Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

muda mwingine tumia kiswahili, inaonekana unakimudu kiasi kuliko kiingereza.
Habari zinazoletwa hapa si za majibu ya ndio na hapana, bali zinaletwa ili wadau ambao ni 'great thinkers' suppossedly 'think tanks' waweze kufanya uchanganuzi yakinifu kwa lengo la kupata ukweli.
Njiwa humu umepotea, jaribu fb.

nadhani weye ndio umepotea ... Unajiita greatthinker kwa kuleta home work ya wanafunzi wa shule ya msingi! ... Ati ccm ili mpindua nani ...?
 
CCM Ni Chama Cha Mapinduzi kweli "Coup d'etat" ndiyo maana
  1. Mwenyekiti wao wa Taifa ni MWANAJESHI
  2. Katibu mkuu wao ni MWANAJESHI
 
wanasema nyani haoni kundule.nasubiri kamusi ya kiswahili ituambie juu ya maana ya 'mapinduzi' kwa sababu ukienda misri unaambiwa kuna Mapinduzi ya kijeshi.
Naona kwa kuwa ccm iko madarakani kwa sasa imekosa cha kupindua na sasa imeamua kuwa chama cha mauaji.

Hata mimi napenda tulinganishe kati ya Chama Cha Mapinduzi vs Chama Cha Demokrasia na maendeleo.
Hakika msajili wa vyama asingekubali kusajili chama cha siasa chenye jina lenye maudhui ya kimapinduzi lakini kama tujuavyo ccm haina usajili.
 
Last edited by a moderator:
Kwenye mjadala wa "Red Brigade" kama uliusoma vizuri nilishasema CCM is irreparably lost and irredeemably unsalvageable, and therefore not worth wasting my breath or keystrokes over. Of course the context may warrant a trashing, even if in the form of a silly Juvenalian satire trashing.

This gives me a chance to reiterate that, the reason I am so vocal about CHADEMA's "Red Brigade" blunder is because I think they are not irreparably lost and irredeemably unsalvageable.

Chama Cha Mapinduzi is a shell of it's former self and an embarrassment to the revolutionary ideas of Galileo, Copernicus, Hegel, The French Revolution, The American Revolution, The Zanzibar Revolution, the list goes on.
 
Ni chama kilichotokana na mapinduzi,
kwao la muhimu ni kupindua
ndiyo maana hawaoni shida kupindua hata demokrasia.
 
CCM=Chama Cha Mafreemasons=wauaji,wanyonyaji wa damu za watu.
 
Kwenye mjadala wa "Red Brigade" kama uliusoma vizuri nilishasema CCM is irreparably lost and irredeemably unsalvageable, and therefore not worth wasting my breath or keystrokes over. Of course the context may warrant a trashing, even if in a silly Juvenalian satire trashing.

This gives me a chance to reiterate that, the reason I am so vocal about CHADEMA's "Red Brigade" blunder is because I think they are not irreparably lost and irredeemably unsalvageable.

Chama Cha Mapinduzi is a shell of it's former self and an embarrassment to the revolutionary ideas of Galileo, Copernicus, Hegel, The French Revolution, The American Revolution, The Zanzibar Revolution, the list goes on.
Nashukuru kwa kuja...naona hapa hutaki kuwapa ushauri hawa jamaa zetu kubadili jina.
 
Chama cha mapinduzi= ina maana hata kikishindwa uchaguzi mkuu, bado kitarudi na kuipindua serikali iliyoko madarakani.
 
Chama cha mapinduzi=Revolutionary Party.....a dirty meaning and matches the various incidences...Kolimba, Sokoine, Mwandosya, Mwakyembe,Ulimboka,Kibanda...na mambo mengine mengi sana...hiki si chama jamani na Nyerere hakuangalia future ya Taifa..hawa waliopo ndio kabisa wanatupeleka kaburini
 
Nashukuru kwa kuja...naona hapa hutaki kuwapa ushauri hawa jamaa zetu kubadili jina.

