VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
God forbids! Lakini, yawezekana kukatokea kama yale ya tetemeko la Kagera au yanayofanana na yale. Kutaundwa tena Kamati ya Maafa. Kutafunguliwa tena akaunti ya kuchangia waathirika. Je, watanzania wataambiwaje ili wachangie tena kama kwa wanaKagera?
Iko wazi kuwa pesa zilizochangwa na walioguswa na maafa yale ya tetemeko zitaishia 'kukibeba' chama chetu cha CCM kisiasa. Ingawa inadaiwa kuwa 'Serikali' inajenga na kukarabati miundombinu yake, utakapofika uchaguzi (kwakuwa Serikali ni ya CCM), CCM itatamba kujenga!
Wachangiaji wa nje ya nchi nao wanajisikiaje ikiwa walivyoambiwa sivyo ilivyofanyika? Yaani, michango ilikuwa ya waathirika lakini imeishia kukarabati miundombinu ya Serikali. Bajeti za miundombinu zinazotengwa kila mwaka kwa ajili ya miundombinu zimechwa pembeni.
Imesemwa kuwa kila mtu abebe msalaba wake.Msalaba wa wanaKagera ni malazi, mavazi na chakula chao. Msalaba wa Serikali ndiyo michango ya waathirika? Naungana na Mzee Mwanakijiji kuwaambia waliochangia waathirika wa Kagera kuwa 'wakome'!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam