Swali Fikirishi: Je Tanzania tunapambana na nani DRC (EA)?

Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,555
9,330
Kwa majonzi leo tumewaaga Ndugu zetu, Watanzania wenzentu (Hamad Haji Bakari, Chazil Khatibu Nandonde, Idd Abdallah Ally, Juma Mossi Ally, Ally Haji Ussi, Pascal Singo, Samwel Chenga, Deogratius Kamili, Mwichumu Vuai Mohamed, Hassan Makame, Issa Mussa Juma, Hamad Mzee Kamna, Salehe Mahembano na Nazoro Haji Bakari), ambao wameuawa huko Nchini DRC, ni vifo vya kusikitisha kwa sababu ndugu zetu kama Askari pamoja na uchache wao na vifaa duni walivyokuwa navyo huku wakishtukizwa kuvamiwa kambini, waliweza kupambana kwa weledi mkubwa kwa zaidi ya masaa 13, Sambamba na hao 14, kuna ndugu zetu wengine 40 wamejeruiwa na wengine 2 mpaka sasa hawajulikani walipo, SWALI FIKIRISHI, JE (TANZANIA) TUNAPAMBANA NA NANI NCHINI DRC (EA)?

Vita ndani ya DRC ni ya Muda mrefu, na kwa miaka yote UN, waliweka vikosi mbalimbali vya umoja wa mataifa (MONUSCO), kulinda amani ndani ya DRC, Pamoja na kuwa na Waasi wengi, KIKUNDI CHA WAASI CHA M23, KILIONEKANA NI KIKWAZO KIKUBWA NA KILIFIKA KWENYE LEVEL YA KUWA JESHI KAMILI LILILO ORGANIZED, tofauti na vikundi vingine vya waasi,
kwa hiyo terehe 28 March 2013 – Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikaa na kupitisha kuanzishwa kwa intervention brigade ndani ya jeshi la kulinda amani la UN (MONUSCO) lililopo DRC., Security Council walikubaliana kuwa;

"The intervention brigade will carry out targeted offensive operations, with or without the Congolese national army, against armed groups that threaten peace in the eastern part of DRC – a region that is prone to cycles of violence and consequent humanitarian suffering".

Nchi Tatu za Tanzania (Jeshi la nchi Kavu) Malawi (Jeshi la nchi Kavu) na RSA (Anga), walipewa jukumu hilo, na Ilipofika 10 May 2013 – Special force ya Tanzanian iliwasili kwenye mji wa Goma uliopo Kivu Kaskazini na jeshi hilo likawa sehemu ya watunza Amani 3,069 wa UN (MONUSCO) waliopo DRC, huku Wao (Watanzania) wakiwa na kazi maalum (Intervention Brigade) tofauti na wenzao,

Kazi iliyofanywa na Special Unit ya Tanzania haikuwa ya kawaida kabisa, wataalam wa majeshi Duniani walistajabishwa na uwezo waliokuwa nao Wanajeshi wa Tanzania, Kikawaida kama una Jeshi la Anga na la miguu basi la Anga huwa linashambulia kwanza, kisha Askari wa Miguu ndio wanaingia kumaliza kazi, lakini kwa DRC Askari wa South Africa (Airborne) walikuwa wamapigwa na butwaa, kwani walikiwa walikubaliana kuwa leo waende wakapige sehemu fulani, lakini kabla (SA) hawajarusha ndege zao, wanapewa taarifa na Askari wa Tanzania kuwa wasiangaike kurusha ndege kwani wameshamaliza kazi,

Angalia hiyo link hapo chini ya Special Unit Hatari kabisa Duniani , Tanzania (DRC-Special Unit) tupo namba 27 (hizo namba hazikupangwa kwa kuzingatia ubora)
http://www.atchuup.com/badass-elite-fighting-units/

Wakati vita ikiendelea, Ruters walifanikiwa kuwahoji baadhi ya Askari wa M23 na (Reuters) waliripoti hivi,
"The M23 rebels say their soldiers are more than a match for the untested UN Intervention Brigade. "The Tanzanians are the toughest. But kill five South Africans and they all pack up and go home," one rebel leader said derisively".

