mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,851
- 3,486
TAtizo ni U first lady
Mzee Mwanakijiji kama hajakuelewa mkuu basi amegoma kuelewa. Sio wote tunaunga mkono mabadiliko ni vigeugeu. Actually tumesimamia kwenye hoja ya msingi ambayo ni katiba yetu wananchi kama inavyosomeka katika rasmu ya pili. Tunauhakika zaidi ya 10000000000000% kuwa CCM hawataki hilo. Na tunauhakika 100% kuwa kwenye ukawa hilo ndiyo jambo lao na letu la msingi.Please pitia tena rasmu ya pili ya katiba mpya utajua watz tunataka nn? Hii uliopost si ya level yako Mkuu.
Sorry
Tanzania kamwe haiwezi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM.
CCM itatawala milele.
Anayebisha na alinakili hili bandiko langu kama rejea ya baadaye.
Narudia tena, CCM itatawala milele.
Hivi Dr. Slaa alitokea chama gani?
DAH.....Kulingana na mleta Mada..nadhani itakuwa CNDD(SIEN-DEDE):bolt:
Dah. Kumbe Hata Nyani Naye Ameacha Kurukia Miti. Naekaja Kuisaidia Ccm? Teh. Teh. Teh.
Nimeamini maneno ya Generali Ulimwengu kuwa wakati wa uchaguzi watu huweka akili zao sehemu fulani na kuzifuata baada ya uchaguzi kuisha. Nyani Ngabo amefikia mahali anajifanya hata maana ya neno milele hajui. Duh hii ni hatari sana. Nasubiria hoja zako baada ya uchaguzi
hapo kwenye red=ni Mabadiliko mbele kwa mbele!Na. M. M. MwanakijijiMojawapo ya vitu vinanishangaza sana wakati huu wa kampeni na hasa tangu Lowassa apewe kiti cha enzi CHADEMA ni kuwa watu waliompokea na wenye kumuuza mbele ya umma wanadai kuwa wamempokea ili aongoze harakati za mabadiliko. Utawasikia watu wanasema - bila kufikiria sana "tunataka mabadiliko" na kuwa CCM ikitoka tutapata mabadiliko. Wengi wanazungumzia "mabadiliko" kama tukio fulani ambalo litatokea baadaye. Cha kusikitisha ni kuwa wao wenyewe hawajui au hawataki kujua, hawaamini au hawataki kuamini kuwa tayari mabadiliko yameshatokea; mabadiliko ambayo yamewabadilisha wao. Kama watu wenye akili timamu walishapata mgombea wao wa Urais, wakampitisha na kumthibitisha halafu wiki chache baadaye wakaenda kumchukua mgombea toka CCM na hivyo wakamtupa mgombea wao wenyewe, tena si mtu baki tu Katibu wao Mkuu wa chama, watu hawa hawa wanaweza vipi kuja na kusema ati wanataka "mabadiliko"? Yaani, watu waliobadilika wanataka kubadilika tena? Waweje?Ukiangalia kwa jicho lililotulia utaona kuwa ni sisi ambao hatujabadilika au kubadilishwa na ujio wa Lowassa ndio hasa tunataka mabadiliko au tunahitaji mabadiliko. Ndio sisi ambao tunatakiwa kubadilika! Ndio maana watu wanatuona tumekuwa wagumu na hatuungi mkono harakati zao (hatujabadilika!). Kumbe kati yetu na wao ni sisi tunaweza kwa haki kabisa kuzungumzia mabadiliko kuliko wao. WAo hawana uhalali (legitimacy) wala hoja (reason) za kusema wanataka mabadiliko. Wanayataka mabadiliko yapi na ya nini? Ndio maana mwisho wa siku jibu lao ni "kuitoa tu CCM madarakani mengine baadaye". Kumbe wakati huo huo wamechukua CCM, mgombea wa CCM na wanachama wa CCM wenye kumuunga mkono mwana CCM mwenzao ambao waliapa kuwa "alipo" na wao "wapo"! Wenzetu mnaoimba na kushabikia "mabadiliko" yajayo, hivi hamjioni kuwa tayari mmebadilika? au mtabadilika tena ikitokea mshinde au mkishindwa tena mtabakia hivyo hivyo - naamini wengi watabadilika baada ya kushindwa na kujaribu kurudi mlikokuwa - mkitaka mabadiliko tena! Isije kuwa wenzetu ni watu wa kubadilika badilika tu na ujio wa upepo wa mabadiliko! Si kiongozi mwenyewe wa mabadiliko tayari ameshabadilika? na akija kubadilika tena sijui tutawaitaje. Vinyonga wa kisiasa? Fikiria.MMM
Naona enyi 'waMarekani' mmeamua kutukatisha tamaa na kutuchagulia Magufuli. Ingependeza mngekuja kujiandikisha na kupiga kura, ndipo tungejua kama maneno yenu yanatoka kwenye keyboard au moyoni.Mimi wala si CCM.
