Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jul 22, 2008.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 22, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Tarehe 5 mwezi februari mwaka 1977 nikiwa mwanafunzi wa Form 3, nilikuwa mmojawapo wa waliochukuliwa kutoka shuleni kwetu kuunda gadi moja ya kucheza halaiki tukishirikiana na wanafunzi wa shule za msingi.

  Katika hotuba yake Mwalimu Nyerere aliyoitoa kutokea uwanja wa Aman kule Zanzibar alituahidi kuwa waliamua kuunganisha vyama vya TANU na ASP ili kuunda chama kiomoja chenye nguvu kitakacholeta mapinduzi ya haraka kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa watanzania wote. Wakati huo TANU ilikuwa imefikisha umri wa miaka 23 wakati ASP ilikuwa na umri wa miaka 20 tu. Katika kipindi cha uhai wa vyama hivyo vya TANU na ASP vilikuwa vimeshaleta mafanikio makubwa sana nchini. Vyote viliondoa ukoloni nchini na vilikuwa vimeshaanza kuboresha maisha ya mtanzania. Vilijenga mazingira ambamo wanachi walikuwa wanajivunia nchi yao na viongozi walikuwa wanajua kuwa wao ni watumishi wa wananchi; malalamiko ya wananchi yalikuwa yakichukuliwa kwa uzito sana na ule msingi wa CHEO NI DHAMANA ulikuwa na uzito sana.

  Leo hii ni miaka 31 tangu CCM izaliwe; huo ni umri mkubwa sana zaidi ya ule wa vyama vilivyoizaa. Mazingira yaliyojengwa na chama hiki ni yale ambamo wananchi hawana imani na utawala, na vile vile watawala wamekuwa hawaogopi malalamiko ya wananchi. Yote hayo kwa pamoja yameondoa uzalendo kabisa miongoni mwa watu wetu ambapo, viongozi wetu bila woga wanaweza kusaini mkataba wa kukodisha yetu kwa mtu mwingine milele!! !!. na mtu akiuliza kulikoni, basi anapewa vitisho vikali.

  Mfano mzuiri ni hili tishio lililotolewa na Katibu Mkuu wa CCM dhidi ya kijana Nape Nnauye kufuatia tamko lake kuhusu ufisadi ndani ya UVCCM. Tihio hilo linaonyesha jinsi gani chama hicho kinavyoheshimu mafisadi na kuwapuuza wananchi tofauti na ilivyokuwa wakati wa TANU na ASP. Kwa nini Makamba amtishie kijana yule badala ya kumtaka alete ushahidi ili yeye (Makamba) aweze kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa hao badala ya kutoa onyo kabla ya kuangalia ushahidi unasemaje. Huko siyo kujenga mazingira ya mapinduzi.

  Ndiyo maana najiuliza, je kweli chama hiki bado ni chama cha Mapinduzi yale tuliyoahidiwa mwaka 1977?
   
 2. H

  Haika JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  ccm si chama cha mapinduzi, mapinduzi makubwa alifanya nyerere, mapinduzi amabayo sasa yako kwenye vitabu vichache sana vya historia, kwa uhakika yatatotolewa.

  sasa chama hiki hakina jipya, hakina mkakati wa kusaidia nchi unaotekelezeka, basi tu tupo kwa mazoea.
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  CCM kama Chama si kibaya, walio wabaya ni watendaji na viongozi wake. Ni viongozi na Watendaji ambao wamekidhalilisha Chama cha Mapinduzi na kukifikisha mahali kilipo.

  Kama tunavyoongelea Chadema na Ukabila, Chadema kama chama si cha Kikabila, ila ni uongozi ambao umefanya kionekane kuwa ni cha Kikabila, same with CCM na Ufisadi.

  Viongozi na watendaji wengi wa CCM, hawafuati kwa undani imani ya Chama chao, ndio maana kinaonekana kupoteza mwelekeo.