Ukini quote au kuni mention karibu mara zote sitakosa kuja.

Kuhusu CCM.

Mtu anayejifia kitandani kubadili jina kutamsaidia nini?

This is why I am so adamant that we have a serious and dedicated opposition.

CCM is dying. If we don't have a strong opposition, the next ruling party will be revolving in the same despicable swamp of corruption by institutional failure we now see in CCM.

Mbowe kaongelea kuhusu CHADEMA kuondoka katika activism party per se, na kuelekea kujiandaa kuchukua dola, if he is sincere about that, the wrath of Kiranga is the least of things CHADEMA should be worried about.
 
chama cha mapinduzi mean kila kitu kwao nikupindua haki ionapinduliwa kuwa zulumati, polisi wanapinduliwa kuwa wahuwaji...
 
Kwa kihaya kuna msemo unasema "eibala libi lita nyinalyo" maana yake jina baya umdhuru mwenye jina (tafsiri isiyo rasmi). Mimi nimelifikiri mara nyingi bila kupata majibu, lakini kwa yanayotokea kwa siku za karibuni naanza kupata majibu. Hawa watu wanapindua ukweli kuwa uongo, kwa mfano chukulia matokeo ya uchaguzi ya Arusha mjini, Mwanza mjini, Ilemela bila nguvu ya umma kutetea haki yao hawa jamaa walikuwa wako tayari kupindua matokeo na sasa hivi haya majimbo yangekuwa na wabunge wa CCM.

Hata wanaposema wanataka amani mdomoni wanamaanisha kwamba wanataka kinyume chake, kwa kuwa matendo yao hayaendani na dhamira ya kweli.
 
When I think of CCM I real go crazy. CCM is a group of corrupt people who do not think of democracy.
 
This gives me a chance to reiterate that, the reason I am so vocal about CHADEMA's "Red Brigade" blunder is because I think they are not irreparably lost and irredeemably unsalvageable.

Mkuu Kiranga! Opposition inaweza kuwa ya uchungu, lakini ikiwa ni ya hasira inaweza isifikie matarajio yake na ya jamii, au madhara yake yakawa ya hasi isiyo na tija. Kama Red Brigade ya Chadema ni "blunder", alternative yake ni ipi katika mazingira ya kisiasa yaliyopo?
Pili, seriousness ya opposition unai - define vipi... maana tunao wanasiasa wa upinzani wanaoonyesha uwezo mzuri wa kuchanganua na kukosoa mambo. Na hata Chadema ikichukua dola uwezekano wa kupata mabadiliko/mapinduzi ya nguvu katika kipindi kifupi halitakuwa jambo rahisi, unless tukubaliane kuwafurusha watu wengi tu kwa kuwapeleka kunako ahera !
 
Nimesema hapo awali kwamba sifagilii vi militia vya vyama vya siasa, vyote, si Red Brigade wala Green Guard wala Blue whatever. Nakumbuka polisi walishavipiga marufuku. Ila tatizo polisi (policcm kama wanavyoiita wafuasi wa CHADEMA, not without reason) inafanya kazi kwa kuogopa CCM. Hence wamepiga mkwala, halafu wanaona CCM wanaendeleza vi militia hivi, wanashindwa kusimama thabiti kusema vifutwe vyote. Matokeo yake vinaachiwa.

Sasa basi, maadam vi militia vimeachiwa, I am all for fairness. Kama CCM wanaweza kuachiwa wawe na Green Guard, CHADEMA nao waachiwe wawe na ki-militia chao.

Kwa hiyo kimsingi mimi sina tatizo na idea ya CHADEMA kuwa na militia ya ulinzi wao. Actually kama mtu ninayeamini katika watu kuchukua jukumu la kujilinda wenyewe na kutoitegemea serikali, ningewaona wapumbavu kama wangekuwa wanapigwa mabomu kila siku halafu wanasema "hewalla" tu wasingefikiria kujiimarisha kwa ulinzi.

Tatizo langu liko sehemu ndogo sana, lakini linabeba uzito mkubwa sana.

