Swali kwa mara ya mwisho, Wataalamu wa mining, kwanini Serikali isinunue Acacia?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Nimeona Serikali yetu imepokea Mabilioni ya Fedha ktk kwa Mashirika yetu (hongera kwetu), sasa kwa nini Serikali yetu isinunue mmoja wa Migodi ya Acacia kama vile Buzwagi na kufanya production yenyewe, nina uhakika chini ya usimamizi wa Raisi wetu Magufuli na Waziri Mkuu wetu Majaliwa tutaweza kuuendesha Mgodi wenyewe, kwani mara ya mwisho nilisoma kwamba thamani ya Buzwagi ni kama milioni 300 USD, hii ni kama sawa tu gawio la ktk kwa mashirika yetu kama sijakosea, ...
 
Hahaha mgonjwa ajitibu ajitundikie diripu na dawa juu

haiwezekani

"Ukitaka kula lazima uliwe, wewe unataka kula hutaki kuliwa HAIWEZEKANI" maneno ya rais mstaafu Jakaya Kikwete
 
Bombardier na Dreamliner zingeweza kununua migodi karibu yote. Kupanga ni kuchagua ...!!

Soma andiko la Zitto, nini angefanya kama angepewa madaraka.

Alipewa PAC alifanya nini zaidi ya kuiba hela zetu, kujitajirisha na kuanzisha act? Au unafikiri Zito Kabwe angekuwa an access na fedha yote hii angewekeza chochote zaidi ya kuiba?

Isitoshe pamoja na kununua Ndege, SGR kujengwa Hospitali nchi nzima lkn bado fedha ndefu inaingia Serikalini kama hii ya gawio, hivyo hiyo siyo sababu!
 
Alipewa PAC alifanya nini zaidi ya kuiba hela zetu, kujitajirisha na kuanzisha act? Au unafikiri Zito Kabwe angekuwa an access na fedha yote hii angewekeza chochote zaidi ya kuiba?
Kama wanaoiba awamu hii aise mwizi anahofu kubwa ya kuibiwa kuliko mwema
 
Nimeona Serikali yetu imepokea Mabilioni ya Fedha ktk kwa Mashirika yetu (hongera kwetu), sasa kwa nini Serikali yetu isinunue mmoja wa Migodi ya Acacia kama vile Buzwagi na kufanya production yenyewe, nina uhakika chini ya usimamizi wa Raisi wetu Magufuli na Waziri Mkuu wetu Majaliwa tutaweza kuuendesha Mgodi wenyewe, kwani mara ya mwisho nilisoma kwamba thamani ya Buzwagi ni kama milioni 300 USD, hii ni kama sawa tu gawio la ktk kwa mashirika yetu kama sijakosea, ...
Hakuna pesa iliyopokelewa, ni maonesho tu Yale.
Labda kwa kuwa 7'7 mkuu hakutokea ndio wameamua wayafanye pale.
 
Tunawadai tril 400+ halafu tutoe pesa tena kununua migodi wanayoimiliki!No,mi nasema tukatane juu kwa juu!
Napendekeza pia tuisake migodi ya ACASIA iliyo nje ya nchi na tuitaifishe kufidia deni tunalowadai la tril 400+!Tufanye kama wale waliozui bombardier yetu huko Canada!

Ni aibu unamkamata mwizi wako halafu unaamua kukinunua kile alicho kuibia

Maajabu ya awamu ya tano
 
Thamani ya buzwagi iwe dola mil 300,iweje tuambiwe tunawadai Acasia dola bil 200+?

Nilimaanisha hela iliyotumika kujengea mgodi ya Buzwagi na siyo thamani ya walichozalisha kuanzia kuanzishwa kwao, hilo sifahamu!
 
Hakuna pesa iliyopokelewa, ni maonesho tu Yale.
Labda kwa kuwa 7'7 mkuu hakutokea ndio wameamua wayafanye pale.

Kwa nini tukuamini wewe na siyo Raisi wetu na Viongozi wa Mashirika yetu?
 