Jeshi la Tanzania liliwanyongonyesha sana M23 na wengi walikimbilia Uganda na Rwanda, lakini katika kutapatapa kwao , Mwezi wa July 2013 Tanzania ilipata Pigo kubwa sana Nchini Sudani Kusini ambapo Askari wetu 7 waliuawa na wengine 17 wakijeruiwa wengine vibaya sana,, Tanzania hatukuwa na Intervention Brigade Sudan, tulikuwa na Peacekeeper wa Kawaida tu ambao kazi kubwa ni kuangalia amani na kujihami na sio kushambulia,
MAJESHI YA UN SUDAN YA KUSINI YAPO MENGI, IWEJE TUSHAMBULIWE SISI (Watanzania)? je ni wale M23 walitoka DRC wakaingia Uganda kisha Sudan Kusini na kuwafuata Watanzania kulipiza Kisasi?,,

Hayo yakapita na labda tuseme serikali kwa kutumia weledi wake usio na shaka hata kidogo, watakuwa walilifatilia hilo swala kwa kina,

lakini likaja hili la Dec 2017 ambalo ndilo linakuja na SWALI FIKIRISHI, JE TANZANIA TUNAPAMBANA NA NANI DRC (EA)?

Ni Ukweli usiofichika kuwa Hakuna vita unayoweza kushinda bila kuwa na intelejensia kali sana, lazima upate taarifa za adui yako, Nguvu zake, pamoja na mapungufu yake, Wakongo wanasifa moja kubwa sana ya KUTOKUWA NA SIRI, ni watu ambao hawawezi kutunza Siri ya aina yoyote, hata Hao waasi wa M23 japo wengiwao walikuwa ni Watusi lakini pia kulikuwa na Wacongo ambao kwa vyovyote vile ilikuwa ni rahisi sana kwao kuvujisha Siri za kikundi hicho cha M23,

Kutokana na Muktadha huo;
1: Hao waliotushambulia, Walituchunguza kwa muda mrefu, kujua idadi ya Askari waliopo, wapiganaji ni wangapi, officers ni wangapi,Muda gani watu wamerelax, change shift, muda wa kula, kulala, aina ya Silaha walizo zano, Logistic support, communications, msaada utatoka wapi? (NB: ndio maana wanajeshi hawapendi kabisa uingie ndani ya maeneo yao wakikukuta lazima wakupe kibano, hiyo yote ni kuhepuka kuchunguzwa, so Hakuna cha mwokota kuni wala mpita njia)

2: Hao waliotushambulia sio kikundi cha Waasi, bali ni jeshi lililo kamili, lenye Vifaa na Askari wenye Weledi waliokamilika, hakuna waasi wanaoweza kusimama na trained army kama la,Tanzaniamkwa more than 10hrs,

3: Mpango wa kuchunguza kambi ya mtu na kupanga mbinu za kushambulia sio za muda mfupi, na Kutokana na Tabia ya Wakongo KUTOKUWA NA SIRI, ni lazima wangesema tu, so Sidhani kama kulikuwa na Mcongo ndani ya hicho kikundi, na hata kama walikuwepo hawakuwa wanajua kinachoendelea wao walikuja kupewa task tu,

4: Sababu hasa ya Watanzania kushambuliwa ni hipi?, Je Ni M23 kwa mgongo wa ADF wanalipiza kisasi?

5: Majeshi ya MONUSCO yapo mengi ndani ya DRC (Uruguay, China, Pakistan, Brazil, India! Ghana, Tanzania, Malawi, RSA nk), kwa nini Watanzania pekee ndio tumeshambuliwa kiasi hicho? Je sisi ni kikwazo kwa sababu tunawajua kiundani?

Hili tukio ni Zito mno na lazima kila mmoja wetu tujiulize, JE WATANZANIA TUNAPAMBANA NA NANI NCHINI DRC (EA)?