Hili jina la Red Brigade. Kwangu mimi jina hili halina tofauti na Al-Qaeda. Na kama Matanzania ambaye najua kuna Watanzania wenzangu wameuawa kwa ugaidi wa bomu la Al-Qaeda liliopiga ubalozi wa Marekani 1998, na ninayepinga ugaidi kokote duniani, kusikia chama ambacho kina "a real chance" ya kuchukua madaraka Tanzania kinaiita security organ yake "Red Brigade" kunanikera. Kwa sababu kunamaanisha ama wana endorse ugaidi, au ni ignorant hawajui historia ya hilo jina. Tumeona kwamba Dr. Slaa kaja hapa kusema kwamba anajua historia ya hilo jina, na alivyokuwa anasoma sheria Italy maprofesa walikuwa wanaleta kesi za Red Brigade kufundishia, sasa kwa nini kutumia jina hili? Majina yameisha? This was really immature. Na inaumiza kabisa kwa sababu CHADEMA si chama cha briefcase kinasubiri uchaguzi, ni chama chenye mass appeal.

Seriousness inaanzia hapo kwenye kuchagua jina la security organ. Watu walio serious na kuongoza nchi, wako conscious na image ya chama, hawataki chama kionekane cha kigaidi gaidi, hawawezi kuipa security organ ya chama jina la "Red Brigade".

I would expect watoto wa shule kama pale Tambaza niliposoma, in their youthful indiscretion, kuunda vikundi na kuvipa majina kama haya ya "Red Brigade", they could later discount that as a youthful experiment, a phase in life.

Hawa CHADEMA ni watu wazima, wasomi, kuna ma prominent lawyers, ma doctors of philosophy, imekuwaje wamekubali kujipaka mashonde bila sababu?

Is that what you call a serious opposition?
 
Seriousness inaanzia hapo kwenye kuchagua jina la security organ.
Hawa CHADEMA ni watu wazima, wasomi, kuna ma prominent lawyers, ma doctors of philosophy, imekuwaje wamekubali kujipaka mashonde bila sababu?

Is that what you call a serious opposition
?

Naam! Kama discussion yenye point hii (ya jina la Red Brigade) ilinipita utaniwia radhi....lakini niliposikia jina hili hata mimi nilipata shida sana. Naweka hapa nukuu toka vyanzo vya ki- academia:
"Red Brigades: Italian "Brigate Rosse", militant left-wing organization in Italy thatgained notoriety in the 1970s for kidnappings, murders, and sabotage. Itsself-proclaimed aim was to undermine the Italian state and pave the way for aMarxist upheaval led by a "revolutionary proletariat."
Nakubalina na hoja hii...HAYA WANA CHADEMA MPO?
Brigades took responsibility in the 1990s for various violent attacks, including those against a senior Italian government adviser, a U.S. base in Aviano, and the NATO Defense College"

Red

Threads zipo kibao

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...amuzi-wa-kujilinda;-lakini-wako-sahihi-1.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ni-lengo-baya-chadema-wangeiweka-wazi-1.html

Nasikitika kuona wanaotatizwa na vitu kama hili Tanzania ni wachache.

Kwanza wengi hata hawajui historia kiasi cha kujua "Red Brigades" ni kitu gani.

Halafu wachache wanaojua wanadismiss kama si kitu muhimu.

Mzaha mzaha hutungua usaha.

Usipoziba ufa, utajenga ukuta.

Na ukimsifia sana mgema, tembo hulitia maji.

Na mwisho, mchelea mwana kulia, hulia yeye.
 
Tarehe 5 mwezi februari mwaka 1977 nikiwa mwanafunzi wa Form 3, nilikuwa mmojawapo wa waliochukuliwa kutoka shuleni kwetu kuunda gadi moja ya kucheza halaiki tukishirikiana na wanafunzi wa shule za msingi.