Lakini nikiangalia Watanzania walio wengi, nikiangalia mambo mengine kama tume ya uchaguzi ya CCM (NEC), nikiangalia jinsi ambavyo watu uliodhani ni wataka mabadiliko ya kweli ila hivi sasa hata hawaeleweki ni watu wa aina gani, nakosa matumaini kabisa.
Hivyo narudia tena, CCM itatawala milele nchii hii. Kwa hiyo nawe lihifadhi tu hili bandiko langu kwa rejea ya baadaye.
Naona enyi 'waMarekani' mmeamua kutukatisha tamaa na kutuchagulia Magufuli. Ingependeza mngekuja kujiandikisha na kupiga kura, ndipo tungejua kama maneno yenu yanatoka kwenye keyboard au moyoni.
Nilitaka niandike kitu lakini nafikiri hapa umemaliza, ila uchaguzi huu umenifanya nione kwa nini tanzania kama taifa tumezorotaMwanakijiji wewe unasema hujabadilika wenzio wanakuona umebadilika. Siyo yule kamanda waliyekuwa naye wakati huo.
Tatizo ni nini? Tatizo kubwa kwangu mimi ni mtazamo wa mabadiliko. Wakati wewe muda wote uliangalia watu wenzio walingalia mfumo. Kwa mfano wewe unaona Lowassa ambaye alikuwa kiongozi CCM na kwa hiyo na yeye amechangia kutufikisha hapa, hawezi kuleta mabadiliko. Wenzio wanaona CCM kama mfumo ambaye imetufikisha hapa haiwezi kuleta mabadiliko. Hivyo wakati wewe unakataa mtu wa CCM asichukuliwe wenzio wanaamini yeyote atakayesaidia kubomoa mfumo CCM anafaa.
Nachoshangaa mimi ni wewe kuwaona wenzio kama hawafikirii vizuri
This is indeed a poor thinking!Lowasa anakashfa za wizi wa mali ya umma, Slaa hana!Lowasa hajashiriki kuijenga chadema, Slaa ameshiriki mpaka kapata ulemavu wa mkono, Slaa alihamia chadema kwa kuombwa na wana karatu -Lowasa alikuja chadema kwa matakwa yake ya kutaka Urais, Chadema haikuwahi kumtuhumu Slaa kwa kashfa yoyote kabla hajajiunga nayo-Chadema ilimwita Lowasa fisadi na kutoa orodha ya mafisadi "List of shame" na kumtaja Lowasa na mengineyo. Kweli hujui utofauti wa Slaa kuja chadema na kuja kwa Lowasa huuoni wala huujui????!Poor analysis. Kwani huyu Katibu mkuu alitoka wapi? Sio CCM? Sasa ana tofauti gani na hawa watanzania wengine waliojiunga na CHADEMA sasa? Lowasa kwa sasa ni mwanachama wa CHADEMA na kadi alipewa mbele ya macho ya watu wote. Ana haki ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mabadiliko yanatakiwa ni kuitoa CCM na mfumo wake madarakani. Kama hujakubali hulazimishwi, wengine wamestaafu siasa. Hii ni demokrasia.
