Swali kuhusu bosi mpya wa TPDC

Swali kuhusu bosi mpya wa TPDC

Kwa nafasi ya huyu jamaa ina amke sense kwasababu kampuni za kuwekeza nyingi ziko US, Canada na Europe sasa deal atafanyaje bila kusafiri.
 
Na imani ulimaanisha billion 25 za kitanzania na sio dolla billion 25
Tanzania says LNG project could cost up to $30 bln - CNBC Africa
Watu wanapost vitu vınavyowajia vichwanı mwao wala hawajali.Dola bil 25,labda alimaanisha dola ya Zimbabwe au Angola.
Tanzania says LNG project could cost up to $30 bln - CNBC Africa
Una uhakika na ulichokiandika au umekurupuka tu?
Tanzania says LNG project could cost up to $30 bln - CNBC Africa
Hivi una uhakika ni hicho kiasi cha pesa ulichoandika? USD 25 billions? Unajua mradi wa kujenga reli Standard Gauge kwa kilometer 2,500 ni USD 7 billions? Hiyo LNG plant tu ndio iwe USD 25 billions? Kweli?
Tanzania says LNG project could cost up to $30 bln - CNBC Africa
safari zimepigwa marufuku rasmi
Alhamdullillah
Kwa nafasi ya huyu jamaa ina amke sense kwasababu kampuni za kuwekeza nyingi ziko US, Canada na Europe sasa deal atafanyaje bila kusafiri.
Narudia haendi hizi safari kikazi anakwnda kutazama familia yake huko Marekani kwa pesa za walipa kodi.
 
Ndugu unakula mezani pake nini maana huu Ujinga ulioandika nitashangaa ikiwa hushiriki japo makombo yake...Kwaakili yako kusafiri ndio kufanyakazi?....alaaniwe Mchina kule vitu vya electronic vya bei rahisi kila MTU anatumia kuandika bila kufikiria

Kwa wqtu mliozoea quantity hili hamuwezi kulielewa, kukaa muda mrefu ofisini sio kigezo cha ufanisi wa kazi, unaweza kwenda ofisini mara 3 kwa wiki na ukawa umefanya kazi kubwa kuliko alieenda siku 5.

Hapa ishu ni ubora na ufanisi wa kazi, anafanya kazi kisayansi, mambo ya kiswahili ya kukaa muda mrefu ofisini unapiga umbea na kuchat hana.

Ameshika senior position kwenye mashirika makubwa ya dunia, wewe unaetaka awepo ofisini muda wote ili iweje?
 
Hivi huyu jamaa analipwa mshahara kiasi gani?

Na inawezekana vipi akawa anatumia milioni 70 za walipa kodi kila mwezi kwenda kutazama familia yake USA na kurudi?

Kwanini anatumia muda mrefu zaidi USA kuliko ofisini kwake?

Cha ajabu toka apewe hiyo kazi hakuna lolote la maana alilolifanya mradi wa mtambo wa LNG wa dola bilioni 25 na ushee huko Mtwara ushakwama kwa sababu watu wamekula pesa za viwanja na kesi za ajabu ajabu zimefunguliwa.

Mbaya zaidi huyu jamaa amebatizwa jina pale ofisini kwake wanamwita CAPTAIN AMERICA na wengine wanamwita MSAFIRI. Hivi haoni wenzake kama bosi mpya wa TCRA wanavyofanya kazi?

Halafu Magufuli ana tafuta wachawi wakati wapo wazi wazi.
Asante kwa taarifa.
 
Kwa wqtu mliozoea quantity hili hamuwezi kulielewa, kukaa muda mrefu ofisini sio kigezo cha ufanisi wa kazi, unaweza kwenda ofisini mara 3 kwa wiki na ukawa umefanya kazi kubwa kuliko alieenda siku 5.

Hapa ishu ni ubora na ufanisi wa kazi, anafanya kazi kisayansi, mambo ya kiswahili ya kukaa muda mrefu ofisini unapiga umbea na kuchat hana.

Ameshika senior position kwenye mashirika makubwa ya dunia, wewe unaetaka awepo ofisini muda wote ili iweje?