Katika hotuba yake Mwalimu Nyerere aliyoitoa kutokea uwanja wa Aman kule Zanzibar alituahidi kuwa waliamua kuunganisha vyama vya TANU na ASP ili kuunda chama kiomoja chenye nguvu kitakacholeta mapinduzi ya haraka kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa watanzania wote. Wakati huo TANU ilikuwa imefikisha umri wa miaka 23 wakati ASP ilikuwa na umri wa miaka 20 tu. Katika kipindi cha uhai wa vyama hivyo vya TANU na ASP vilikuwa vimeshaleta mafanikio makubwa sana nchini. Vyote viliondoa ukoloni nchini na vilikuwa vimeshaanza kuboresha maisha ya mtanzania. Vilijenga mazingira ambamo wanachi walikuwa wanajivunia nchi yao na viongozi walikuwa wanajua kuwa wao ni watumishi wa wananchi; malalamiko ya wananchi yalikuwa yakichukuliwa kwa uzito sana na ule msingi wa CHEO NI DHAMANA ulikuwa na uzito sana.

Leo hii ni miaka 31 tangu CCM izaliwe; huo ni umri mkubwa sana zaidi ya ule wa vyama vilivyoizaa. Mazingira yaliyojengwa na chama hiki ni yale ambamo wananchi hawana imani na utawala, na vile vile watawala wamekuwa hawaogopi malalamiko ya wananchi. Yote hayo kwa pamoja yameondoa uzalendo kabisa miongoni mwa watu wetu ambapo, viongozi wetu bila woga wanaweza kusaini mkataba wa kukodisha yetu kwa mtu mwingine milele!! !!. na mtu akiuliza kulikoni, basi anapewa vitisho vikali.

Mfano mzuiri ni hili tishio lililotolewa na Katibu Mkuu wa CCM dhidi ya kijana Nape Nnauye kufuatia tamko lake kuhusu ufisadi ndani ya UVCCM. Tihio hilo linaonyesha jinsi gani chama hicho kinavyoheshimu mafisadi na kuwapuuza wananchi tofauti na ilivyokuwa wakati wa TANU na ASP. Kwa nini Makamba amtishie kijana yule badala ya kumtaka alete ushahidi ili yeye (Makamba) aweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa hao badala ya kutoa onyo kabla ya kuangalia ushahidi unasemaje. Huko siyo kujenga mazingira ya mapinduzi.

Ndiyo maana najiuliza, je kweli chama hiki bado ni chama cha Mapinduzi yale tuliyoahidiwa mwaka 1977?

Mkuu Kichuguu

Swali matata sana hili, lakini kwa hali ilivyo sasa naliwahi kufikiri na kukubaliana na waliosema kuwa "Chama Cha Mapinduzi kinaogopa mapinduzi" kama sio hivyo, basi Mapinduzi yaliyokusudiwa na CCM naweza kuyafananisha na Ubeberu ambao una sura nyingi tofauti maarufu kwa kimombo kama Social Democratic, Conservative ama Liberal ama aina nyingine ya ubeberu. Bahati mbaya sana ubeberu wa CCM ulidumu kwa muda mfupi sana kwenye sura ya kidemokrasia, ukadumu kwa muda mfupi sana kwenye uliberali na sasa ni kama tunajielekeza kwenye ubeberu wa kulindana "mwenzetu huyu". Natumai u-mfuatiliaji mzuri wa mabadiliko ya sera za kiuchumi na kisiasa nchini mwetu, hivyo utagundua ya kwamba Mapinduzi yaliyopigiwa kelele na CCM hayana yaendako katika kuhakikisha Watanzania walio wengi wanafurahia uraia na utaifa wao. Kwa maneno rahisi ni kuwa CCM inaogopa mapinduzi ya kweli yenye lengo la kumnufaisha Mtanzania. Utaona namna wanaokemea rushwa na ufisadi wasivyopendwa na watawala wa CCM nchini mwetu. Itoshe kusema kuwa CCM haikumbuki tena mapinduzi iliyoahidi, bali inaogopa aina yoyote ya mapinduzi pamoja na kujiita chama cha mapinduzi.
 
Back
Top Bottom