Nimeona Serikali yetu imepokea Mabilioni ya Fedha ktk kwa Mashirika yetu (hongera kwetu), sasa kwa nini Serikali yetu isinunue mmoja wa Migodi ya Acacia kama vile Buzwagi na kufanya production yenyewe, nina uhakika chini ya usimamizi wa Raisi wetu Magufuli na Waziri Mkuu wetu Majaliwa tutaweza kuuendesha Mgodi wenyewe, kwani mara ya mwisho nilisoma kwamba thamani ya Buzwagi ni kama milioni 300 USD, hii ni kama sawa tu gawio la ktk kwa mashirika yetu kama sijakosea, ...

Kumiliki kwa sasa hapana, ila serikali imtume Charles Mwijage aende Botswana akajifunze mambo makuu mawili.

Kwanza, akajifunze kwa wenzetu wabotswana wanajiendesha vipi na sera yao ya madini na wanatumia mpango uitwao Tokafala Enterprise Development Programme.

Mradi huu unabadilisha njia mbalimbali za kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa wananchi ambapo wanasaidiwa (mentoring) kutengeneza njia za kutengeneza pesa na kupata wateja.

Mpango huu ulianzishwa mwaka 2014 na mpaka sasa umesaidia kuongea pato la taifa litokanalo na madini kwa asilimia 39.

Pia biashara ndogondogo nyingi zimetengenezwa na kukua kwa asilimia wastani wa 260, nafasi za ajira 1500 migodini na nafasi za moja kwa moja migodini 280.

Pili, Serikali ya Botswana kupitia wizara ya madini na wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda wametengeneza kitu kiitwacho Memorandum of Understanding ambapo wadau wote wa sekta ya madini wakiwemo Anglo American, De Beers Global Sightholder Sales na Debswana wamesaini hio MoU.

Kusaini huko ni katika kupata uhakika au "assurances" kwamba makampuni hayo yatashiriki na kusaidia mpango wa Tokofala Enterprise Development.

Serikali ya Botswana imeweka malengo yake kuhakikisha kwamba ajira zinatengenezwa kupitia maeneo kama hayo ya madini, na sekta binafsi zinashiriki kikamilifu kutimiza malengo hayo.

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya viwanda na Biashara hadi sasa sijaona imekuja na aina hiyo ya kuleta maendeleo kupitia sera kama hizo za wenzetu.

Hawa mawaziri kama Mwijage wanatakiwa wazunguke wasome kwenye mitandao na kutafuta madini mbalimbali yalojaa kwenye sehemu kama hizi za JF kupata kupanua wigo wa uelewa wa masuala muhimu.

Mwisho wa siku raisi akiwasema baadhi ya mawaziri kwamba wamezubaazubaa anakua hakosei kama hakuna jitihada zinazoonekana.
 
kupitia

Kumiliki kwa sasa hapana, ila serikali imtume Charles Mwijage aende Botswana akajifunze mambo makuu mawili.

Kwanza, akajifunze kwa wenzetu wabotswana wanajiendesha vipi na sera yao ya madini na wanatumia mpango uitwao Tokafala Enterprise Development Programme.

Mradi huu unabadilisha njia mbalimbali za kukuza uchumi na kutengeneza ajira kwa wananchi ambapo wanasaidiwa (mentoring) kutengeneza njia za kutengeneza pesa na kupata wateja.

Mpango huu ulianzishwa mwaka 2014 na mpaka sasa umesaidia kuongea pato la taifa litokanalo na madini kwa asilimia 39.

Pia biashara ndogondogo nyingi zimetengenezwa na kukua kwa asilimia wastani wa 260, nafasi za ajira 1500 migodini na nafasi za moja kwa moja migodini 280.

Pili Serikali ya Botswana kupitia wizara ya madini na wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda wametengeneza kitu kiitwacho memorandum of understanding ambapo wadau wote wa sekta ya madini wakiwemo Anglo American, De Beers Global Sightholder Sales na Debswana wamesaini hio MoU.

Kusaini huko ni katika kupata uhakika au "assurances" kwamba makampuni hayo yatashiriki na kusaidia mpango wa Tokofala Enterprise Development.

