Swali kwa mababa wa kambo

Swali kwa mababa wa kambo

Ulikutana na mkeo akiwa tayari ana mtoto anaitwa John. Baada ya kuishi pamoja mkazaa mtoto mkamwita George.

Je, utamwita mkeo mama John au mama George?
Ukimwita mama John inapendeza zaidi maana ndo mtoto wake wa kwanza.

Ukija kwenye uhalisia sidhani kama ni issue kwa mtu anayejiamini na akaamua kubeba single mother.
Mfano lets say umetofautiana na mkeo, na mna watoto 2, mwanaume mwingine akachukua jiko akaweka ndani, unadhani atajali sana anaitwa mama nani na marafiki zake? yeye atajilia tu na kumpa mimba kama wewe ulivyompa. Pengine wakati anamtongoza na kukubaliwa alitumia jina la mtoto wako.
 
Pyeeeeeee unazuga tu, eti tumejihisi kumkosea heshima shemeji mpya kwa hiyo umbea wenu huko ndio uje uulete hapa kwa great thinkers ona ulivyovuliwa nguo hapo kuchutama unataka kukimbia unataka hapo hapo unatamani uzi ungefutwa ila ndio baaasi tena.
😂😂😂😂😂😂
 
Hapo nimekupata mzee baba. Unajua kuna dada mmoja alikuaga na mtoto. Alipotea kwa muda kidogo, sasa hivi karibuni karudi yeye na boyfriend wake mpya wamepanga maeneo ya mtaani.

Wengi hatukua tunamjua huyu shemeji mpya. Juzi tulijumuika nao kupata kinywaji tukawa tumwaita mama wa jina la mtoto wa kwanza. Kuja kugundua kumbe ana boyfriend mpya na wana mtoto dizaini nafsi zikaanza kutusuta kujiona kama tumemkosea heshima yule shemeji mpya.

Ndio maana nikauliza kwa uzoefu wa mababa wa kambo hilo suala limekaaje
Mkuu, sasa kwa hivi vigezo vya heshima vya mtaani kwenu kesho kutwa huyo dada akibadili tena boyfriend akapewa mimba nyingine? si itabidi muwe mnafanya mazoezi ya jina jipya kabla hamjakaa na shemeji? Hahaha, kazi mnayo hapo mtaani.
 
Anakosa usingizi kwa mambo yasiyomuhusu! Unawezaje kujadili jambo ambalo hujawahi pitia kwa wivu mkubwa hivi😁 Mtu aliyeoa bikra na ukoo mzima hakuna single maza ana pesa achafu mpaka za kutulea na koo zetu kutwa kukicha ni singo maza mabikra mpaka anawaota! Hakuwahi tegemea ataokota bikra la mjini nini🤣
Huyo ni zao la single mom niamini mimi dear, ukisoma mambo ya mental health utamuelewa haraka sana huyo kijana na wenzie wanaomsapoti, hakua na utoto mzuri wakati analelewa na single mom, anajihisi yupo hivyo alivyo kwa sababu ya malezi duni alopata ndio akatengeneza chuki kali kwa singo moms wote duniani,
Afya ya akili ipo, hao wagonjwa waleteni kwangu.
 
Kwamba ninyi mlioifurahia hii comment ndo single mama!

Seran leo dada Dr. Mariposa.
Huenda, usingo mama sio ulemavu wala tusi, singo mama ni mwanamke shujaa aliyeamua kusimama na mtoto/watoto wake hadi mwisho, mwanaume mpumbavu hukimbia damu yake na mwanamke shupavu hulea mayai yake ili baadae wakija kua wakina Diamond muanze kujiliza liza mnataka misaada.
 
Very true.
 
Ila pia Kuna single mothers by choice, wanawake wapo kwenye jamii yetu wanaoamua kuwa single kwa chaguzi zao wenyewe sio kwa kukimbiwa, kuna kijana alikuwa anamuomba binti aliyezaa nae amuoe ila binti hakumtaka.

Kijana alipambana kweli ila alifeli, binafsi nina mtu tunafahamiana kwa ukaribu sana yeye alimuacha mume wake akiwa tayari na mtoto.

Mume alipambana kumrudisha kupitia wazazi na vikao ila mpaka leo huyu dada aligoma na ni single mother mpaka sasa.

Kuna jambo tumejiaminisha wanaume kuwa mwanamke anaitaka sana ndoa ila kwa niliyoshuhudia kwenye jamii, wapo wanawake wanaona kuwa na mwanaume ni mzigo tu.
 
