Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Na. M. M. Mwanakijiji
Kuna mambo mengine yakijirudia unaweza ukafikiria bado uko ndotoni. Maana kuna baadhi ya ndoto zinajirudia rudia hata kama huzitaki. Wengine wanaita "jinamizi". Zinakuja zinatisha halafu unashtuka unasema "duh hii ndoto hii!". Unarudi kulala unafikiri itapita; kumbe ukisinzia tu jinamizi linaanzia pale lilipoishia!
Fikiria mambo ya Bodi ya Mikopo unaweza ukafikiria hili tatizo lingekuwa limeisha zaidi ya miaka ishirini toka tulipolivalia njuga suala la vijana wetu kule Ukraine enzi hizo. Suala la Sukari ni hivyo hivyo, toka miaka ya tisini bado tunazunguka nalo tu; kila baada ya muda linaibuka tena! Hapa naogopa hata kutaja suala la umeme. Yaani, unaweza kuamka asubuhi ukafikiria uko mwaka 1996! Sijagusa suala la uhaba wa fedha za kigeni, naogopa kuuliza kuchelewesha mishahara, nashindwa kuzungumzia mafao ya wazee/wastaafu, na hapa hatujataja suala la ajira kwa wahitimu.
Yaani, ukisoma sasa kuhusu "tuko mbioni", "serikali inajipanga", "tuko tayari kuanza kutekeleza", "tumetoa siku kadhaa hili liwe limeisha".. yaani, unaweza kukuta watu wanapiga makofi wakisahau kumbe baba zao na mama zao na wenyewe walipiga makofi miaka thelathini iliyopita kushangilia matamshi yale yale yaliyotolewa na watu wale wale kwenye matatizo yale yale!
Watanzania ni lazima waamue kama watu wale wale, wenye mipango ile ile, wakikabili matatizo yale yale kwa namna ile ile wanastahili kupewa nafasi zile zile za kuongoza tena! Nje ya hapo ni lazima tujiulize labda kuna vizazi vitaendelea kutushangaa sana kwanini tumeendelea kuwa vile vile! Kwani, matatizo gani wamewahi kuyatatua yakaisha kabisa? Yaani, watakuja tena kuomba miaka mitano mingine na tena wana ujasiri wa kuimba "CCM ni ile ile!"
Kwanini matokeo yasiwe vile vile?