Swali Fyatu: Walitaka Rais afanye nini hasa baada ya ripoti ile?

Sidhani kama unawajua wenye tabia ya kubadili safari angani; wanaobadili gia hawana tatizo sana kwani wanaweza kwenda kwa kasi Zaidi au pole pole; tatizo ni wenye kubadili safari angani!
Ni vijiswahili,ila najua u r not stupid enough kutokuelewa!
 
Chadema ni wafaidika wa rupia ya Makampuni ya Kizungu, kuna sababu kwa nini Rostam aligharamia Kampeni za chadema, Mwapachu ambaye ni top boss wa Acasia TZ alienda chadema na Wanasheria watetea Mafisadi kama Sanare, Tundu Lisu & Co.!

Jiulize swali Zito Kabwe anapata wapi fedha za kuendeshea Chama cha Siasa? Zito Kabwe hautoki familia ya kitajiri hivyo hana fedha za urithi na kwa mshahara wa Ubunge huwezi kuendesha Chama cha Siasa, hivyo chadema, Zito Kabwe & Co. wote kwangu mimi ni criminals!

Hii ndio shida ya watz.. Mambo serious wanayatafutia solution rahisi rahisi ya muda mfupi.. Thinking ya uchama uchama tu.
 
Mkuu tunaambiwa mtumikie kafiri upate mladi wako..na suala la ufisadi katika nchi changa kama Tanzania ni ngumu sana kulimaliza,sidhani kama hiyo ishu ya mchanga inaweza kubadili maisha ya Mtanzania hata kidogo.kiufupi chini ya one man army hatuwezi kufanikiwa.
Unajitahidi kutoa maoni lakini Hapo sio, kwani ukiachwa na gari LA kwanza unaacha kabisa kusafiri? Tuiache Jana imepata kesho bado tuiangalie leo. Sawa tulisha ibiwa sana aidha kwa kujua au kutokujua, na Ulikuwa bado sasa umefika acha Mkuu wetu wa nchi afanye Kazi nas tumuombee kher
 
Nachosikitika ni kwamba ACACIA wanafunga mgodi wao 2019.ccm waachie nchi iendeshwe na watu wenye akili mpya
 
Kama kosa lipi walilofanya ACACIA Mkuu? Mmeletewa report ya upande mmoja. Upande wa pili wanawaambia hawakubaliani na findings za hiyo report. Sasa huoni kama hapo tume huru ndo ilipaswa kuchunguza hili suala? Mbona ni suala dogo tu kulielewa Mkuu. Content ya report inaweza kuwa ya kweli kabisa, lakini kitendo tu cha hiyo report kuwa inatoka upande mmoja, ni tatizo kisheria na hakuna jaji au hakimu ana akili timamu ataikubali hiyo report pasipo independent investigation. ACACIA nao wakija na tume yao ikasema tume ya Magufuli ilisema uongo utaumalizaje huo mgogoro bila mtu wa kati asiye na maslahi pande zote mbili (independent expert investigator)

Magufuli anaweza kutumia report ya wakina Prof. Mruma kuwafukuza watu wake hao wakina Muhongo, lakini sheria bado haipo upande wake kuhusu hatua anayoweza kuwachukulia ACACIA.

Narudia watanzania siyo wajinga...Give it time meeeen...Hii ni zama nyingine!
 
SWALI FYATU:
Baada ya ripoti ya jana, na yote yaliyosemwa, Rais alikuwa anatakiwa afanye nini? Aunde kamati nyingine kuthibitisha matokeo ya kamati ile; au aanze tena uchunguzi wa kuchunguza alichounda kuchunguzwa? Tuchukulie kwa mfano baada ya ripoti ile iliyojaa "madoido" ya Prof. Mruma, Rais angesema ni ripoti nzuri anawashukuru halafu watu wakaondoka zao bila hatua yoyote kali; kwamba alitaka kujua tu kinachoendelea; ni sauti gani zingepazwa? Siyo kwamba Magufuli angeonekana anambeba tena Muhongo?