Ila wadanganyika huwa nawashangaa kwenye kuiga mambo ya wazungu kwenye matumizi kuliko kazi yaani kwakuwa Mzungu anafanya hivyo nanyie mnacopy kwa tija gani mnayozalisha kama sio kufisadi Taasisi mnazozisimamia..kusafiri kungekuwa na maana kwenye Nchi zetu hizi kwa safari alizofanya JK naamini tungeifunika hata Marekanai kwa maendeleo....Acheni kukariri....daah..!!! Wakati mwingine huwa nasema kuwa mtu mweusi ni kama Laana flan hivi
 

Sasa wewe mtumishi wa TPDC huwa Hanna vikao ofisini kwenu? Hujui anuani ya aliyemleta hapo? Au kama vipi nenda kasome uchukue cheo chake,umetuchosha,
 
Magu njoo uokoe jahazi huku
 
Mataragio ameingia kwa matarajio makubwa, hakuna GM aliyetokea kama huyu tpdc, jamaa ni very smart
 
Tatizo wana JF mnapost mada isiyokuwa na chanzo cha habari (source). Huyo Boss mpya wa TPDC ni nani? Mimi namjua Yona Kilighane kama ameingia Mzungu tueleze mtoa mada.
Huyo yona killlagane alisha stafu kiongozi wamemuweka mwingine sasa
 
Mpeni muda aonyeshe uwezo wake. Kwa mchechu mlianza hivi hivi, lakini leo NHC ndilo shirika la umma tajiri kupindukia. Mpeni muda huyu kijana.
Mmmh, litapigwa mnada soon, NHC naitabiria kuwa kama THB au ATCL katika miaka 5 ijayo.
 
MD wa TPDC bado hana tatizo lolote ni mchapakazi mzuri sana tena ni mzalendo aliekubali kuacha kazi yenye malipo mazuri USA na kurudi Tanzania kwenye maslahi duni na mfumo mbovu kiutendaji tatizo lililopo ni watendaji wizarani na tpdc bado wana ile govt mentality ya bussiness as usual
Wabongo tuna kazi kweli!
 
Acha ujinga wako kwani kazaliwa wapi
Swala la maslahi ni gumu sana. Hakuna aneyejua alikotoka alikuwa analipwa hela sh ngapi. Atakama ni mtanzanai siku zote mtu anapoitwa kufanya kazi swala la maslahi ni muhimu. Otherwise alikuwa na haki ya kukataa. Kwa kuwa hakuna mwenye uhakika ya kuwa amesomeshwa na serikali ya Tanzania. Hakuna mtu wa kumlaumu
 
huyu mtoa mada nadhani hata exchange rate kwake ni tatizo.
 
It is saddening for a concerned citizen not to know the cost of the LNG project. Especially one with access to information such as the internet. This goes to show how ignorant we are with our national matters -- na hii gas ndiyo tunajisifia nayo.

Mtu atasema huwezi kujua kila kitu, kweli, lakini kutokujua a $20 bn project (ambayo news zake ni 2+ years now) ni kuonyesha tuna taifa la watu wasiojua mambo wanayopaswa kujua. Hatari zaidi ni vipi wale waliopo vijijini?

Si ajabu kuitwa malofa na wapumbavu. Si ajabu kwa mgeni kuja na suit na kuondoka na $$$ za kutosha.

Back to the OP, kama kweli MD wa TPDC analipwa TZS 36m per month, I would say he is underpaid or he is a true patriot.. or incompetent and did not deserve that post in the first place.

Kupata mtu mwenye experience, skills and competence ya kuwa MD TPDC na kumlipa US $18,000 kwa mwezi ni sawa na mshahara wa assistant manager in a private Oil & Gas company.

Oot, @HNIC kama kweli the whole LNG project imekwama, will Dangote make a profit out of his cement? Was he not eyeing the LNG project and not the common mwananchi?
 

MAAJABU KUMI YA SHIRIKA LA TPDC CHINI YA KAULI MBIU-HAPA KAZI TU-PART 1.