Naomba niwaache na baadhi ya maneno ya Bob Marley katika kibao chake kikali kabisa WHO THE CAP FIT

Man to man is so unjust, children
You don't know who to trust
Your worst enemy could be your best friend
And your best friend your worst enemy

Some will eat and drink with you
Then behind them su-su 'pon you
Only your friend know your secrets
So only he could reveal it
And who the cap fit, let them wear it,

Some will hate you, pretend they love you now
Then behind they try to eliminate you

But who Jah bless, no one curse
Thank God we're past the worse

Hypocrites and parasites
Will come up and take a bite
And if your night should turn to day
A lot of people would run away
And who the stock fit let them wear it (repeat)
 
10 May 2013, Brigadier General James Mwakibolwa akiwapokea Special unita ya Tanzania- Mjini Goma
image.jpg

Juky 2013, Askari wa Tanzania waliouawa nchini Sudan ya KusiniWakiagwa
View attachment 651468

14 Dec 2017 , Miili ya Askari 14 Waliouawa DRC wakiagwa Ngome- Dar
image.jpg
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    64.3 KB · Views: 68
Kwanza Tanzania haina Jeshi Sudan kusini. Pili kama ni intervention Brigade kwahiyo wako vitani wanapambana sio kulinda amani muda ndio msema kweli wao nao wapambane kwa kulipiza kisasi hii vita naona ni kama vita ya kupambana na ugaidi humjui adui yako ni nani ndio kama DRC adui hajulikani most of the time wanajichanganya na Raia ushauri Tz itoe Jeshi DRC basi sababu DRC ina matatizo yake toka Patrice Lumumba kauwawa.
 
Mchanganuo mzuri. Kongo yenyewe misitu tupu na minene. Unaweza kuwakusanya wapiganaji ukawapa mafunzo bila kujulikana kirahisi, hasa usipokuwa na vifaa.

Kitu cha msingi ni kuwa ile vita inalelewa. Na waleaji wa vita ile wanajulikana. Akina kagame na m7 wanaweza kuwa wameongezeka siku hizi lakin miaka mingi Kongo ni shamba la makampuni ya kizungu, ya nchi tajiri. Ndo sehemu ya kuchukua bure malighafi za viwanda vyao, mazahabu na mk

Nina was was sana na uhusika wa waasi wenyewe, Rwanda na Uganda. Labda kama wametumika. Kwamba kuna nchi Kubwa au kampuni likubwa limesema wafanye hivyo na watasaidia Tanzania ikija juu.

Lasivyo waasi, Rwanda na Uganda huenda haziwez kujiamini sana kuanzisha hilo zogo na Tanzania. Na tukichunguza tukumbuke kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wahusika halis wa hilo shambulio kujulikana, japo inawezekana ikawa ngumu sana pia

Umahiri wenyewe wa maandalizi na shambulio unaweza kutupa mwangaza wa nani ni wahusika. Kwa kiasi fulani tunajuana uwezo wetu

Bado nabaki na makampuni na serikali zinazopalilia vita Kongo kama wahusika wakuu wa hilo shambulizi. Hao wengine watakuwa wa kutumika tu,

Na hivyo ni bora afrika nzima ijitoe kwenye kupeleka askari Kongo maana hamna nia ya dhati ya kumaliza vita vya pale. Makampuni yanayochota Dhahabu pale yanataka wakongo waendelee kupigana ili wachote Dhahabu kirahisi na bila kulipa kodi
 
Unazungumzia lini Tanzania haina jeshi Sudan Ya Kusini? Yes wako vitani DRC, swali wanapambana na nani?
 
Unazungumzia lini Tanzania haina jeshi Sudan Ya Kusini? Yes wako vitani DRC, swali wanapambana na nani?

Ninachojua Tz wako katika Jeshi la UNAMID Ila sio Sudan kusini.kuhusu kupambana na nan waulize waliowapeleka kule ndio watakupa majibu.
 
Hoja fikirisha sana nadhani kwenye namba 2 kuna ukweli mkubwa ila tunafichwa tu,poleni ASKARI wetu
 
Mchanganuo mzuri. Kongo yenyewe misitu tupu na minene. Unaweza kuwakusanya wapiganaji ukawapa mafunzo bila kujulikana kirahisi, hasa usipokuwa na vifaa.

