Mababu zetu waliingia mikataba mingi 'mibovu' kwa sababu kubwa mbili ya kwanza
ni kutokujua (ignorance) na ya pili waliwaamini wazungu (bona fide).
Kwetu sisi sababu kubwa siyo ujinga tena - kwani tuna watu wengi wamesoma kama hawa wengine; sababu yetu kubwa ni kutumia nafasi hii kujinufaisha (opportunism) .
Kwa hivyo wao waki declare contents zao kwenye bills of lading au customs au what not sisi tunaamini kwa sababu tunaamini wazungu wanajua zaidi na wanatutakia mema na hivyo hawawezi kutudanganya! Kosa hili la mababu tunalirudia sana.
Sababu nyingine hata hivyo ni kwa sababu tuna woga; huu woga unatokana na mabaki ya athari za fikra za kutawaliwa (colonial legacy's mentality). Tangu kutawaliwa fikra zetu bado hazijafunguliwa vya kutosha kuweza kujiamini.
Kumbe basi, matatizo yetu ya leo yanatokana na sisi wenyewe. Watu wanataka kujinufaisha kwa haraka na kutokana na madaraka yao. Mababu zetu hawakufanya hivyo ili wajinufaishe; walifanya hivyo wakiaminishwa kuwa wanaisaidia jamii yao. Hawa ndugu zetu wanajua kabisa wanachofanya wanachoombea ni kuwa wasijwe kukamatwa.
Katika sababu ulizoeleza wino mwekundu ni sababu halisi. Tuna 'greedy' kwamba kwavile watu wanapata 10% au ni sehemu ya Bodi hakuna anayefikiri nchi.
Mikataba ipo kwa miaka 16 kelele zimepigwa, viongozi walikuwepo. Nini kilitokea?
Pili, ignorance unayosema ni kweli. Hoja zikiletwa bungweni na hasa na wapinzani, viongozi walioko leo walitumia Bunge kuzifinyanga. Sababu ni greedy ingawa leo wanaonekana tofauti
Ni kiongozi gani katika waliopo aliyekuwa hayupo serikalini miaka 16 iliyopita?
Je, hakuna aliyeona uozo huo hadi taarifa ya Jana?
Tusiwalumu wazungu sisi ndio tatizo wala siyo ignorance.
Kilichopo ni ujinga, ubinafsi na woga.Watu wanaogopa nafasi zao badala ya masilahi ya Taifa.
Hatua za jana ni nzuri, lakini je, zimezingatia hali iliyopo?
Tunakumbuka mikataba tuliyopeleka mahakamani na kushindwa?
Kwanini tumeshindwa kuvunja mkataba wa IPTL?
Watakokwenda mahakamani ni wale waliohusika na mikataba miaka 16 iliyopita. Tutashindwa
Muhimu ni hatua za dharura, kisha hatua za muda mrefu ambazo ni kuwaweka wazi wote waliohusika kutufikisha hapa miaka 16 iliyopita
Hoja hiyo inaji 'defeat' na ukweli kuwa wanajuana,ni waoga, greedy ni mwongozo.
Hawataweza kuwachukulia hatua kwasababu ya woga uliosema na ubinafsi