Sasa baada ya madudu yote yale kuibuliwa Magufuli kweli alikuwa na kitu kingine cha kufanya? Baadhi yetu tunategemea ataenda mbele zaidi maana japo jana limeripotiwa sana la Muhongo lakini tayari kuna watu wengine wengi wamekwenda na maji na kupoteza nafasi zao na sitoshangaa wengine wakajikuta kizimbani.

Lakini zaidi ni hii kampuni ya ACACIA; majibu yake yamejaa ujanja wa maneno na inapuuzia ukweli ambao wengi wetu tunaujua - Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye ufisadi wa kutisha. Suala la ufisadi Tanzania halijakoma kwenye sekta moja; sekta ya madini ni miongoni mwa sekta ambazo zimeathirika sana na ufisadi. Zipo ripoti nyingi zinazoonesha jinsi makampuni makubwa ya uchimbaji madini yanavyotumia mbinu mbalimbali nyingine za kibabe (bullying tactics) katika kuzibana nchi na serikali zisizokaa kwenye mstari wao.

Namna pekee ya kuelewa uzito wa ripoti hii na hatua za Rais ni kuangalia ufisadi kama sehemu kubwa ya haya yanayotokea. Ni nani ambaye hajui jinsi gani ni rahisi kupenyeza rupia ili kupitisha au kujaza fomu fulani ziseme kile ambacho kitaridhisha macho ya wakubwa fulani?
Binafsi nilitarajia hatua kali zaidi kuliko hizi; ikiwemo kuifungia kampuni ya ACACIA kufanya kazi za uchimbaji madini Tanzania kwa miaka kumi ijayo! Ni lazima tufike mahali tujue kuwa kuna umasikini unaoweza kutokana na mtu kupoteza vitu fulani; lakini umaskini wetu sisi ni wa kuamua kwa hiari na kwa kushirikiana sisi kwa sisi kupoteza mali zetu ili tusiwaudhi wakubwa.
Kama ACACIA inaona imeonewa na haiwezi kufanya kazi Tanzania na kuwa yaliyosemwa yote ni uongo (hii ndio maana ya ripoti yao!) njia pekee ni kuondoka na kuacha madini na michanga yetu! Ili tuishi katika kujidanganya sisi wenyewe.

Wakati umefika tuwe tayari kuwaudhi wakubwa ili angalau watoto wetu waje kufurahi mbeleni. Ndugu zetu wanaotaka tuingiwe na hofu ya kuwa sasa tutakiona cha moto wanasikitisha sana; ina maana wenzetu hawa watakuwa wanapiga magoti kila wakipigwa mikwara na makampuni haya makubwa? Ina maana wenzetu watatuma washenga kwenda kuwabembeleza wasiondoke?

Tumenyonywa kiasi cha kutosha; ni kweli! Lakini itakuwaje kama sisi wenyewe tunalilia tunyonywe tena tunawashikia mirija wakubwa hawa na kuichomeka hata sehemu ambazo hazitajiki ili watunyonye hadi chembe za mwisho za supu ya mifupa yetu?
Angekaa na watu waliobobea kwenye sheria na kujadiliana way forward, vilevile vyombo vya usalama vimpe jumuisho ya jinsi wlivyoona wao maana wako kila mahali
 
Hapa Africa ikisimama kiume na kuamua kwenda na BRICS watakuja wenyewe kupiga magoti...Tubadile kabisa na lugha za kuobgea tuanze huongea hu hai uone kama hawakuja mbio na misaada kedekede...Acheni utani, its time for Africa and o other countries of the world to say no to this nonsense!