1. Ni shirika pekee ambalo ajira zake zimekuwa zikifanywa kwa upendeleo mkubwa bila kujali kwamba kuna vyombo vya dola vinavyoweza kubatilisha wala kukemea upuuzi wao. Ni hivi majuzi tu shirika limetangaza nafasi za kazi za mameneja wa vitengo mbali mbali lakini ajabu na kweli waombaji kutoka nje ya TPDC waliopata nafasi za kazi si zaidi ya watatu kati ya nafasi zaidi ya 15. Hata hao waliopata, wawili kati yao wameshikwa mkono na ‘wakubwa’ wa shirikani. Vigezo vilivyowekwa kwenye tangazo ilikuwa ni kuwahadaa watanzania kwani havikufuatwa wakati wa zoezi zima. Hii ni aibu kwa Shirika na Wizara ya Nishati na Mamlaka zinazosimamia ajira nchini.


2. Ni shirika pekee la Umma linaloweza kuajiri bila kuomba kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais Utumishi Kama taratibu zinavyotaka. Mfano, nafasi hizo za managers zimetangazwa na kuajiriwa bila kuwa na kibali cha ajira kutoka mamlaka husika. Anayebisha aende kwenye mamlaka za ajira akathibitishe hili. Hii ni kashfa kubwa ya matumizi mabaya ya ofisi.



3. Ni shirika pekee ambalo linapuuza taaluma na baadala yake kujikita kwenye uzoefu tu wakati wa kuajiri watumishi wake. Ni aibu kwa Shirika kubwa kama TPDC kuamua kuajiri mtu kwenye nafasi nyeti tena ya manager wa hesabu na fedha bila kuthamini taaluma kama CPA ambacho kilikuwa kigezo cha lazima kwa mujibu wa tangazo. Kama waombaji wenye sifa walijitokeza, kuna sababu gani ya kuajiri mtu mwenye sifa za mashaka? Aibu aibu aibu!


4. Ni shirika pekee ambalo linaweza kuajiri baadhi ya watumishi wake bila kuwafanyia vetting. Taratibu zinataka watumishi wote ilimradi wanapewa majukumu mapya (tena hawa wanapewa majukumu makubwa zaidi na ni nafasi za uteuzi). Unajiuliza katika nchi hii inayofuata misingi ya haki na utawala bora, kwanini watumishi waajiriwe kwenye nafasi kubwa bila kufanyiwa vetting? Haya ni makusudi yenye nia ya kulipaka shirika matope. Waliofanya hivi wanajua walikuwa na malengo gani….waulizeni labda wanayo majibu! Mkurugenzi Edith Semtengu na meneja wake Rwechungula waeleze walitumia kanuni gani katika kufanya haya.








5. Ni shirika pekee ambalo Mkurugenzi wa Utawala kwa kushirikiana na Kaimu Meneja wa HR ambao ni marafiki wakubwa wanaweza kujiamulia kupanga na kuidhinisha viwango vya mishahara ya Mameneja bila kupata idhini ya Bodi ya Wakurugenzi, Msajili wa Hazina au Mkurugenzi Mtendaji. Hakuna Waraka wowote wa Mshahara unaoonyesha viwango vya mishahara wanavyotakiwa kulipwa Mameneja kwa sababu vyeo hivi havikuwahi kuwepo shirikani. Kama waraka upo basi wauonyeshe. Wawili hawa waulizwe wamepata wapi kibali cha kupanga mishahara ya mameneja? Itakumbukwa kuwa vigogo hawa wa idara ya Utawala wamekuwa wakishirikiana hata kuwahamisha watumishi shirikani hasa wale ambao hawaelewani nao. Ni kweli mamlaka haziyaoni haya?


6. Ni shirika pekee ambalo nafasi za ajira zinaweza kutangazwa na baadaye nafasi mojawapokuondolewa ili kumnufaisha mmojawapo wa waombaji. Wakati wakurugenzi wote waliomba kazi na kufanya usaili, Mkurugenzi mmojawapo wa shirika ameendelea kutesa bila kufanya usaili. Bado tuendelee kuamini kwamba ni shirika lenye fursa sawa kwa wote? Ukihoji unahamishwa.



