Kitaturu,
Kuna kitu umenikumbusha hapa. Kwamba JK aliyaona haya lakini akatuliza bori. Naona ni kwasababu JK alikuwa na upeo wa Kimataifa kuhusu Mikataba na Foreign Affairs issues. Lakini Ngosha mpaka leo hajakanyanga Ulaya, Asia wala Marekani. Yumkini ndiyo maana anafanya madudu kila kukicha....!
Siyo tu yamkini alikuwa na upeo wa mambo kimataifa, lakini pia KUSIKILIZA na KUWA MTULIVU kabla ya kuamua jambo, ni hekima na busara zaidi ambayo ni Mungu pekee ndiye atoaye hilo especially kwa viongozi wakubwa kama Magufuli aliyebeba mstakabali wa mamilioni ya watu....
Kosa dogo kwa maamuzi yasiyoongozwa na hekima na busara, ni kilio na kusaga meno kwa wanaokutegemea !!!
Binafsi sisemi kuwa, Rais Magufuli asi - review makosa ya watangulizi wake kina Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete na kisha kufanya marekebisho inapowezekana....la hasha....
Hoja na point yetu sisi wengine ni, HOW EXACTLY THIS IS DONE ?...... baasi
Lakini inavyoonekana, wapiga zumari wengi wa huko mtaa wa pili wa - CCM hawatuelewi na merely think sisi tunapinga tu.... kumbe sisi ndiyo hasa wazalendo.....
Mzalendo wa kweli ni yule mwenye uwezo wa kutambua makosa yake na kuyarekebisha kwa busara, uwazi na hekima bila kulaumu wengine.......
This is absolutely contrary to Magufuli na wana CCM wenzake huko..... Wao kila kitu wanakipeleka kwa lengo la kupata "political scores" tu... Wengine wakijibu mapigo, wanaleta figisufigisu za kipuuzi !!
No way, hawa ni kuwadunda tu kushoto, kulia, mbele na nyuma until they get out of our way....
Makosa waliyafanya wao kwa kusaini mikataba ya hovyo na kinyonyaji utadhani walikuwa wamefumba macho yao ya nyama na yale ya ufahamu wao waliopewa na Mungu, Leo wanajitokeza kwa njia za kinafiki kutaka kurushia zigo la lawama kwa wengine wakiongozwa na jazba huku maarifa, hekima na busara wakiwa wameziweka mifukoni mwao !!!