Mkuu, sasa kwa hivi vigezo vya heshima vya mtaani kwenu kesho kutwa huyo dada akibadili tena boyfriend akapewa mimba nyingine? si itabidi muwe mnafanya mazoezi ya jina jipya kabla hamjakaa na shemeji? Hahaha, kazi mnayo hapo mtaani.
😀😀😀 ni balaa kwa kweli. Sema sidhani kama atarudia kosa mara mbili
 
Mimi jinsia me mdogo angu. Nimeuliza maana huku mtaani tunakutana na ugumu. Unakuta single mother tushazoea kumwita mama damiani sasa karudi kitaa akiwa na bwana mwingine na mtoto wamezaa tunapata kigugumizi tumwite mama nani
Kwa mfano ww ukimuita kwa jina lolote kati ya hayo, kunatokea tatizo gani
 
Huenda, usingo mama sio ulemavu wala tusi, singo mama ni mwanamke shujaa aliyeamua kusimama na mtoto/watoto wake hadi mwisho, mwanaume mpumbavu hukimbia damu yake na mwanamke shupavu hulea mayai yake ili baadae wakija kua wakina Diamond muanze kujiliza liza mnataka misaada.
Toa hiyo title ya Dr.. Unawaabisha wenye taaluma yao.
 
Ila pia Kuna single mothers by choice, wanawake wapo kwenye jamii yetu wanaoamua kuwa single kwa chaguzi zao wenyewe sio kwa kukimbiwa, kuna kijana alikuwa anamuomba binti aliyezaa nae amuoe ila binti hakumtaka. Kijana alipambana kweli ila alifeli, binafsi nina mtu tunafahamiana kwa ukaribu sana yeye alimuacha mume wake akiwa tayari na mtoto. Mume alipambana kumrudisha kupitia wazazi na vikao ila mpaka leo huyu dada aligoma na ni single mother mpaka sasa.
Uko sawa kabisa dia, hapo hapo by choice kuna wengine waliamua kuzaa baada ya kuona ndoa hazipo, umri unasonga kabla hajafika menopause anazaa mtoto mmoja au wawili anatulia, sasa sisi WaTz na ushamba wetu bado tuna mawazo ya kizamani yote hii ni watu kutokusafiri akili zimeganda sehemu moja tu
 
Sasa kama una majibu yako unayoyataka ww mwnyw bc usingeanzisha uzi, ungekaa nao ghetto kwako ujadiliane na vikombe
Mkuu kwani ukijibiwa, ukataka kujua zaidi ni kosa? Jibu alilonipa jamaa ni refu sana sikujua nini exactly anataka kusema ndio maana nikaomba jibu ambalo ni short and clear
 
😀😀😀 ni balaa kwa kweli. Sema sidhani kama atarudia kosa mara mbili
Mkuu, kwa jamii ya leo kama ilivyo kwa baadhi ya wanaume kuzaa na wanawake tofauti hawaoni ni kosa wapo pia wanawake kuzaa na wanaume tofauti hawaoni kama ni kosa. Jamii hii si ya enzi zetu na mama zetu. Zile enzi za ukipata mimba kabla ya ndoa ni laana.
 
Ila pia Kuna single mothers by choice, wanawake wapo kwenye jamii yetu wanaoamua kuwa single kwa chaguzi zao wenyewe sio kwa kukimbiwa, kuna kijana alikuwa anamuomba binti aliyezaa nae amuoe ila binti hakumtaka.

Kijana alipambana kweli ila alifeli, binafsi nina mtu tunafahamiana kwa ukaribu sana yeye alimuacha mume wake akiwa tayari na mtoto.

Mume alipambana kumrudisha kupitia wazazi na vikao ila mpaka leo huyu dada aligoma na ni single mother mpaka sasa.

Kuna jambo tumejiaminisha wanaume kuwa mwanamke anaitaka sana ndoa ila kwa niliyoshuhudia kwenye jamii, wapo wanawake wanaona kuwa na mwanaume ni mzigo tu.
Single babaz na single mamaz tulionao mtaani katika kizazi cha vijana wa sasa wengi wao ni kwa sababu ya ujinga wa kuweka nyege na tamaa mbele ya akili na mipango.

Mimba sio malaria ambayo inakuja kwa kushtukiza.
 
Back
Top Bottom