kama unaiwaza tu hujaiona ni laki mbili maana hutokaa uione
 
Mimi kama mimi pato haliwezi kuwa laki 7 wala haliwezi kuwa laki 2.
Mimi ntachangia pato la familia lakini sio hela yote.
 
Inategemeana na ulivyoseti familia yako, mi na mke wangu hata kama sijapata hata mia lakini yeye kapata milioni ni za familia yangu
 
Hapo kipato cha familia ni laki mbili, kwa mujibu wa maandiko ya dini mwanaume ndiye kichwa cha familia na ndiye aliyepewa jukumu(adhabu) ya kula kwa jasho lake, mwanamke alipewa adhabu ya kuzaa kwa uchungu hivyo mke ana hiyari ya kuchangia au kutokuchangia kipato. Imagine uzae kwa uchungu halafu ule kwa jasho lako, utumikie adhabu yako na ya Mme, not fair
 
Wewe mwanaume una laki mbili

Na mkeo ana laki tano....

Swali ni hili...hapo kipato cha familia hapo ni kiasi gani?

Nimeikuta watsap groups imeleta ubishani..

hebu wana MMU tutajie majibu kwa mujibu wa uzoefu wako...
Ni laki mbili tu....no mjadala
 
Kwangu mimi itakua laki 5, ntamuongezea laki 3 laki 2 ntaiweka pembeni nifanyie vitu vyangu vingine!
 
Wewe mwanaume una laki mbili

Na mkeo ana laki tano....

Swali ni hili...hapo kipato cha familia hapo ni kiasi gani?

Nimeikuta watsap groups imeleta ubishani..

hebu wana MMU tutajie majibu kwa mujibu wa uzoefu wako...

Nadhsn hii inategemea famila na familia.
 
Kwanza hiyo laki tano umeshaiona au??
Kama umeiona basi ni laki saba lakini kama unaiwaza tu hujaiona ni laki mbili maana hutokaa uione

We mumeo asipoona hela yako hapati hata robo?
 
Kwanini wanawake harusi...na kitchen party wanazijali kuliko familia?
Inategemea na aina ya mwanamke na malezi aliyonayo,kwa experience yangu kwa maisha ya sasa hivi wanawake tuneibeba familia kwa asilimia kubwa kuliko wanaume na kwa kiasi kikubwa tuna mapato makubwa kuliko nyie wanaume na ndio maana unaona hata mwanaume kipato kikiyumba familia bado inabaki stable,hakuna maisha ya kumtegemea mtu mmoja kuendesha famila karne,hiyo ilikua zamani sana na ndio maana na sisi kina mama tunafight kwa kila njia kubuni vyanzo vingi vya income hata kama tumeajiriwa unakuta hukosi kuuza vitenge,vipodozi au hata una kagenge kauokoteza visent vya kununua mboga
 
Hongera sana kama ni kweli unafanya hivi
 
Kwa uzoefu wangu hapo ni laki mbili maana wakina mama kuchangia matumiz ya familia wanaona sio lazima,ikitokea kachangia chochote anakua kama kakopwa.Ni wanawake wachache sana wanaoweza kua na nafsi yakuchangia maendeleo ya familia bila kua na roho yaubinfsi.Hiyo ni sawa nakukuta mwanamke mwenye kipato kikubwa au msomi zaid ya mumewe na akawa hana maneno maneno kwa mumewe.Wengi wao ikiwa ivyo lazima uisome namba kwa herufi kubwa.
 
Hongera sana kama ni kweli unafanya hivi
Nimepitia huu uzi nimeaikitika sana,sijajua kama hizi coments za wanaume ni za kweli au wanaongea tu kwa sababu kuna jinsi wanavyotuchukulia, mwanaume anaweza kutelekeza familia lakibi sio mwanamke, hata atelekezwa na watoto kumi there is no way atakuabali kuwaacha watoto wafe njaa,she will fight hata kwa kuuza vitumbua watoto wale,na wanawake wengi zama hizi wanabeba familia zao na pia maisha yamebadilika,majukumu ya familia yanachangiwa na wote baba na mama,wakati mwingine hata hujui pesa ya mume imepitia wapi ila maisha yanasonga na hakuna kinachopungua kwenye familia,nadhani hii inatokana na misingi ya familia yenu mliyoijenga tangu mlipoingia kwenye ndoa,ila kamamwanaume ulimzoeza mke kuwa tegemezi kwa kial kitu usitegemee kwamba leo unaweza kumshawishi achangie kipato cha familia maana sio misingi uliyomjengea

Kwa hiyo wanaume mtuache jamani,ur coments are too negative compared to reality
 
jamani mi ni mwanamke na nimeolewa, sio wanawake wote wanatabia hiyo kwenye familia yangu hiyo ni laki 7. kama mume wangu anapesa ya ziada namuomba anipe nikasuke n. k ninapenda kila kipato ninachopata nishirikiane na mume wangu kukifanyia maamuzi. Ila siku nikijua mume anamchepuko hahahhaaaaa zoezi litaishia hapo, badala ya laki 7 itakuwa 2.
 
Nimepitia huu uzi nimeaikitika sana,sijajua kama hizi coments za wanaume ni za kweli au wanaongea tu kwa sababu kuna jinsi wanavyotuchukulia, mwanaume anaweza kutelekeza familia lakibi sio mwanamke, hata atelekezwa na watoto kumi there is no way atakuabali kuwaacha watoto wafe njaa,she will fight hata kwa kuuza vitumbua watoto wale,na wanawake wengi zama hizi wanabeba familia zao na pia maisha yamebadilika,majukumu ya familia yanachangiwa na wote baba na mama,wakati mwingine hata hujui pesa ya mume imepitia wapi ila maisha yanasonga na hakuna kinachopungua kwenye familia,nadhani hii inatokana na misingi ya familia yenu mliyoijenga tangu mlipoingia kwenye ndoa,ila kamamwanaume ulimzoeza mke kuwa tegemezi kwa kial kitu usitegemee kwamba leo unaweza kumshawishi achangie kipato cha familia maana sio misingi uliyomjengea

Kwa hiyo wanaume mtuache jamani,ur coments are too negative compared to reality

Mbona hujasema lolote kuhusu comments za wanawake waliosema pesa ya familia ni ya mume tu
yao ni ya binafsi
 
Back
Top Bottom