  Kinachoipa CCM nguvu ni wanachama wakweli, Wakulima na Wafanyakazi ambao wamekuwa katika chama na kushuhudia uimara wake, na bado wanasubiri siku ya nuru ambapo kitarudia hadhi na heshima yake.
   
 4. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CCM si chama cha mapinduzi,hili ni jina tu lililotafutwa na wajumbe na baada ya kina Thabit kombo kulipenda kutokana na mapendekezo basi cham kikaitwa hivyo.

  Mapinduzi gani?Ya kuleta hali nzuri kwa wananchi? Au mapinduzi ya zanzibar? Inategemea kilichokuwa ndani ya vichwa vya wajumbe.HEUNDA WALIKUWA WAMESHIBA PILAU NA STAREHE ZA TAARABU MMOJA AKAKURUPUKA NA NENO MAPINDUZI...
   
 5. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Ndio ni chama cha mapinduzi kwani hata sasa kimeamua kufanya mapinduzi na kulifanya taifa la kifisadi.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Tulitegemea mapinduzi yalete positive results na kwa kuwa negative na positive yote ni majibu,basi CCM inabaki kuwa chama cha mapinduzi.Sasa mapinduzi kutoka wapi kuelekea wapi ni suala lingine.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mchungaji, hshima kwako.
  Ninavyoelewa mimi, tafsiri ya chama ni; Kikundi cha WATU wenye itikadi...
  sasa nashangazwa sana na mchango wako ambao unataka kukitenga CHAMA na WATU. Ninavyofahamu, chama hakiwezi kuwa chama bilawatu. Set of rules and regulations in themselves cam hardly be CHAMA, Ni lazima wana wa adamuw awepo ndipo chama kinapotimia.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jul 22, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  ..an excellent observation indeed.

  ..wengi wetu tumechukuliwa msukule na hii dhana kwamba CCM iko kivyake, na viongozi wako kivyake.
   
 9. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Mafisadi
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  cember 26, 2008
  CCM: Ni chama cha Mapinduzi?

  Sielewi kwa nini watu wanaamini kuwa CCM ni chama cha mapinduzi. Sijawahi kuelewa na bado sielewi kwa nini. Dhana ya mapinduzi ilielezwa vizuri na TANU, katika "Azimio la Arusha," "Mwongozo," na maandishi, hotuba na mahojiano mbali mbali ya Mwalimu Nyerere. Matokeo ya yote hayo ni kuwa Watanzania tulifahamu vizuri na kukubali dhana na maana ya mapinduzi katika nchi yetu. Yeyote ambaye hajasoma maandishi hayo, au kusikiliza hotuba hizo, ningemshauri afanye hivyo, ili aweze kufahamu msingi wa ujumbe wangu.

  CCM ilipoanza, ilijinadi kuwa ni chama cha mapinduzi. Lakini baada ya muda si mrefu, mwelekeo wake ulijionyesha kuwa si wa mapinduzi. Badala ya kuendeleza fikra na mwelekeo wa "Azimio la Arusha," "Mwongozo" na mengine yote niliyoyataja hapo juu, CCM ilitoa "Azimio la Zanzibar." Ingawa CCM haikutoa fursa iliyostahili kwa wananchi kuliangalia na kulijadili "Azimio la Zanzibar," habari zilizojitokeza ni kuwa Azimio hili lilikiuka yale yaliyokuwemo katika "Azimio la Arusha." Mwalimu Nyerere alilishutumu "Azimilo la Zanzibar" kwa msingi huo.

  Kitu kimoja kilichokuja kufahamika wazi ni kuwa "Azimio la Zanzibar" lilibadilisha masharti ya uongozi yaliyokuwemo katika "Azimio la Arusha" na "Mwongozo." Kwa mfano, "Azimio la Zanzibar" liliondoa miiko ya uongozi iliyokuwepo.

  Baada ya CCM kuvunja misingi ya mapinduzi, kilichofuatia ni kuimarika kwa ubepari, matabaka, na ufisadi. Chini ya himaya ya CCM, "Azimio la Arusha" halisikiki, "Mwongozo" hausikiki, wala maandishi na hotuba zingine zilizofafanua maana ya mapinduzi hazisikiki. Inaonekana kuwa CCM ilikusudia tangu mwanzo kuwafanya watu wasahau hayo yote, ili iendelee na sera za kujenga ukoloni mamboleo nchini mwetu.