Kitu cha msingi ni kuwa ile vita inalelewa. Na waleaji wa vita ile wanajulikana. Akina kagame na m7 wanaweza kuwa wameongezeka siku hizi lakin miaka mingi Kongo ni shamba la makampuni ya kizungu, ya nchi tajiri. Ndo sehemu ya kuchukua bure malighafi za viwanda vyao, mazahabu na mk

Nina was was sana na uhusika wa waasi wenyewe, Rwanda na Uganda. Labda kama wametumika. Kwamba kuna nchi Kubwa au kampuni likubwa limesema wafanye hivyo na watasaidia Tanzania ikija juu.

Lasivyo waasi, Rwanda na Uganda huenda haziwez kujiamini sana kuanzisha hilo zogo na Tanzania. Na tukichunguza tukumbuke kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wahusika halis wa hilo shambulio kujulikana, japo inawezekana ikawa ngumu sana pia

Umahiri wenyewe wa maandalizi na shambulio unaweza kutupa mwangaza wa nani ni wahusika. Kwa kiasi fulani tunajuana uwezo wetu

Bado nabaki na makampuni na serikali zinazopalilia vita Kongo kama wahusika wakuu wa hilo shambulizi. Hao wengine watakuwa wa kutumika tu,

Na hivyo ni bora afrika nzima ijitoe kwenye kupeleka askari Kongo maana hamna nia ya dhati ya kumaliza vita vya pale. Makampuni yanayochota Dhahabu pale yanataka wakongo waendelee kupigana ili wachote Dhahabu kirahisi na bila kulipa kodi

Wazungu hawataicha kongo kuiba milele labda Yesu arudi kwanza Waafrica wenyewe useless kabisa kila mtu anaangalia kwake hao Kagame na M7 wacha waibe nao na watz wakitaka wacha waibe tu hakuna namna nyingine kongo kua salama bora aibe Mwafrica ila sio Mzungu na Kagame kama anaiba namkubali anajenga kwakwe kuliko wale wezi wa Escrow sijui Ufisadi wa rada wanaficha pesa nje.
 
Hao wanaoiba wanapeleka wapi?
 
Kwanza Tanzania haina Jeshi Sudan kusini. Pili kama ni intervention Brigade kwahiyo wako vitani wanapambana sio kulinda amani muda ndio msema kweli wao nao wapambane kwa kulipiza kisasi hii vita naona ni kama vita ya kupambana na ugaidi humjui adui yako ni nani ndio kama DRC adui hajulikani most of the time wanajichanganya na Raia ushauri Tz itoe Jeshi DRC basi sababu DRC ina matatizo yake toka Patrice Lumumba kauwawa.
Kuna Uhitaji Mkubwa Sana Wa Wanajeshi Katika Maeneo Mbali Mbali Kwa Ajili Ya Operation Za Aman Katika Nchi Tofaut Tofaut

Na Ninapo Ongea Sasa Kuna Mazoez Yanayoendelea Kwa Ajili Ya Kwenda Huko Kwenye Izo Nchi

Na Hao Wanajeshi Wanapo Toka Kwenda Nje Ya Nchi Kwa Shughuli Za Kulinda Aman Wanakuwa Chin Ya Jeshi La UN Dats Y Huwa Unawaona Wanavaa Kofia Za Un

Binafsi Nimetembelea Kongo Nimezunguka Sehem Nying Za Kongo Kwa Ufup Tuuu

Kongo Hakuna Aman Kongo Kuna Mkono Wa Mfaransa Katika Kuinyonya Ile Nchi

Kagame Na Yeye Anainyonya Iyo Nchi Kupitia Icho Kikundi

Kinacho Iponza Kongo Ni Rais Kuyang'ang'ania Madaraka kupindisha Pindisha Katiba
 
Kama kagame anaiba mwache aibe tuuu hakuna njia nyingine as mnaawaaminisha watu kua anaiba acha aibe na rwanda ipo pale ilipo
 
Back
Top Bottom