7. Ni shirika pekee ambalo mshindi kwenye usaili anakosa nafasi na nafasi yake kwenda kwa mteule mwingine hata kama hakushinda usaili kwa kutumia kigezo cha uzoefu. Bora mwombaji ashinde usaili lakini ashindwe kwenye vetting, hapo hakuna shaka. Lakini hapa hadithi ni ni tofauti kabisa. Swali rahisi la kujiuliza hapa ni kwamba, kama uzoefu kilikuwa ni kigezo kwanini mtu aitwe mpaka kwenye usaili wa hatua za mwisho?Je, si ilikuwa busara kumuondoa mtu huyo ili kuwaacha wenye sifa sawa wapambane mpaka mwisho ili mshindi apate haki yake? Hiyo ndiyo TPDC bwana.



8. Ni shirika pekee la Umma ambalo haliogopi mamlaka kwani limeendelea kuajiri mameneja hawa hata bila kuwa na approved scheme of service kwa nafasi za managers. Unawezaje kuajiri bila kuwa na nyenzo hii muhimu? Msajili wa Hazina na Utumishi wa Umma wapo lakini labda hawana taarifa. Wakati haya yakitendeka, Mkurugenzi wa Utawala na Kaimu Meneja wa HR wameendelea kuchapa kazi bila kuona kama wanatenda ‘uhalifu’. Hakika hii ni kali kuliko.



9. Ni shirika pekee ambalo masuala ya ajira kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakifanywa na watu wasiokuwa na uzoefu wa Utumishi kwenye mashirika hasa ya mafuta na gesi. Maamuzi yote hayo yamekuwa yakifanywa kwa kiasi kikubwa na Mkurugenzi wa Utawala na Kaimu Meneja HR ambao walishirikiana kuwaondoa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha na Kaimu Meneja HR waliokuwa wanafanya kazi zao kwa weledi mkubwa. Wamebaki na wameachwa wakiendelea kulihujumu shirika kwa muda sasa. Hii ni hatari kwa ustawi wa utumishi wa umma.



10.Ni shirika pekee ambalo, tunaamini TAKUKURU na vyombo vingine vimeshindwa kulifikia labda kutokana na kuwasubiri Mh. Rais au Waziri Mkuu wafike ili kujionea wenyewe. Ni wazi uchunguzi ukifanyika yatabainika mengi zaidi ya haya. Je huu ni uungwana?


Watu walisema lakini wakawa ignored

nasubiri PART 2
 
Napita tuu waungwana lakini kaeni mkao wa kula kuna mambo mazito sana kuhusu yanayoendelea TPDC na huyu bosi wo mpya

The same applies to you Mheshimiwa Rais

Admin (wapatieni wachangiaji ruhusa ya kubadili kichwa cha thread) by that I mean thread starter should have permission to edit the thread header.
 
nitarudi baadae wakuu
 
Hivi huyu jamaa analipwa mshahara kiasi gani?

Na inawezekana vipi akawa anatumia milioni 70 za walipa kodi kila mwezi kwenda kutazama familia yake USA na kurudi?

Kwanini anatumia muda mrefu zaidi USA kuliko ofisini kwake?

Cha ajabu toka apewe hiyo kazi hakuna lolote la maana alilolifanya mradi wa mtambo wa LNG wa dola bilioni 25 na ushee huko Mtwara ushakwama kwa sababu watu wamekula pesa za viwanja na kesi za ajabu ajabu zimefunguliwa.

Mbaya zaidi huyu jamaa amebatizwa jina pale ofisini kwake wanamwita CAPTAIN AMERICA na wengine wanamwita MSAFIRI. Hivi haoni wenzake kama bosi mpya wa TCRA wanavyofanya kazi?

Halafu Magufuli ana tafuta wachawi wakati wapo wazi wazi.

