Swali kuhusu bosi mpya wa TPDC

Swali kuhusu bosi mpya wa TPDC

Tatizo wana JF mnapost mada isiyokuwa na chanzo cha habari (source). Huyo Boss mpya wa TPDC ni nani? Mimi namjua Yona Kilighane kama ameingia Mzungu tueleze mtoa mada.

Kilagane muda wake uliisha Huyo jamaa ni Product ya JK katika misele yake ya uGHAIBUNI ndo kamleta
 
MD wa TPDC bado hana tatizo lolote ni mchapakazi mzuri sana tena ni mzalendo aliekubali kuacha kazi yenye malipo mazuri USA na kurudi Tanzania kwenye maslahi duni na mfumo mbovu kiutendaji tatizo lililopo ni watendaji wizarani na tpdc bado wana ile govt mentality ya bussiness as usual
 
Kumbe ni majungu at work...kwi kwi kwi...
wenzenu walipokuwa wanabukuwa nyie mlikuwa wapi?
 
nchi yangu naiona inazidi kuzama kwa kukosa viongozi wazalendo na wanaowajali waliowaweka makazini.
 
Watu wanapost vitu vınavyowajia vichwanı mwao wala hawajali.Dola bil 25,labda alimaanisha dola ya Zimbabwe au Angola.
Ni kweli LNG plant ni zaidi 20 billion US $, STATOIL na BG ndio watatoa hiyo pesa, sawa na bajeti nzima ya Tz kwa 2.5 years. Prof Muhongo alivyokuwa anasema haitaji madalali alikuwa anamaanisha, sema Tz kuna ma nyumbu wengi wakadakia hata wasivyovijua
 
TPDC walileleka maombi EWURA kupandisha mishahara mkurugenzi mkuu tsh 36,000,000/= kwa mwezi, mkurugenzi msaidizi tsh 28,000,000/= karani tsh 5,400,000/= so uaishangai. Umenisoma braza
 
Kuna mtu yuko idara ya sheria TPDC anapenda majungu sana,atawasumbua mno
 
swala la hawa wakurugenzi kuwekwa kikada tuliliweka vema kwenye rasimu ya warioba, ila kwa nguvu zote wanaCCM walikata mauno bungeni kuhakikisha rasimu ya chenge inafutilia mbali maoni yenye tija juu ya nyadhifa hizi.
 
Hivi huyu jamaa analipwa mshahara kiasi gani?

Na inawezekana vipi akawa anatumia milioni 70 za walipa kodi kila mwezi kwenda kutazama familia yake USA na kurudi?

Kwa nini anatumia muda mrefu zaidi USA kuliko ofisini kwake?

Cha ajabu toka apewe hiyo kazi hakuna lolote la maana alilolifanya mradi wa mtambo wa LNG wa dola bilioni 25 na ushee huko Mtwara ushakwama kwa sababu watu wamekula pesa za viwanja na kesi za ajabu ajabu zimefunguliwa. Mbaya zaidi huyu jamaa amebatizwa jina pale ofisini kwake wanamwita CAPTAIN AMERICA na wengine wanamwita MSAFIRI. Hivi haoni wenzake kama bosi mpya wa TCRA wanavyofanya kazi?

Halafu magufuli ana tafuta wachawi wakati wapo wazi wazi.

Una uhakika na ulichokiandika au umekurupuka tu?
 
Hivi una uhakika ni hicho kiasi cha pesa ulichoandika? USD 25 billions? Unajua mradi wa kujenga reli Standard Gauge kwa kilometer 2,500 ni USD 7 billions? Hiyo LNG plant tu ndio iwe USD 25 billions? Kweli?
 
Mpeni muda aonyeshe uwezo wake. Kwa mchechu mlianza hivi hivi, lakini leo NHC ndilo shirika la umma tajiri kupindukia. Mpeni muda huyu kijana.
 
Kumbe ni majungu at work...kwi kwi kwi...
wenzenu walipokuwa wanabukuwa nyie mlikuwa wapi?

katika watu ninawadharau nchi hii ni wasomi, mingi ya mikataba ya kipuuzi imeingiwa na hao wasomi. Hebu jaribu kuangalia wasomi wengi wanapenda kuajiriwa na mengi ya taasisi/mashirika wanayaendesha kwa hasara. Unakuta mtu ni msomi lakini anachojua ni kujivuna na kuandika proposal nzuri ili wazungu watoe pesa. Lakini kwa upande wa pili mingi ya miradi ama biashara zenye mafanikio zinaendeshwa na watu wenye elimu ya wastani tu. Sasa kama kweli kinachosemwa kuhusu huyo bwana kama kina ukweli hapo kuna tija? Unaweza kuta analipwa kiasi hicho cha pesa lakini output ni nusu ya malipo anayopata.
 
Mpeni muda aonyeshe uwezo wake. Kwa mchechu mlianza hivi hivi, lakini leo NHC ndilo shirika la umma tajiri kupindukia. Mpeni muda huyu kijana.

Sawa Manyerere, hilo NHC ni shirika la umma kwa ajili ya wananchi wa kawaida au matajiri? Ama wanaoishi humo ni wale Magufuli amepiga stop safari zao za nje mpaka atoe kibali? Wakati nakua niliishi kwenye nyumba za NHC, wakati ule kweli lilikuwa shirika la umma, leo hii mwananchi wa kawada ambao ndio wengi sidhani kama kuna mwenye uwezo wa kuishi nyumba hizo. Kwanini nyie waandishi wa habari msitumie nafasi yenu kuwaambia hao jamaa wajenge nyumba za watu wa kipato cha 100,000- 300,000 ambao ndio wengi? Sikatai NHC kujiendesha kibiashara ila napata ukakasi wanapojiita shirika la umma wakati wengi wa wananchi tunajikunyata kwenye nyumba za wajanja hata wasiolipa kodi za majengo.
 
Cjui kwa nini tunawaajiri diaspora wakati tuna wataalamu wengi tu wa ndani. Kwani wakati huo akisoma, alikuwa peke yake darasanai? swala la uzoefu sio kigezo..jamaa tayari anaakili za kimagharibi...sio raisi kujitolea wa Taifa tena... Tungeachana naye na kutafuta mtu mwingine ambaye hataligharimu taifa, na kodi za wananchi kama ilivyo kwa Dr. Mataragio..
 
Hivi una uhakika ni hicho kiasi cha pesa ulichoandika? USD 25 billions? Unajua mradi wa kujenga reli Standard Gauge kwa kilometer 2,500 ni USD 7 billions? Hiyo LNG plant tu ndio iwe USD 25 billions? Kweli?

Shirikisha ubongo wako kufikiria.

Unaweza pia kutumia google kupata taarifa ya gharama nchi nyingine zilizoingia kujenga LNG Plant.
 
Watu wanapost vitu vınavyowajia vichwanı mwao wala hawajali.Dola bil 25,labda alimaanisha dola ya Zimbabwe au Angola.

Nadhani hajakosea. Mradi wa LNG ni USD billioni ishirini na tano.
 
Back
Top Bottom