Mkuu, NImekusoma vilivyo na nakuunga mkono kabisa. Ila, kuna changizo nimeweka kwenye uzi huu huu kuwa; Tumekosa kabisa Siasa safi na Uongozi Bora.
Mtu anachaguliwa na Watanzania wote. Wa chama chake na wasio wa chama chake. Akiisha kuingia anajua moja tu tena anasema wazi wazi kuwa; Chama changu ndo kimenileta hapa. Napigania chama changu kiendelee kutawala at any cost! Huu sio uongozi Bora.
Watu wanapakana matope hadi kuitana Wafu wanaojifilia etc. Hii sio siasa safi.
Tufike mahali;
Tukifufue tena kile chuo chetu cha kivukoni walichokifanya ati ni cha chama flan. Kiwe ni chuo cha kitaifa cha Uongozi. Hapa, viongozi walipelekwa pale wakalishwa uzalendo. Mtu aliyeenda pale alitoka akiwa mzalendo wa nchi yake hii Tz sio chama. Chama kilijiingiza tu kwa sababu chuo kilianzishwa kwa mawazo ya uongozi wa chama flani kilichokuwa ndicho pekee.
Huwezi pata watu wenye uongozi bora waliojiokotezea elimu yao ya uongozi huko na huko.
Hoja yako niliyo i quote hapo juu haiwezi kuja bila uzalendo ndani ya mtu. Ukichaguliwa kwenda kule, wazo la kwanza; Nitapata ngapi hapa?? Huo sio uzaendo. Ukifika unajitahidi kuhakikisha usipungue sana target uliyoweka. Kwani hujui kama bahati hii itakutokea tena. Ndio mwanzo wa kuficha mihela huko huko nje.
Tuwakamate kwanza na kuwang'oa hawa majambazi. Halafu tuanzishe haraka chuo cha Kivukoni wala kisiitwe tena cha chama bali cha uzalendo.
 
Mwanakijiji! Kama unaona mchanga ule ni utajiri wa Taifa letu, basi rudi huku Tanzania uje uusimamie ili Taifa letu lifaidike. Munajitia uzalendo wakati wazee wenu ndio waliotufikisha hapa tulipo sasa. You have no moral authority to criticize wazungu wakati umewafata kwao. Tulitegemea mtu kama wewe baada ya kulelewa na kusomeshwa kwa previledges za Taifa hili uwatumikie watu wako, badala yake unaishi ukimbizini. You can not be serious!
 
nilitegemea Raisi ange step down maana umeliingizia Taifa hasara kwa miaka 2 kwa kutomusimamia Waziri wake wa Nishati ilihali alisha ambiwa na watu kuwa huyo waziri hafai na alishiriki kwenye ufisadi wa Escrow ulio ligharimu Taifa Mabilioni ya pesa.
kwa kweli wa kulaumiwa kwenye sakata hilo ni raisikwa kutosikiliza ushauri sio Prof Muhongo

Ni wewe unayeandika haya, au kuna mtu ameiba password yako?? Na huyo aliyeiba password yako inaonekana kabla ya kuandika hicho alichoandika alikuwa tayari ameshapuliza bange.
 
Sisi wapinzani wazee wakupinga kila kitu tunasema hatua ya Rais sio sahihi. Kwanini tuwakwaze wakubwa, tutaishia kuwalipa kama IPTL na escrow ni bora angeacha tu waendelee kuiba hadi mikataba itapoisha sisi tutavumilia. Tunawapenda sana wawekezaji hatuwezi waudhi watatupeleka kwenye tribunals za kimataifa.

Sincerely,
Wazee wakupinga kila kitu WAPINZANI.
 
ni fundisho na pia ni somo tosha kwa watendaji wote wa serikali kwanza eleweni cheo chako ni dhamana!

awamu hii ya tano chini ya amiri jeshi mkuu JPM haina uswahiba na mtendaji mzembe, fisadi, asiye mzalendo, mfitini n.k,

hakika watendaji watakao salia ktk awamu hii ni, wachapa kazi kwa uadilifu, wazalendo wanao tanguliza maslahi ya taifa mbele, wanao jali wanyonge, wabunifu ktk maendeleo nk.

hatua anazo zichukua mhe rais zinafaa kuheshimiwa na wananchi wazalendo!

anaye weza kukosoa hatua hizi basi lazima tuwe na shaka na uraia wake au huenda anatumiwa kwa maslahi ya wanyonyaji.!!!
 
