SWALI FIKIRISHI: Je, Magufuli ameondoka na Corona? Hatusikii tena kelele zake

Kweeliiii???
Hili wimbi linapotea Tanzania tuu.
Vipi majirani zetu Kenya ambao wamejifungia toka MWAKA Jana,
Tena wakajarobu kufungua shule MWAKA huu, lakini yamewashinda,
Bado wamefunga shule, ikiambatana na hatua nyingine Kama lockdown, nk
Huko pia lilipita sa hii kumepoa pia.
 
FRANCIS DA DON huko sawa kabisa. Kila jambo lina sababu. Wahenga walisema "UKIONA KIFARANGA KIKO JUU YA CHUNGU UJUE MAMA YAKE YUKO CHINI".
JPM alitujenga kisaikolojia kuhusu vita za wababe wa ulimwengu. Kazi iliyobaki ni sisi wananchi mmoja mmoja kuijua falsafa hii ya JPM na kuitetea ili sisi na vizazi vyetu tuwe salama.
Hawataweza kuelewa mpaka shingo zivunjike,na haya ndiyo madhara ya kuwa na wachumia tumbo wengi
 
Vyombo vya habari vya mabeberu pamoja na Kenya wote kimya...
Mama kasema anaunda tume ya wataalamu wabobezi kuhusiana na Corona.

Kelele zipi tena kabla ya mrejesho?

Tulipo tunasubiria kufahamu tume imeshaundwa na imefika wapi.

Kelele za nini hapo?
 
Uliza BRAZIL wanakufa watu mpaka 3000 kwa siku moja unasemaje haipo

Mkuu kwa ukubwa wa Brazil ukilinganisha na Tanzania. Usishangae kuwa kiwiano na sisi tuko kwenye viwango hivyo hivyo vya vifo kwa siku.
 
Angefanya JPM aliyofanya Samia, kusingekuwa na kelele.

Samia kachukua njia iliyo sahihi kuwaacha wataalamu washauri kitalaamu na kwa uhuru wao wote.

Angefanya hivyo JPM mbona tungemwuunga mkono kama tunavyomwuunga mkono mama?

Hapendwi mtu. Matendo!
Kwahiyo ndio mkawa mnasingizia kila kifo ni Corona? If not, Tanzia kwanini hamleti tena? Why? Leteni Tanzia hata mtu akipata ajali mseme ni Corona, kifo cha JPM kimewaacha uchi wa mnyama
 
Kwahiyo ndio mkawa mnasingizia kila kifo ni Corona? If not, Tanzia kwanini hamleti tena? Why? Leteni Tanzia hata mtu akipata ajali mseme ni Corona, kifo cha JPM kimewaacha uchi wa mnyama

Mtakuwa mmevurugwa kweri kweri. Kifo cha JPM kituache uchi wa mnyama sisi au nyie? Umewauliza mataga wenzio, bashiri, pole pole au katelefoni kabla ya kuandika huu utopolo wako?

In short, sisi kiroho safi tunasubiria tume ya mama ya Corona. Siyo yale mambo yenu na mwendazake ya nyungu nyungu na juice za NIMRI.

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
 
Ile nyomi kipindi cha kumuaga walisema mambo yatalipuka mpaka sasa tunahesabu majuma hatuoni mlipuko wa corona au tuendelee kusubiri siku bado
Propaganda tu na ujuaji wa kijinga. Hakuna kitu kama hicho
 
Back
Top Bottom