Swali kwa mara ya mwisho, Wataalamu wa mining, kwanini Serikali isinunue Acacia?

Kununua mgodi na kuendesha mgodi ni vitu viwili tofauti kabisa. Havifanani hata kidogo. Kukuelewesha vizuri nitatoa mfano huu: Mfano unaofanana na wazo lako ni kama vile unataka bodi ya Shirika la Afya Muhimbili iwaondoe wafanyakazi wake wooote (eg madaktari, manesi, watu wa maabara, wafasia nk) halafu ichukue watu mtaani wakazibe zile nafasi!

Kwani Serikali haiwezi kununua Mgodi na kuendelea kuundesha wakati kila kitu kikiwa intact, kama Wafanyakazi na Mikataba yao, na mambo mengine ambayo yapo? Kwa kifupi ni kama kubadilisha mmiliki tu lkn kila kibakie vile vile labda hata kuweka makubaliano na wauzaji kwenye kukodisha expertise n.k.
 
STAMICO WAKO PALE TULAWAKA WANAJIITA STAMIGOLD, UNGEAANZA KWANZA KUANGALIA MAENDELEO YA ULE MGODI KAMA CASE STUDY HALAFU NDIO UANGALIE HII HOJA YAKO.
 
Lkn hiyo ni acacia yote hapa nimeongelea moja ya mali zao hapa TZ kama vile Mgodi wa Buzwagi pekee, wanaweza kuamua kuuza kwa mtu mwingine na sidhani kama Mgodi wa Buzwagi utakuwa Billions USD!
Accacia ina Operate Tanzania tu na ina migodi mitatu tu Buzwagi, North Mara na Bulyakhulu. Sasa hz nchi nyingine ina exploration tu sio migodi.
 
Kuweka record sawa sawa ni hivi; Acacia/Barrick walikua wanamiliki migodi ifuatayo nchini Tanzania:-
  1. Kahama mining Ltd (sasa Bulyankulu Gold mining)
  2. Buzwagi Gold mining
  3. Tulawaka Gold mining
  4. North Mara Gold mining.
Namba 3 ilichukuliwa na serikali, tumeshindwa kuuendesha huo mgodi na ni kama umefirisika, remember Acacia walitachia kila kitu, hadi magari madogo waliacha, ilifika hatua hadi wakuu wa pale Watanzania wenzetu waliita hadi waganga wa kienyeji kuja kutambika ili tupate Dhahabu. Just the information which you didn't have
 
Kwani Serikali haiwezi kununua Mgodi na kuendelea kuundesha wakati kila kitu kikiwa intact, kama Wafanyakazi na Mikataba yao, na mambo mengine ambayo yapo? Kwa kifupi ni kama kubadilisha mmiliki tu lkn kila kibakie vile vile labda hata kuweka makubaliano na wauzaji kwenye kukodisha expertise n.k.
Kwenye programming kuna kanuni moja: Ukishindwa ku-code program ndogo na rahisi basi kubwa na complex hutaiweza. Kuna vitu vingi tuliwahi kuchukua kwa wazungu tena vidogo vidogo tu na tulishindwa kuviendesha! Je mgodi utawezekana. Fikiri kitu kidogo tu kama shamba! Kuna mashamba tuliwahi kuchukuwa na hatukuweza kuyaendesha!
 
Kwa kuwa tu umeshindwa ku-programm hiyo unayoiita programm ndogo haimaanishi kwamba hauwezi na hautaweza ku-programm, kuna tofauti kati ya kushindwa kitu na kutokuweza kitu kwa maoni yangu!
 
Accacia ina Operate Tanzania tu na ina migodi mitatu tu Buzwagi, North Mara na Bulyakhulu. Sasa hz nchi nyingine ina exploration tu sio migodi.

Nimeongelea mgodi mmoja kama wakiamua kuuza na siyo acacia yote na mali zao zote, na sidhani kama wakiamua kuuza mgodi mmojawapo watadai billions (USD).
 
