Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Kuabudu ni uhuru wa mtu kama hutaki kuangalia wengine wakiabudu kupitia TBC wewe zima TV yako au badili channel.

Huo uwezo wetu wa kuvumilia na kuchukuliana kama tulivyo ndio umetuwezesha kufikisha miaka 60 ya uhuru msidhani ni jambo jepesi tu kama kwenda chooni asubuhi baada ya kuamka.

Nchi yetu haina dini ila kila mtu anayo dini yake na anao wajibu wa kuheshimu dini ya mwenzake.
 
Umekwenda nje ya hoja iliyo mezani. Tunajadili hoja hii:

1. Matakwa ya kikatiba ya kutenganisha dini na dola yanaweza kutekelezwa kwa njia kuu mbili: American style or Germany style.

2. German style inabagua baadhi ya dini na kulazimisha baadhi ya walipa kodi kubeba mzigo usiowahusu; wakati American style haina mapungufu hayo.

3. Kwa hiyo, twende na American style?

Kwa hiyo, utaona kuwa hayo mambo ya dansi,mziki,ngoma,makala za biashara,kilimo,ujasiriamali, sio sehemu ya hoja hii.

Kama nasahihisha karatasi ya majibu ya mtihani wa mwanafunzi ningekwambia: Jibu swali uliloulizwa.
 

Hapana. Habari ya "kuzima TV" haina nafasi katika hoja hii kwa kuwa TBC ni civi space.
Yaani TBC ni eneo ambalo linapaswa kuwa huru dhidi ya kanuni na mienendo ya kiparokia (particular phenomena), ambayo ni kinyume cha kanuni na mienendo mtambuka (universal phenomena).
 
Kwanza hizo sehemu zinazotumika kiarabu mbona ni sehemu chache sana nashangaa kwanini hii nayo ni hoja humu!
Hoja inayohusu lugha za kiarabu na kilatini kutumika kwenye TV ya Taifa sio tatizo dogo kwa sababu kuu tatu.

1. Jambo hilo linakula nafasi ya lugha ya Taifa ambayo ni nyenzo muhimu ya kujenga utaifa.

2. TBC wanao wajibu wa kukuza umoja wa Taifa kwa kutumia lugha ya Taifa, na ndio maana wametofautisga kati ya TBC1, TBC2, etc.

3. Ukoloni wa lugha ni tatizo lisilovumulika.
 
Naona unachanganya mambo. Hebu nirekebishe hivi:

1. Chombo chao cha habaro: KIna nani? Katoliki wana Tumaini TV, KKKT wana Upendo TV, Waislamu wa Iman TV, Watanzania wote wana TBC. Kwa hiyo, masuala ya kisekta yanapaswa kuonyeshwa kwenye TV za kisekta, na masuala ya kitaifa kwenye TV ya kitaifa. Hiyo ndiyo maana ya civic space.

2. Utoaji wa huduma za jamii kama vile afya na elimu kupitia ushirika wa serikali na mashirika ya dini: Dini zinasajiliwa MOHA, shule zinasajiliwa Wizara ya Elimu, AZAKI zinasajiliwa Wizara ya Ustawi wa Jamii. Kwa hiyo, huduma za jamii kama vile afya na elimu sio kazi ya msingi ya taasisi za dini. Zinaweza kufutiwa leseni za shule na hospitali na kubakiza leseni ya MOHA.
 
Unajua lolote kuhusu ibada za kiisalamu? nakuuliza hivyo kwa sababu huko kutumia kiarabu kwenye ibada ni sehemu ya ibada yenyewe kwa maana inatakiwa yatamkwe hayo maneno kwa kiarabu na si kwa lugha nyengine hivyo si suala la ukooloni wa lugha kama unavyofikiri, na hizo sehemu zenye kulazimika kutamka maneno kwa kiarabu ni sehemu ndogo sana tena zengine hata huwasikii husoma kimoyo moyo sasa ndio maana nashangaa hili suala linakuaje ni hoja humu? labda ingekuwa wanatoa mawaidha kwa kiarabu tu hapo sawa tungejadili lakini sio ibada usifananishe ibada ya waislamu na wengine kuna tofauti ungezingatia hilo usingekuja kuleta hii hoja.
 
Ila wewe kuwa mkristu au muislamu kwa kuwa wazazi wako wanatoka kwenye imani hizo ni fresh tu au sio
 
TBC haipaswi kuwa jukwaa la dini yoyote?
 
Na vile vipindi vinavyoonesha tamaduni za makabila yetu navyo Tv yao ni ipi?
 
Wote tupinge kwa nguvu zote kuiingiza dini yoyote katika masuala ya serikali. Kuna faida kubwa zaidi serikali kutochanganywa na dini kuliko hasara itokanayo na dini kuunganika na serikali.
 
Siku zote nitapinga kuingiza mambo ya dini yoyote katika mifumo, taasisi na shughuli za serikali.
 
Nimekuwa nikipinga kuchanganya shughuli za kidini kwenye shughuli, mifumo na taasisi za serikali bila kujali mfalme ni nani.
 
Taasisi za serikali kutumika kama majukwaa ya dini ni matumizi mabaya sana ya pesa za walipakodi. Wote tupinge huu utaratibu.
View attachment 1792752
Rubish

Dini zote zinamhubiri Mwenyezi Mungu, hao walioko kwenye hilo taifa ni wacha Mungu, na hicho chombo ni chao kwakuwa kinaendeshwa kwa kodi zao

Mleta mada nenda kakate gogo kwanza kuna zigo linakusumbua
 
Vyombo vya serikali visitumike kama jukwaa la dini yoyote.
...na ukashangaa..maana ulifikiri hao waislam hawana haki ya kutumia hiyo stesheni ya Luninga..ila wakristo tu siku ya Jumapili? Nafikiri ungeyaacha kama yalivyo!
 
Ila wewe kuwa mkristu au muislamu kwa kuwa wazazi wako wanatoka kwenye imani hizo ni fresh tu au sio
Wapi nimesema mimi ni mkristo au muislamu kwa sababu tu wazazi wangu ni wakristo/waislamu? Mimi hadi hapa sasa nafuata imani niliyonayo kwa hiari yangu na sababu zangu na sio et kwa sababu ya kufuata wazazi wangu. Sasa nyie mnafuata imani kisa wazee wenu huko walikuwa na hizo imani sasa hapo mnafuata imani au hao wazee?
 
Tuache kupoteza muda na mambo ya kubalance. Taasisi, mifumo, idara na shughuli zote za serikali zisitumike kama jukwaa la dini YOYOTE.
 
Sio sawa kabisa.Naunga hoja mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…