Mkuu ukiona mtu ameanza lugha za picha jua hoja andishi zimefika kikomo, kufika mwisho wa ukomo wa kuandika humaanisha mwisho wa ukomo wa kufikiri, huleta dhana ya kukata tamaa!! hapo ndipo alipofikia mzee mwenzangu Mwanakijiji. Msameheni bure si wazee wote wasiojitambua nchi hii ni baadhi tu kama yeye. yeye ni miongoni mwa watazamao maslahi yao zaidi kuliko taifa ndio maana watu wa aina yake huabudu na kutumai katika watu.Nilitaka niandike kitu lakini nafikiri hapa umemaliza, ila uchaguzi huu umenifanya nione kwa nini tanzania kama taifa tumezorota
1.ni kuwa na kizazi cha wazee kama akina mwanakijiji ambao wengi wao
-waoga
-wanafki
-maslahi mbele na kujidai wanapenda taifa
Lakini wakazalisha kizazi cha watu waoga, cowards- watu waliokosa uthubutu kwenye kila nyanja. Unafikiri watoto wa mwanakijiji watakuwa watu wa aina gani..?
Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya vitu vinanishangaza sana wakati huu wa kampeni na hasa tangu Lowassa apewe kiti cha enzi CHADEMA ni kuwa watu waliompokea na wenye kumuuza mbele ya umma wanadai kuwa wamempokea ili aongoze harakati za mabadiliko. Utawasikia watu wanasema - bila kufikiria sana "tunataka mabadiliko" na kuwa CCM ikitoka tutapata mabadiliko. Wengi wanazungumzia "mabadiliko" kama tukio fulani ambalo litatokea baadaye.
Cha kusikitisha ni kuwa wao wenyewe hawajui au hawataki kujua, hawaamini au hawataki kuamini kuwa tayari mabadiliko yameshatokea; mabadiliko ambayo yamewabadilisha wao. Kama watu wenye akili timamu walishapata mgombea wao wa Urais, wakampitisha na kumthibitisha halafu wiki chache baadaye wakaenda kumchukua mgombea toka CCM na hivyo wakamtupa mgombea wao wenyewe, tena si mtu baki tu Katibu wao Mkuu wa chama, watu hawa hawa wanaweza vipi kuja na kusema ati wanataka "mabadiliko"? Yaani, watu waliobadilika wanataka kubadilika tena? Waweje?
Ukiangalia kwa jicho lililotulia utaona kuwa ni sisi ambao hatujabadilika au kubadilishwa na ujio wa Lowassa ndio hasa tunataka mabadiliko au tunahitaji mabadiliko. Ndio sisi ambao tunatakiwa kubadilika! Ndio maana watu wanatuona tumekuwa wagumu na hatuungi mkono harakati zao (hatujabadilika!). Kumbe kati yetu na wao ni sisi tunaweza kwa haki kabisa kuzungumzia mabadiliko kuliko wao. WAo hawana uhalali (legitimacy) wala hoja (reason) za kusema wanataka mabadiliko. Wanayataka mabadiliko yapi na ya nini?
Ndio maana mwisho wa siku jibu lao ni "kuitoa tu CCM madarakani mengine baadaye". Kumbe wakati huo huo wamechukua CCM, mgombea wa CCM na wanachama wa CCM wenye kumuunga mkono mwana CCM mwenzao ambao waliapa kuwa "alipo" na wao "wapo"!
Wenzetu mnaoimba na kushabikia "mabadiliko" yajayo, hivi hamjioni kuwa tayari mmebadilika? au mtabadilika tena ikitokea mshinde au mkishindwa tena mtabakia hivyo hivyo - naamini wengi watabadilika baada ya kushindwa na kujaribu kurudi mlikokuwa - mkitaka mabadiliko tena! Isije kuwa wenzetu ni watu wa kubadilika badilika tu na ujio wa upepo wa mabadiliko! Si kiongozi mwenyewe wa mabadiliko tayari ameshabadilika? na akija kubadilika tena sijui tutawaitaje.
Vinyonga wa kisiasa?
Fikiria.
MMM