Swali kwa wanachama wenzangu CCM, mmewahi kuwaza kuwa yaweza siku moja chama tofauti na sisi kuongoza nchi? Tumejiandaa kisaikolojia?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Ikumbukwe ikatokea Chama tofauti na sisi kikaongoza basi yafuatayo ndo tutayajutia
1. Rais wao atakuwa na madaraka kadhaa ambayo yapo juu ya Mungu
Kuua, Kuteka, Kusweka watu ndani, namaanisha mmepuuza katiba mpya subiri nao waongoze,

2. Rais akitoka upinzani atatumia dola kulinda nguvu ya chama chake

3. Atatumia Rasilimali za nchi kuimarisha chama

4. Atateua wakurugenzi siyo kutumikia wananchi bali kutumikia Chama

Ndo maana Nasema Mlikata katiba mpya hali hii yaweza kuwakuta
 
Yaaani hizo hofu zote hazipo endapo Tundu Antiphas Lissu akiwa Raisi!!

Hii ni kwa sababu hoja kuu ya Chadema katika uchaguzi wa mwaka huu ni kuwa wataanzisha mchakato wa Katiba mpya ambao utaanzia pale alipoishia Jaji Warioba!

Watanzania tuna assurance ya asilimia 100 kuwa Chadema wakishika madaraka tabia za kijinga za CCM hazitakuwepo kwa sababu ya uwepo wa Katiba mpya ya wananchi ambayo inapunguza madaraka ya Raisi na kuweka mifumo mipya ya utawala!!
 
Huo muda wa Chama mbadala haujafika bado, ukifika itaonekana tu, na CCM wenyewe wataanza kuona dalili za mwisho wao na watajipanga, haya mambo huwa hayatokei tu ghafla bin vuu, ni process na mpaka sasa hivi hata dalili hakuna, Raisi Magufuli Uchaguzi ujao atashinda kwa > 80% na Wabunge na Madiwani wengi sana, kwanza chadema wala siyo tishio kwa CCM sasa ukilinganisha na 2015, ...
 
Umesahau habari ya kupe?

Toka ng’ombe anapelekwa mnadani yeye yumo tu ananyonya!

Ng’ombe anauzwa mnadani yeye bado yumo kwenye ngozi. Anachinjwa na ngozi kuchunwa, yeye bado ameng’ang’ana! Ngozi inaanikwa na kuja kuwambwa anafia humo.

Hata manzi yana tabia hiyo hiyo ya kufia kwenye kidonda.

Busara na ccm wapi na wapi?
 
Chadema hatuhitaji mizizi bali tunawasikiliza watanzania!
Watanzania wametaka muda mrefu kuwa na katiba mpya huku chama chenye mizizi kikikwepa kwa maslahi yao ili kiendelee kufisidi nchi na kutapanya rasilimali za umma
Thubutu! Ccm ndio washitaki, ndio mawakili na ndkio jaji. Atashindwaje hiyo kesi? Ndiye kocha na refa na mchezaji atashindwaje mechi hiyo? Ikibidi hata goli la mkono mradi kushinda. Labda nguvu ya umma lakini Watz waoga! Jpm akishindwa atatangazwa kwa lazima na hamtafanya chochote.
 
Ikumbukwe ikatokea Chama tofauti na sisi kikaongoza basi yafuatayo ndo tutayajutia
1.Rais wao atakuwa na madaraka kadhaa ambayo yapo juu ya Mungu
Kuua, Kuteka, Kusweka watu ndani, namaanisha mmepuuza katiba mpya subiri nao waongoze,

2.Rais akitoka upinzani atatumia dola kulinda nguvu ya chama chake

3.Atatumia Rasilimali za nchi kuimarisha chama

4.Atateua wakurugenzi siyo kutumikia wananchi bali kutumikia Chama

Ndo maana Nasema Mlikata katiba mpya hali hii yaweza kuwakuta
Ccm ingekuwa na watu wenye akili,magu asingekuwa rais
 
Siku tukitoka madarakani it will take century kuwa kwenye power.
It will never happen ccm kurudi tena madarakani.
Why?

Chama kimelelewa kwa mfumo wa kulindwa na dola na unafuu wa kufanikisha maslahi ya mtu mmoja mmoja.

Hivyo kikitoka madarakani kundi lote la wanaccm ambao ni wasaka maslahi watakihama chama kwenda kwenye chama kilichopo madarakani ili kupata unafuu wa madaraka na shughuli zao.

Kinachoiunganisha ccm kwa sasa siyo itikadi ni uwepo wa dola tu. Short of that hakuna ccm.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Unafikri ccm haiko tayari kuachia wengine waongoze?

Au unafikri wanachi hawapo tayari kuwapa wengine waongoze?
Wapo tayari sana, shida inakuja,

Je nani atakuwa mbadala wa ccm? We fikira mtu kama Lisu leo anasimama anasema hutuwezi kuishi bila wazungu!, hapo hapo Amsterdam amejipinda huko Twitter ameacha kila kitu anampigania Lisu awe rais, watu wanajiuliza huyu ana maslahi gani na Lisu? Ni uanasheria tu kwa yaliyomkuta au kuna lingine?

Kisha anasema hana maslahi na Zanzibar, maana yake Zanzibar hata ikienda na maji yeye kwake sawa tu.
Unafikri hili hata vyombo vya usalama vitamuunga mkono mtu kama huyu?

Wanachi wakifikiria yote hayo wanaona bora wampe tu ccm aendelee kutawala.
 
Katika historia hakuna utawala wa kibinadamu ulidumu milele, hakuna! Kwanini sisi tudhani ni baghairi (exceptional)? Nithibitishe hoja yangu kwa mifano michache ya mataifa makubwa yaliyowahi kutawala dunia, lakini yaliangukia pua:

(1) Babeli, chini ya Nebukadneza, iliyashinda mataifa makubwa na kutawala tangu 626 - 539 B.C. ikaanguka na kufutika katika historia. (2) Umedi na Uajemi waliungana na kuangusha himaya ya Babeli, na wenyewe ulianguka (539 - 331 B.C.). (3) Ugriki/Uyunani ukainuka kwa kishindo chini ya kijana machachari, Alexander Mkuu, lakini ulianguka na kufutika (331 - 63 B.C.). Leo hii Ugriki ni moja ya mataifa maskini ulaya, kama vile halikuwahi kuongoza dunia kwa wasomi, siasa na uchumi. (4) Himaya ya Roma ikainuka na kutawala zaidi ya miaka mia tano, lakini ikafutika (63 B.C. - 476 A.D.).

Seuze CCM! CCM ni kitu gani? Wapumbavu pekee ndio wanaamini kuwa hawawezi kushindwa milele. Hamjifunzi hata kwa majirani zetu ukweli huu wa historia? Historia haidanganyi kamwe!
 
Back
Top Bottom