Swali Fyatu: Walitaka Rais afanye nini hasa baada ya ripoti ile?

Swali Fyatu: Walitaka Rais afanye nini hasa baada ya ripoti ile?

That's not how it works. Hawa serikali na ACACIA ni two parties in a contract. One party (serikali) is claiming to be defrauded by another party (ACACIA). Serikali ilipaswa kuunda tume huru, isiyohusisha watu wake walioteutliwa na serikali peke yake. Sasa ona jinsi ambavyo ACACIA wanasema hawakubaliani na findings za tume. Kwenye mahakama yeyote iliyo huru findings za hii tume haziwezi kutumika kama ushahidi wa kutolea hukumu kwasababu "bias" ilianzia kwenye uundwaji wenyewe wa hii tume. Findings za hii tume zinaweza kuwa za kweli, lakini ili kuepuka utata wa kisheria na maswali juu ya validity ya hizi findings serikali ilipaswa kuunda tume huru. I would have reacted the same way if I were ACACIA. Now, the government is the one using bullying tactics against ACACIA.
Usipumbazwe na zama za huko nyuma ambapo kitu kidogo ndicho kilichotusumbua...bado kuna watanzania wenye akili ambao wanaweza ng'amua milango ya kuvunjilia mbali hii mikataba kwa makosa obvious yaliyofanywa na hao watu...
 
Off topic:
96% ya wafanyakazi wa hii migodi ni watanzania, miaka takribani 18 tulishindwa ku plant watu wetu wa usalama wenye elimu ya miamba kupiga ushushushu.
Ndugu yangu mafisadi ndiyo waliokuwa na upper hand nani awapande wakati wao walikuwa wanakwepa ujambazi wao kujulikana? Yaani inashangaza hata hakuna locals mmoja ambaye anajua wanafanyagaje uchumbaji anagalau basi hata tungeanbualia transfer ya technology lakini wapi...yaani ni kapa hakuna elimu wala ujuzi ni ZERO...kwa sauti ya Mh!
 
Tanzania Tunapenda Kuiga Mambo Ya Kijinga, Hivi Waliosaini Hii Mikataba Hawakujua Madhara Yake? Kansa Ikishambulia Kidole Kidole Hukatwa Vivyo Hivyo kwa Miguu! Tuiwahi Kabla Haijatumaliza Kabisa
 
Hii ACACIA nashauri ifutwe kabisa kufanya extractions zao nchini waondoke,bora tukutane huko kortini,watu weupe wengi wao si watu wazuri halafu bado wanajitutumua kujibu,waondoke.
 
Ajiuzulu, kwani miaka Ya Mkapa kwa mbwewe Magufuli aliunga Mkono Miswada ya mikataba Madini. Na Wakati wa Kikwete pia. Magufuli anajifanya kilia machozi ya Mamba ila Kura yake na za Maccm wenzake kwa mbwewe ndio walionza haki ya kumiliki dhahabu yetu kwa kikapu mkononi! what a Shame!
 
Ni maamuzi sahihi.Ila inaonekana Muhongo na Mawaziri waliomtangulia walilifahamu hili.
 
Usipumbazwe na zama za huko nyuma ambapo kitu kidogo ndicho kilichotusumbua...bado kuna watanzania wenye akili ambao wanaweza ng'amua milango ya kuvunjilia mbali hii mikataba kwa makosa obvious yaliyofanywa na hao watu...

Kama kosa lipi walilofanya ACACIA Mkuu? Mmeletewa report ya upande mmoja. Upande wa pili wanawaambia hawakubaliani na findings za hiyo report. Sasa huoni kama hapo tume huru ndo ilipaswa kuchunguza hili suala? Mbona ni suala dogo tu kulielewa Mkuu. Content ya report inaweza kuwa ya kweli kabisa, lakini kitendo tu cha hiyo report kuwa inatoka upande mmoja, ni tatizo kisheria na hakuna jaji au hakimu ana akili timamu ataikubali hiyo report pasipo independent investigation. ACACIA nao wakija na tume yao ikasema tume ya Magufuli ilisema uongo utaumalizaje huo mgogoro bila mtu wa kati asiye na maslahi pande zote mbili (independent expert investigator)

Magufuli anaweza kutumia report ya wakina Prof. Mruma kuwafukuza watu wake hao wakina Muhongo, lakini sheria bado haipo upande wake kuhusu hatua anayoweza kuwachukulia ACACIA.
 
