SoC03 Kuwepo na juhudi endelevu za usimamizi wa maafa ili kutekeleza mkakati wa taifa wa usimamizi wa maafa

Stories of Change - 2023 Competition

Tonytz

Senior Member
Jul 18, 2022
159
1,142
UTANGULIZI.

Maafa ni madhara yanayotokana na janga ambayo yanajumuisha uharibifu wa mfumo wa kawaida katika jamii ambao husababisha vifo, majeraha, madhara ya kisaikolojia,, upotevu au uharibifu wa mali, mifumo mbalimbali ya kiteknolojia na huduma za kiuchumi na kijamii au mazingira, ambapo jamii iliyoathirika haiwezi kukabili kwa kutumia rasilimali zake bila msaada kutoka nje ya jamii hiyo (nukuu kutoka chapisho la sheria ya usimamizi wa maafa, 2022). Maafa husababishwa na majanga mbalimbali kama vile mafuriko, tetemeko la ardhi, mlipuko wa volkano, mlipuko wa magonjwa na mlipuko wa moto. Majanga ambayo huweza kuleta maafa hutokana na nguvu za asili au nguvu zisizo za asili (husababishwa ba binadamu).

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambayo inakabiliwa na majanga mengi ambayo ni ya asili na yasiyo ya asili kama vile tetemeko la ardhi, ajali za vyombo vya usafiri, mlipuko wa magonjwa, na janga la moto mashuleni, viwandani, kwenye masoko na maofisini, ambayo hupelekea kutokea kwa maafa mengi hapa nchini. Katika jitihada za kupambana na kupunguza maafa nchini, kumekuwa na juhudi mbalimbali kuhakikisha kunakuwa na usimamizi wenye tija katika kuzuia maafa. Miongoni mwa hatua ni kuundwa kwa sheria ya usimamizi wa maafa, sheria na.6 ya 2022 “sheria ya kuweka mfumo wa usimamizi wa usimamizi na uratibu wa maafa kwa ajili ya hatua za kuzuia na kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea pamoja na kuanzisha na kusimamia mfuko wa usimamimizi wa maafa na mambo yanayohusiana nayo”(nukuu kutoka chapisho la sheria ya usimamizi wa maafa, 2022). Katika kutekeleza mikakati ya sheria hiyo kukaundwa kamati Elekezi ya Kitaifa ya usimamizi wa maafa yenye jukumu la usimamizi wa maafa katika ngazi ya Taifa.

Miongoni mwa mambo yanapelekea maafa ni pamoja na umasikini, uongozi mbaya na machafuko ya kisiasa, miundombinu mibovu na kujengwa chini ya kiwango, ongezeko kuwa la watu sehemu moja na kukua kwa miji, uharibifu wa ardhi na ukataji holela wa misitu, mabadiliko ya tabianchi na shughuli haramu za kibinadamu. Kiuhalisia mambo haya na mengineneyo mengi hupelekea maafa makubwa nchini kwetu. Kwa kuwa yanaleta maafa makubwa ni jukumu letu sote kuyakabili ili kupunguza kiwango cha maafa hapa nchini. Japokuwa Tanzania kupitia serikali ya awamu ya sita inajitahidi sana katika kutekeleza mikakati iliyoainishwa kwenye sheria ya usimamizi wa maafa, 2022, bado kuna maboresho Zaidi yanahitajika ili kuleta ufanisi Zaidi katika usimamizi na kukabiliana na maafa hapa nchini.

MAMBO YATAKAYOWEZA KUONGEZA UWAJIBIKAJI ZAIDI KATIKA KUIMARISHA UDHIBITI WA MAAFA NCHINI TANZANIA.

Kila Mtanzania anapaswa kuwajibika kwa kushiriki kuunga mkono jitihada za serikali katika harakati za kukabiliana na maafa nchini kwa kushiriki moja kwa moja ua kwa namna nyingine iliyo sahihi. Hapa nitaelezea mambo machache yatakayoongeza uwajibikaji katika kudhibiti maafa nchini Tanzania.

Kwanza, kuwepo na utamaduni endelevu wa kuwajengea uwezo wataalamu, maafisa wa kiserikali, wadau na watoa huduma wa kujitolea wa usimamizi wa maafa. Suala la kutoa mafunzo na mazoezi ya mara kwa mara kwa watu hawa ni muhimu ili kuwaweka tayari muda wote kwa ukombozi wakati wa maafa. Hivyo kama Taifa ni wakati sasa wa kuwekeza Zaidi kwenye program za mafunzo mbalimbali ya usimamizi wa maafa na namna ya kukabiliana nayo ili kupunguza kiwango cha utokeaji wa maafa.

