Hii tofauti mkubwa, Idd Amini hakuja nchini kwetu na mkataba alikuja kwa uvamizi hawa qalikuja kwa mikataba. Hivyo kimataifa step ya kwanza ni round table. Mkishindana ndio mnakuja kwenye war mongering kama hii. Hakuna maana yoyote ya kuleta global attention kabla ya kutafuta suluhu. Unless hili liwe limeshibdikana. Lakini kitendo cha ACACIA kutoa press immediately na kuipinga hiyo report maana yake wao hawajashirikishwa. That means lazima third party aje kama msuluhishi. Haya sio mambo ya ubabe. Tuna sababu zote za kutaka fair share ya rasilimali zetu. Lakini hata haki yako, yataka kufuata taratibu ili kuipata.Wewe unaweza kujadiliana na jambazi akiwa kazini? ...unafikiri kuna nchi duniani imewahi kufanikiwa duniani kwa staili ya kubembelezana? ....kama tulikubali kufunga mkanda baada ya vita vya Kagera bora tufunge pia kwenye hili watoto wetu wakute japo masalia ya madini na si mashimo migodini hadi barabarani .....
Hii migodi ina ulinzi wa hali ya juu. Hata kama ungeweka watu usalama bado wataitaji kupeleka sample mahabara ili kupata majibu. Ni kitu ambacho akiwezekani!Off topic:
96% ya wafanyakazi wa hii migodi ni watanzania, miaka takribani 18 tulishindwa ku plant watu wetu wa usalama wenye elimu ya miamba kupiga ushushushu.
Mzee Mwanakijiji ahsante kwa kuibua swali korofi. Kama ulivyosema, jana ilikua ni manyunyu tu naamini mvua inafuatia. Huenda hata hiyo kampuni ikawajibishwa licha ya kujiwahi kutoa tamko kabla hata ya kuipata ripoti kamili.
Huwa najiuliza swali moja, tunapata wapi ujasiri wa kuwacheka na kuwalaumu babu zetu walioingia mikataba mibovu na akina Carl Peters wakati na sisi tunarudia makosa yaleyale? Afadhali yao hawakujua kusoma na kuandika, sisi tutasingizia kipi?
Hii migodi ina ulinzi wa hali ya juu. Hata kama ungeweka watu usalama bado wataitaji kupeleka sample mahabara ili kupata majibu. Ni kitu ambacho akiwezekani!
Kwahiyo mzee Mwanakijiji tuwasemehe waliotufikisha hapa.Kwako vile vile, nimefurahi kukuona upo. Tatizo hata tukianza huko sijaona nani mwingine ambaye anaweza hata kutuonesha njia! Angalau chini ya JPM njia tunaitafuta na ikibidi tunatengeneza njia nyingine! Labda waje watu wengine kabisa na sijui watatoka wapi
Majadiliano!!!!Hili jambo linaenda kuiweka nchi worse than before economically. Afrika tuna sababu zote za kuzuia ubadhirifu wa mali za umma lakini tunakuja kuangukia pua kwa mbinu tunazotumia. Tunaanza ubabe halafu ndio majadiliano, wakati tungefanya kinyume chake tungelifaidika sana. Hivi hili tunalofanya lina tofauti gani na alichofabya jirani yetu Mugabe? Je maisha yameboreka kiasi gani?
After the committee report?Majadiliano!!!!
Kwani hawajawai kujaribu?!
You are very right. Kiukweli hapa tunaomba report na methodology yote ya kamati yetu iwe sahihi hata kwa third party. Ikiwa biased jua tumeumia.kosa la kwanza lilikuwa tume ambayo mchakato wa uundwaji wake haukuwa all inclusive, kwa maana ya kushirikisha upande wa pili.
angalia kwa jicho lolote lile - kisheria, kibiashara au kimahusiano - ile tume haiko credible.
hapa Acacia wametukamata balls.
nikujibu swali lako sasa..... rais alipaswa kutambua kuwa haya ni masuala ya mikataba. so alipaswa kuitisha jopo lake la wanasheria likiongozwa na waziri husika - am sure angefanya maamuzi based on a well informed opinion.
otherwise, where we stand this minute - it's one big catastrophe!
uko juuuuuuuu big upSWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?
Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.
Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.
Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.
Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?
Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?
Kuna watanzania sijui wana hangover isiyoisha? Maana hakuna jambo la utaifa hata mojaKwahiyo? Yaani tushindwe kuchukua hatua kwavile ni too late? ...
Ni nani anatakiwa ku initiate majadiliano?After the committee report?
Ninachosikitika ni kuwa tumelijua hili mapewa wakati wameshabeba madini ya kutosha... Sasa yamebaki mashimo ndio haya mapywa yanaibuka. Its so sad...
Me nafikiri jambo hili kulihusisha na vyama tunakosea sana, nafikiri ishatokea tufikiri tu the way forward.Mi nipo naangalia hatma ya hili sakata
Ila serekari ya ccm imeharibu sana hii nchi.
Sasa inatakiwa kujirekebisha kwani haya yote ni zao la ccm
Suluhu? Container zilizokamatwa bandarini ambazo kamati imegundua kuna udanganyifu inataka suluhu? ....Suluhu na wezi? ....Kuwa na Mkataba wowote si room ya kutaka majadiliano hata kwenye uvunjifu wa wazi wa sheria ambao unataka serikali kuchukua hatua mara moja ....Hii tofauti mkubwa, Idd Amini hakuja nchini kwetu na mkataba alikuja kwa uvamizi hawa qalikuja kwa mikataba. Hivyo kimataifa step ya kwanza ni round table. Mkishindana ndio mnakuja kwenye war mongering kama hii. Hakuna maana yoyote ya kuleta global attention kabla ya kutafuta suluhu. Unless hili liwe limeshibdikana. Lakini kitendo cha ACACIA kutoa press immediately na kuipinga hiyo report maana yake wao hawajashirikishwa. That means lazima third party aje kama msuluhishi. Haya sio mambo ya ubabe. Tuna sababu zote za kutaka fair share ya rasilimali zetu. Lakini hata haki yako, yataka kufuata taratibu ili kuipata.