Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,873
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?
Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.
Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.
Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.
Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?
Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?