Pili, kukuza na kuendeleza ushirikishwaji wa jamii. Ikumbukwe kuwa maafa haya hutokea kwenye jamii zetu, kukosekana kwa elimu na uelewa wa namna ya kukabiliana na maafa, hupelekea maafa kuwa makubwa Zaidi na Zaidi. Serikali kupitia kamati elekezi katika ngazi zote za kiutawala, ihakikishe kuwa jamii inashirikishwa na kuwezeshwa ili kuleta usimamizi mzuri wa maafa. Wanajamii wafundishwe mbinu za uokoaji, huduma ya kwanza na utumizi wa vifaa vya uokozi.

Tatu, kuboreshwa kwa miundombinu na ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miundombinu iliyopo ili kuona ubora na ustahimilivu wa miundombinu hiyo. Haya yanaweza kutekelezwa kwa kuwa na utekelezaji wa kanuni za ujenzi na viwango vya ubora vya ujenzi, na kukarabati mara kwa mara miundombinu inayoonesha kuchoka katika matumizi.

Nne, miongoni mwa changamoto katika usimamizi wa maafa ni umasikini na uhaba wa rasilimali, ili kukabiliana na hilo, kuwepo na tathmini ya mara kwa mara ya hatari na kuchorwa ramani ili kutambua na kuelewa hatari na udhaifu unaowezekana katika mikoa tofauti ya Tanzania. Tathmini na ramani hizi zitasaidia katika kujua kiwango cha rasilimali zinazohitajika katika mkoa husika katika kusimamia maafa hivyo kuwezesha kuandaliwa kwa mikakati itakayoendana na rasilimali zilizopo katika kusimamia maafa.

Tano, kuimarishwa na kupanuliwa kwa mifumo ya tahadhari ya mapema. Mifumo hii itasaidia kutoa taarifa kwa wakati kwa jamii zilizo hatarini. Kwa mfano, kuboreshwa kwa ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuimarisha mitandao ya kimawasiliano, ufuuatiliaji wa miamba na kuelimisha jamii juu ya viashiria vya maafa.

Sita, kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kupashana habari kwa haraka juu ya maafa ndani ya nchi yetu. Kunapotokea dharura yoyote ile ni muhimu habari iifikie jamii kwa haraka sana, mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari na teknolojia ni miongoi vya vyombo vinavyotakiwa kuboreshwa na kuimarishwa Zaidi ili kuongeza uwajibikaji kwa jamii katika kukabiliana na maafa.

Saba, kuongeza uwekezaji kwa kutenga rasilimali fedha za kutosha na kuhakikisha zinatumika kwa ufanisi. Kwa kuwa sheria imeundaa mfuko wa usimamizi wa maafa, ni vema fedha zinazotengwa kwenye bajeti kwa ajili ya usimamizi wa maafa, zitumike kama zilivyokusudiwa. Ili kujipatia pesa Zaidi, hapa inaweza kujumuisha uwekezaji Zaidi kwenye bima za maafa, ufadhili wa kimataifa na misaada kutoka kwa wadau na asasi za kiraia.

Nane, kujumuishwa kwa eliu ya usimamizi wa maafa kwa vitendo katika mtaala wa elimu nchini. Hii itasaidia katika kuwajengea vijana wengi uwezo wa kukabiliana na maafa pale yanapotokea. Hii inaenda sambana na kufanywa kwa kampeni za mara kwa mara za kuhamasisha wananchi kuhusu hatari za maafa na namna ya kukabiliana nayo.

Kwa kuhitimisha, naendelea kuipongeza serikali kwa kuwa macho na maafa yanayojitokeza hapa nchini. Kwa sasa kumekuwa na majanga yanayotisha sana hasa kuungua kwa mabweni ya wanafunzi na ajali ya vyombo vya usafiri, kuungua kwa masoko na viwanda. Rai yangu kwa serikali ni kuweka juhudi endelevu za kuongeza uwajibikaji katika kusimamia na kukabiliana na maafa kwa mustakabili wa Taifa letu. Kwa upande mwingine, wanajamii tuache kuwa vyanzo vya kuleta maafa kwa makusudi kwa sababu binafsi.

isomeke usimamizi hapo kwenye tittle neno usimamimizi liwe usimamizi
 
💪👌
 
Back
Top Bottom