U
kosa la kwanza lilikuwa tume ambayo mchakato wa uundwaji wake haukuwa all inclusive, kwa maana ya kushirikisha upande wa pili.

angalia kwa jicho lolote lile - kisheria, kibiashara au kimahusiano - ile tume haiko credible.
hapa Acacia wametukamata balls.

nikujibu swali lako sasa..... rais alipaswa kutambua kuwa haya ni masuala ya mikataba. so baada ya kupokea ripoti alipaswa kuitisha jopo lake la wanasheria likiongozwa na waziri husika - am sure angefanya maamuzi based on a well informed opinion.

as pleasantly simple as that!

otherwise, where we stand this minute - it's one big catastrophe!
Umejuaje kama hakuitisha? Wewe ni mjumbe wa Cabinet?
 
Huwezi kuchukua hatua kwa KUKURUPUKA. Tunakumbuka fika jinsi tulivyopigwa kwenye Richmond/Dowans, na si ajabu kwenye IPTL na pia symbion.

Hivi lini tutajifunza sisi Watanzania tuache kukurupuka kwa kutaka sifa na kuishia kuliingiza Taifa kwenye hasara kubwa zaidi!?

~**~**~**~**~**~**~**~**

TANESCO ordered to pay $148m over IPTL dispute
m.ippmedia.com/en/news/tanesco-ordered-pay-148m-over-iptl-dispute

after a World Bank tribunal last week ordered the state-owned power utility to pay Standard Chartered Bank-Hong Kong (SCB-HK) $148.4 million (over 320 billion shillings) plus interest in outstanding capacity charges.

The ruling comes nearly three years since the government controversially authorised payments of over $200 million (440 billion/-) from TANESCO-IPTL’s Tegeta escrow account to businessman Harbinder Singh Sethi’s Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP).

This was after SCB-HK purchased the IPTL loan at a discount price of $76.1 million from Malaysia’s Danaharta Bank in August 2005, following the latter’s failure to secure its outstanding loan from IPTL.

The actual face value of the debt was $101.7 million, according to available evidence. IPTL borrowed over $100 million in 1998 from a consortium of Malaysian banks in order to finance construction of its 100-megawatt Tegeta power generating plant.

Under that transaction, SCB-HK was assigned a number of contracts, including the 1997 Security Deed, the Implementation Agreement and the Guarantee Agreement concluded between IPTL and the Tanzanian government.

The available details show that SCB-HK also became the Security Agent under the Share Pledge Agreement and the Shareholder Support Deed.

Part of the agreement said: “As Security Agent, SCB HK holds all of IPTL’s ‘right, title and interest in and to the Assigned Contracts, including all moneys which may at any time be or become payable to the Borrower.’”

TANESCO had earlier taken its dispute with IPTL to the World Bank-affiliated International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID) for arbitration after the state-owned power utility discovered that it was being overcharged in both capacity and energy charges.

Following this move, both parties agreed as stipulated in their 1996 Power Purchase Agreement (PPA) to establish an escrow account with the Bank of Tanzania (BoT), to be used to deposit all payments pending the outcome of the arbitration.

But a few months before ICSID issued its ruling, the government controversially (and secretly?) paid all the escrow money to PAP after the company claimed that it had acquired full 100 per cent ownership of IPTL in September 2013.

The Washington-based ICSID ruled in favour of TANESCO in February 2014, ordering a tariff recalculation so that finally the escrow money could be paid to either IPTL or the power utility firm, only to then be informed that a third party (PAP) had already been paid everything.

SCB-HK took TANESCO to the ICSID after it realised that the money in the escrow account has been paid to PAP at a time when there was still another pending case over the tariff dispute.

The bank was demanding outstanding payments to clear a loan taken by IPTL’s initial owners to set up the electricity generating turbines.

The Hong Kong-based bank took over control of IPTL after the company failed to pay its loan in 2008, and has since then been fighting to recover the debt.

And after more than five years of rigorous legal proceedings, ICSID judges have now finally ruled in favour of the bank.

"The tribunal orders that TANESCO pay to SCB-HK (Standard Chartered Bank Hong Kong) the amount of $148.4 million with simple interest at three month LIBOR (London Interbank Offered Rate) plus 4 per cent from September 30, 2015 until the date of this award," ICSID said in its latest ruling. "Interest shall continue at the same rate until full payment is received," the ruling added.

