Hakuna alosema ni kundi jema, mtu kuwa na mtoto sio kitu cha ajabu na wala si jambo jioya hapa duniani, walikuwepo na wataendelea kuwepo no matter what! Ila udhalilishaji na kuwatukana sana ndio kitu kinashangaza! Mtu kuwa single mama sio kuwa mlemavu, wanaume mnachukulia hili jambo kama la makusudi kwa kila mwanamke! Wewe hapo unaweza ukawa unamuamini sana huyo mkeo siku akiamua kukupiga tukio kw akisirani ukamuacha tayari atakuwa single mama, siku ukifa lazima atabaki singo mama, unasemaje asiolewe na wanaume wenzio?
Ni kwanini mnahisi kila mtu anaenjoy kuwa hivyo? Na hata kama kuna kundi linaenjoy ni kosa kisheria? Kuna kundi kunwa lina majeraha kisa nyie haohao wanaume na ndiomaana wanaamua kujikwamuankiuchumi kisha kuzaa na yeyote na kulea wenyewe, sio kila mwanamke mwenye mtoto ni punguwani, sio kila aliyezalishwa ni malaya au hana akili! Sio kila singo mama hana maisha au pesa! Sijui unanielewaa???
waacheni watu wawe huru acheni kuwapangania wanaume wenzenu maisha mnawapanikisha mwisho wa siku wanaoshi kujioa! Huoni hizi kampeni unazowapigia singo maza kutoolewa ungetumia kukomalia ushoga upungue ungeokoa vijana wangapi? Instead unabebelea mambo yasiyo na maana mtu kaamua kuoa mwanamke mwenye mtoto yakimkuta ndio aanze kutusi watu? Tabia zake chafu zinamhusu vipi huyo mtoto? Au ukizaa kuna hormone ya umalaya na kutojielewa inazalishwa?