Serikali ya Botswana imeweka malengo yake kuhakikisha kwamba ajira zinatengenezwa kupitia maeneo kama hayo ya madini, na sekta binafsi zinashiriki kikamilifu kutimiza malengo hayo.

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya viwanda na Biashara hadi sasa sijaona imekuja na aina hiyo ya kuleta maendeleo kupitia sera kama hizo za wenzetu.

Hawa mawaziri kama Mwijage wanatakiwa wazunguke wasome kwenye mitandao na kutafuta madini mbalimbali yalojaa kwenye sehemu kama hizi za JF kupata kupanua wigo wa uelewa wa masuala muhimu.

Mwisho wa siku raisi akiwasema baadhi ya mawaziri kwamba wamezubaazubaa anakua hakosei kama hakuna jitihada zinazoonekana.

Nimesema hivyo kwa maana kwa mfano sasa hivi acacia wanaweza kuamua kuuza Migodi yao kwa watu wengine labda Wachina au sijui Wazungu gani na wao kusepa, sasa kama wanauza kwangu mimi ingawaje sina ufahamu na mambo ya mining niliona ni bora badala ya acacia kuwauzia wengine sisi tungeununua huo mgodi halafu ndo labda tufanye kama unavyosema, kwa maana nafikiri hii Migodi ingawaje sina uhakika hapo ni mali ya acacia, hivyo kama akiuza ina atakayeinunua pia itakuwa ni mali yake na kufanya atakavyo aidha kuuza tena kutengeneza faida na kusepa au vinginevyo!
 
So tuwape hela tunawadai,thamani ya mgodi zidisha Mara 700 ndio inakaribi hela tunayowadai

Kwa mfano kama acacia wakiamua kuuza leo hii Mgodi yao labda Buzwagi sisi tutafanya nini? Je, tuna uwezo wa kuwazuia?
 
Hili la serikali kuendesha mgodi wa Buzwagi ni changamoto kubwa kwani mpaka kufikia mgodi kufungwa maana yake kibiashara haufanyi vizuri yaani gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa siku hadi siku na hivyo kupunguwa kwa faida kama mtakumbuka serikali nadhani chini ya Stamico kama sijakosea inaendesha mgodi wa dhahabu huko Biharamulo.
 
Ungeanza kuuliza stamigold kabla ya buzwagi ambayo hata wachina waligoma kuununua baada ya kugundua ni chenga.
 
Nimesema hivyo kwa maana kwa mfano sasa hivi acacia wanaweza kuamua kuuza Migodi yao kwa watu wengine labda Wachina au sijui Wazungu gani na wao kusepa, sasa kama wanauza kwangu mimi ingawaje sina ufahamu na mambo ya mining niliona ni bora badala ya acacia kuwauzia wengine sisi tungeununua huo mgodi halafu ndo labda tufanye kama unavyosema, kwa maana nafikiri hii Migodi ingawaje sina uhakika hapo ni mali ya acacia, hivyo kama akiuza ina atakayeinunua pia itakuwa ni mali yake na kufanya atakavyo aidha kuuza tena kutengeneza faida na kusepa au vinginevyo!

Nafikiri hawa jamaa kama Acacia wao bado wana access na markets, supply chain na pia wana access na fedha kutoka huko wanakotoka.

Hivyo kama umenielewa Botswana wamekubali kwamba hawa jamaa wako hivyo lakini wakaamua kutengeneza hizo programmes mbili hiyo Tokofala na hiyo MoU ambayo ndiyo muhimu zaidi maana zinawabana wazungu kwa kiasi kikubwa.

Madini sasa hivi nchini Botswana yanadhibitiwa na benki kuu ya nchi hiyo na kila transaction inaangaliwa.

Pia processing plants zipo Gaborone na zinafanywa na raia wazawa na hao wazungu kazi yao ni kupata wanachotaka (kihalali) na kuuza wanakotaka, lakini wanakuwa wamewajibika kulipa kodi stahiki na mirahaba mingine muhimu.

Ila nafasi ya kujichotea tu mchanga kienyeji na kuupakia kwenye makontena kisha kuyasafirisha bila kukaguliwa, huko Botswana hamna hiyo kitu.
 
Back
Top Bottom