- Thread starter
- #41
Imani ni jambo la binafsi sana na kwa vile imani si kitu kinachoweza kuonekana, kushikika, kunuswa, kusikika, au kuonjeka, ni vigumu sana kujua kina cha imani ya mtu.
Ni mtu mmoja mmoja tu, kwa maana ya yeye kama yeye ndiyo anaweza kusema imani au mashaka yake juu ya uwepo wa mungu ni kiasi gani.
Kwa mfano, mimi siwezi kujua kina cha imani ya Papa Francis juu ya uwepo wa mungu. Wewe unaweza?
Nadhani anachojaribu kusema yeye ni kwamba hakuna mtu mwenye imani ya kuweza kuondoa doubts juu ya exisitence ya mungu.
Sasa sijui yeye amewezaje kutambua imani za wengine.