DUBIOUS ESCROW ACCOUNT PAYMENTS

ICSID also ruled that payments made by the government from the infamous Tegeta Escrow Account "did not discharge TANESCO's obligations under the power purchase agreement (PPA) and thus cannot be used to reduce the amount that TANESCO owes SCB HK."

TANESCO paid more than $120 million from the IPTL Tegeta Escrow Account to Pan African Power Solutions (PAP) under dubious circumstances in 2013.

The escrow account payments triggered a major national corruption scandal which ultimately led to the resignations of at least three senior ministers in then president Jakaya Kikwete's government.

A number of other senior government officials were also charged with corruption at the Kisutu resident magistrate's court over the IPTL escrow account scam.

Lawyers representing Standard Chartered Bank at the arbitration accused TANESCO of misleading the ICSID tribunal judges by concealing facts about the payments made from the escrow account to PAP.

"SCB-HK understands that PAP used $75 million of the funds obtained from the escrow account to pay VIP Engineering and Marketing Limited (owned by Tanzanian businessman James Rugemalira) for its 30 per cent shareholding in IPTL," says part of the 100-page ruling.

"The funds held in the escrow account that should have been available to satisfy TANESCO's payment obligations to IPTL under the PPA (power purchase agreement) have therefore been paid to two Tanzanian parties - VIP and PAP - neither of whom made any financial contribution to the construction of the facility," it adds.

The ruling seen by The Guardian was dispatched to the parties involved in the arbitration - Standard Chartered Bank and TANESCO - on September 12 this year.

The ICSID is part of the World Bank Group and is funded by the Bretton Woods institution. It is headquartered in Washington, DC, in the United States.

An ICSID award is binding on all parties to the proceeding and each party must comply with it.
If a party fails to comply with the award, the other party can seek to have the pecuniary obligations recognised and enforced in the courts of any ICSID member state as though it were a final judgment of that state’s courts.

Members of the tribunal that issued the award in favour of Stanchart were Prof Donald McRae (president), Prof Zachary Douglas (arbitrator), and Prof Brigitte Stern (arbitrator).

In the arbitration process, the bank was represented by a team of lawyers from two London-based law firms - Herbert Smith Freehills LLP and Linklaters LLP.TANESCO was represented by a team of lawyers from Tanzanian-based law firms R.K.

Rweyongeza & Co. Advocates and Crax Law Partners, and a Zurich-based law firm Kellerhals Carrard.ICSID ruled that each party should bear its own legal fees and expenses.

Kwahiyo? Yaani tushindwe kuchukua hatua kwavile ni too late? ...
 
Zungumzeni yote ila msisahau kuwa kutotumia lugha ya kiswahili kwenye kufunga mikataba kumechangia kutuingiza mkengeni kwa asilimia kadhaa. Najua wengi hamtanielewa kwa hili
 
Alitakiwa awafukuze JK na Mkapa ccm..hilo ndo cha kufanya wao na yeye akiwamo alipitisha mikataba hii
 
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?

Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.

Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.

Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.

Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?

Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?
Suala hili litakapokuwa wazi mtabadili gia angani!
 
Chadema ni wafaidika wa rupia ya Makampuni ya Kizungu, kuna sababu kwa nini Rostam aligharamia Kampeni za chadema, Mwapachu ambaye ni top boss wa Acasia TZ alienda chadema na Wanasheria watetea Mafisadi kama Sanare, Tundu Lisu & Co.!

Jiulize swali Zito Kabwe anapata wapi fedha za kuendeshea Chama cha Siasa? Zito Kabwe hautoki familia ya kitajiri hivyo hana fedha za urithi na kwa mshahara wa Ubunge huwezi kuendesha Chama cha Siasa, hivyo chadema, Zito Kabwe & Co. wote kwangu mimi ni criminals!
Afadhali umesema kwako,it does not matter!
 
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?

Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.

Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.

Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.

Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?

Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?
Zaidi ya kuwaadhibisha wale waliokosea nimependa ii kwa kweli
 
Suala hili litakapokuwa wazi mtabadili gia angani!

Sidhani kama unawajua wenye tabia ya kubadili safari angani; wanaobadili gia hawana tatizo sana kwani wanaweza kwenda kwa kasi Zaidi au pole pole; tatizo ni wenye kubadili safari angani!
 
Walitaka magufuli amfate zito na lisu for consultation .. Report ya kisayansi inapigwa kisayansi wala si na kelele za wanasiasa
 
Back
Top Bottom