Mkuu tunaambiwa mtumikie kafiri upate mladi wako..na suala la ufisadi katika nchi changa kama Tanzania ni ngumu sana kulimaliza,sidhani kama hiyo ishu ya mchanga inaweza kubadili maisha ya Mtanzania hata kidogo.kiufupi chini ya one man army hatuwezi kufanikiwa.
Sasa Lowassa angefanyaje?
 
Mzee heshima mbele.

Lazima mbuzi achinjwe kabla ya kuchunwa ngozi, Tuanze na waliotupoteza njia kwanza siyo mkusanya nauli.
Tunayo haki ya kuwatemea mate waharifu wakubwa kiuchumi waliotangulia na kuingiza nchi kwenye msiba mkubwa wa kiuchumi.
Haingii akili kuishia hapo kwa Professor Muhongo.
Muhongo ametumika kama mbuzi wa kafara
Mkapa knew exactly the impact or economic tragedy of fake,bogus minearal deals to our nation.
Na kwanini mikataba mfu ya madini imesainiwa baada ya kifo cha Mwl.Nyerere?
 
Mzee mwanakijiji tunakimbilia kueaona Barick Gold, Ashanti & ACACIA kama wezi, tunasahau kuwa tuliwapa wenyewe na waliowapa bado wapi hai?! Na Bahati mbaya ndiyo mashujaa wetu huku wakiwatukana wananchi malofa, mbumbumbu na wapumbavu kisha tunawapigia makofi.

Shida siyo wazungu Shida ni sisi wenyewe tukubali kujirekebisha
Yupo mmoja alisikika akisema Lowassa ni fisadi mkubwa kumbe ilikuwa kupoteza maboya.Kumbe yeye ni fisadi papa.So sad
 
Kinachomsaidia Mugabe, pamoja na kuua uchumi wa Zimbabwe ni ujasiri wake. Magufuli baada ya kuunda Tume, alikuwa na anazo sababu zote za kufanya alivyofanya. Hatuna sababu ya kumlaumu bali kumsifu kwa ajili ya ujasiri.

Vv
 
Hii ACACIA nashauri ifutwe kabisa kufanya extractions zao nchini waondoke,bora tukutane huko kortini,watu weupe wengi wao si watu wazuri halafu bado wanajitutumua kujibu,waondoke.
Mkuu hao wazungu hawataenda kortini sababu wameishaumbuka na kilichomo ndani ya mchanga.Tume ya wataalamu wazalendo ndio muarobani.
Wao watatumia njia za kidiplomasia watatoa compersation kiasi ikiambatana na ujenzi wa smelter na misaada ya kiuchumi toka nchi kama Uingereza,Canada,Australia na Marekani.
 
Nampongeza sana President Magufuli

Nawapongeza sana wapinzani kwa kuusema ukweli huu kwa miaka yote 18

Ni hatua ya kupongezwa ya Rais Magufuli...Wazungu hawa ni wapuuzi sana..wametuibia sana..wakishirikiana na serikali zote za CCM zilizopita.

Ni wakati mwafaka sasa mabadiliko ya katiba yafanyike ili Rais aliyestaafu awajibishwe kwa makosa aliyofanya wakati anatawala....Mtu kama mkapa na Kikwete hivi sasa wanapaswa kuwa Jela.

Hatuwezi kuendelea kulindana hivi wakati nchi inaangamia

Pia tuko katika hii mess kwa sababu ya aina ya Bunge tulilonalo....Ni Bunge la hovyo kuwahi kutokea...Bunge la wapiga makofi....sheria zote mbovu wanapitisha wao
 
Back
Top Bottom