Ukitaka kujua kwann mashirika ya umma yanakufa tembelea vituo vya mwendokasi

Binafsi naamini ukiamua kutafuta mapungufu popote pale hauwezi kukosa, ni swala la kujiaminisha tu kwamba hauwezi kufanya jambo fulani na itabakia hivyo hadi kiama kuna Watoto wengi tu hawafanikiwi hata Shuleni kwa sababu wameambiwa na Wazazi wao, Walimu au hata marafiki kwamba wao ni wajinga na hakuna kitu wataweza maishani wanaamini na kubakia hivyo maisha yao yote, lkn ukiniuliza mimi Mwendokasi ni success story, mapungufu hayakosekani lkn tumeweza!
 
Nimeona Serikali yetu imepokea Mabilioni ya Fedha ktk kwa Mashirika yetu (hongera kwetu), sasa kwa nini Serikali yetu isinunue mmoja wa Migodi ya Acacia kama vile Buzwagi na kufanya production yenyewe, nina uhakika chini ya usimamizi wa Raisi wetu Magufuli na Waziri Mkuu wetu Majaliwa tutaweza kuuendesha Mgodi wenyewe, kwani mara ya mwisho nilisoma kwamba thamani ya Buzwagi ni kama milioni 300 USD, hii ni kama sawa tu gawio la ktk kwa mashirika yetu kama sijakosea, ...
Mbona hujajiuliza migodi ambayo inamilikiwa na serikali hali yake....ukipata majibu ndo uulize ilo swali lako.
 
Kijana serikali yetu inamiliki mgodi wa Tulawaka kwa asilimia zote.....sasa hivi wapo chaliiiii juu ya mawe

Uzalishaji chengaaaaaa

Wafanyakazi hawajalipwa mishahara miezi mitano.... production hakunaaaaa

Na soon mgodi wataufunga kwa kushindwa kuendesha....japo haitakuwa surprise kwa kuufunga mgodi baada ya kushindwa kuuendesha...Meremeta ulishatu knock out kitambo saaaana!!!

Kuendesha mgodi sio makalio kwamba kila mtu anayo....

Acha mabilioni yaendelee kujenga madaraja
Hahahah umemaliza

Ova
 
Alipewa PAC alifanya nini zaidi ya kuiba hela zetu, kujitajirisha na kuanzisha act? Au unafikiri Zito Kabwe angekuwa an access na fedha yote hii angewekeza chochote zaidi ya kuiba?

Isitoshe pamoja na kununua Ndege, SGR kujengwa Hospitali nchi nzima lkn bado fedha ndefu inaingia Serikalini kama hii ya gawio, hivyo hiyo siyo sababu!
Inawezekana ni mwizi lakini hiyo haimaanishi kuwa mawazo yake ni mabaya.

Alichokiserma ni cha msingi. Tatizo letu ni pariorities zetu.
 
Nimeona Serikali yetu imepokea Mabilioni ya Fedha ktk kwa Mashirika yetu (hongera kwetu), sasa kwa nini Serikali yetu isinunue mmoja wa Migodi ya Acacia kama vile Buzwagi na kufanya production yenyewe, nina uhakika chini ya usimamizi wa Raisi wetu Magufuli na Waziri Mkuu wetu Majaliwa tutaweza kuuendesha Mgodi wenyewe, kwani mara ya mwisho nilisoma kwamba thamani ya Buzwagi ni kama milioni 300 USD, hii ni kama sawa tu gawio la ktk kwa mashirika yetu kama sijakosea, ...
Mikataba ikoje mkuu? labda tungeanzia hapo ili tujue kama inawezekana, kama unavyojua tena mikataba yetu ni ya uwazi mno!
 
Nilimaanisha hela iliyotumika kujengea mgodi ya Buzwagi na siyo thamani ya walichozalisha kuanzia kuanzishwa kwao, hilo sifahamu!
Likini mkuu si tunawadai? Kwa hiyo tufanye negotiations tuwalipe difference au wao ndio watatulipa hiyo difference?
 
Kama nimeamua kuuza basi nitauza, ndo maana nikauliza kama acacia wakiamua kuuza Mgodi wao labda Buzwagi kwa mtu mwingine labda Muhindi ktk India, kwa nini sisi tusiununue kama hiyo hela tunayo?

Kaangalie viwanja vya mpira ccm inavyomiliki vina hali gani ndio ujue kama mnaweza kuendesha mgodi.
 
Back
Top Bottom