Kumekuwa na mjadala kuhusu ukubwa wa malipo ya baadhi ya Wakurugenzi Wakuu (CEO) na Wakurugenzi wa kawaida (average executives) katika mashirika ya kitanzania (ambayo yanapaswa kujiendesha na ikiwezekana kuleta faid), ukilinganisha na wafanyakazi wa kawaida (average worker).

Katika pitapita yangu nimeona discussion paper ya mwaka 2008 waliyoandika Ebert, Torres na Papadakis wa taasisi yenye mamlaka kamili, International Institute for Labour Studies, iliyo chini ya International Labour Organization (ILO). Chapisho hili linaitwa Executive Compensation: Trends and policy issues.

Makala hii ilikuwa inatazama mwenendo wa malipo ya wakurugenzi kwa nchi sita (6) duniani, ambazo taarifa zake zilikuwa wazi – Afrika ya Kusini, Hong Kong (China), Ujerumani, Australia, Uholanzi, Ujerumani na Marekani.

Kwa ufupi chapisho linasema ingawa kuna tofauti ya mishahara kati ya nchi na nchi, lakini Wakurugenzi wanalipwa mishahara mikubwa ukilinganisha na wafanyakazi wa kawaida.

Bila kujali marupurupu mbalimbali, Wakurugenzi (CEO na average executives) walioneshwa kulipwa mara 71 hadi 183 ya malipo ya mfanyakazi wa kawaida.

Ukiongeza marupurupu, malipo yao yaliongezeka na kuwa mara 103 hadi 521 ya malipo ya mfanyakazi wa kawaida!!!

Wakurugenzi waliopo Afrika ya Kusini na Hong Kong (China) walionekana kulipwa kidogo, ukilinganisha na wenzao walioko Marekani, lakini hata hivyo wakurugenzi wa nchi hizi walikuwa wakilipwa mara 48 hadi 148 ya mfanyakazi wa kawaida.

Mkurugenzi mkuu (CEO) aliyepo Afrika Kusini alikuwa analipwa zaidi ya 50% ya mkurugenzi wa kawaida (average executive).

Mwaka 2007, wastani wa mshahara wa Mkurugenzi Mkuu kwa Afrika ya Kusini, ulikuwa Dola 1,370,824 (sawa na Shilingi za kitanzania Bilioni tatu (3)) kwa mwaka. Hii ni sawa na milioni 250 kwa mwezi. Huku Mkurugenzi wa kawaida akiliowa Dola 934,378 (sawa na Shilingi za kitanzania bilioni mbili (2)) kwa mwaka (sawa na Shilingi milioni 170 kwa mwezi).

Ripoti hii ilitumia taarifa kutoka makampuni mbalimbali, mojawapo ya makampuni ya Afrika Kusini yaliyotajwa katika taarifa hii ni Standard Bank (ndugu wa Stanbic Bank), AngloGold Ashanti na Telkom.

Kwa kumalizia, kuna andiko fupi Forbes 2014. Linazungumzia mishahara ya baadhi ya kampuni Marekani kwa mwaka 2013. Chapisho linasema kwa mwaka 2013, Mkurugenzi Mkuu alikuwa analipwa wastani wa mara 774 ya malipo ya mtumishi wa kima cha chini.

Toka mwaka 1978 hadi mwaka 2013, malipo ya CEO Marekani yaliongezeka kwa 725% huku ya mfanyakazi wa kawaida yakiongezeka kwa 127% tu.

Mwaka 1978, CEO alikuwa ana “take home” mara 26.5 ya mfanyakazi wa kawaida, lakini kwa mwaka 2013 take home ya CEO ilipanda na kuwa mara 206 ya malipo ya mfanyakazi wa kawaida.

Nawasilisha.

http://www.ilo.org/wcmsp5/groups/public/---dgreports/---inst/documents/publication/wcms_193236.pdf
Report: CEOs Earn 331 Times As Much As Average Workers, 774 Times As Much As Minimum Wage Earners
The pay gap between CEOs and workers is much worse than you realize
CEO-To-Worker Pay Ratio Ballooned 1,000 Percent Since 1950: Report
CEO Pay Continues to Rise as Typical Workers Are Paid Less
 
Back
Top Bottom