  Inakuwaje basi CCM ijiite chama cha mapinduzi wakati inahujumu mapinduzi? Inakuwaje Watanzania hawahoji jambo hilo? Elimu ni ufunguo wa maisha; bila elimu kuna hatari ya kurubuniwa na kuburuzwa kama vipofu.

  Posted by Mbele
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lyunyungu,
  Hiki kingefaa kiitwe Reactionary Party. Chama kilichokiuka mapinduzi.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hicho ilichokifanya CCM hakistahili kuwa ni aina fulani ya mapinduzi?
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Fafanua Mpita Njia ni yapi hayo ?
   
 14. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu, CCM ni chama cha mapinduzi. Jambo la kujiuliza, ni mapinduzi ya namna gani na kwa faida ya nani? Tumeona watu/vyama vingi vikitumia rhetoric za kisiasa ambazo kiutekelezaji zinakwenda kinyume cha dhana ya hizo rhetoric k.m. democracy etc. etc.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  inatemea una maana gani unaposema "mapinduzi." Kunamapinduzi ya kuvuruga nchi ikose mwekeleo. mapinduzi ya kubadili mwelekea wa nchi kurudi kwenye genesis, na mapinduzi ya kugeuze mweleleo wa nchi kwenda kwenye mafanikio.
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  What's in a name? Who remembers what NCCR stood for? What mageuzi is there in NCCR –Mageuzi? Chama Cha Demokrasia Makini would probably lead carefully and democratically, but the only problem is that they cannot find anybody to lead!

  Does a party of socialism have to be socialist? Absolutely not! CCM is a perfect example of that. Who said a party had to be what it's called?

  Was it Remi Ongala or Chongo that sang : Karibu kwetu CCM ee, Uimarishe hali ya wanyonge, Wafanyakazi viwandani, Na wale walioko mashmbani, Uweke uchumi wetu mikononi mwao" ? It would be a perfect scandal if it was Ongala, for ten years later the same artist sang: "Mrema Oo Mrema…." when Mrema tried to consign CCM to the dustbin of history.
   
 17. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Najjaribu kufikiria na kung'amua mantiki waliyokuwa nayo waasisi wa CCM....1977 TANU na ASP walipoungana kikazaliwa CHAMA CHA MAPINDUZI! Najiuliza, kwa nini kiwe cha Mapinduzi? Kwani nani alipinduliwa hapo 1977? Lakini kufuatana na mambo yalifuata, ni dhahiri MWANANCHI ndiye aliyepinduliwa. Slogans kama "Chama kushika Hatamu" na " CCM ina wenyewe" ni dhahiri kwamba mwananchi wa kawaida alikuwa hana lwake nchi hii. Akubali asikubali mambo yataamuliwa tu.
  Kwa nini huyu aliyepinduliwa naye ajilkalie tu?! Baada ya kupinduliwa mwananchi alikandamizwa mpaka leo. Wahenga walishasema, kila refu lina mwisho. Mwannanchi, huu ndio mwisho wa CCM na ukandamizaji wake.

  CHAGUA CHADEMA, USHINDE MAPINDUZI YA 1977.
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona kuna haja ya mapinduzi kama chama chao kinavyosema,ila mapinduzi ya kifkra na mtazamo juu ya CCM ili uchaguzi ujao nao wakae chonjo uku wakiwa wanapiga Jalamba for 2015.
  Unajua huwezi jua thamani ya kitu mpaka ukiwa haunacho,CCM hawaoni umuhimu wa kututumikia wananchi kwa kuwa hawajawai kutokuwa rulling party waone joto ya jiwe kama wenzao Malawi.One day yes
   
 19. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Maana halisi ya mapinduzi kwa mujibu wa waanzilishi wa chama cha mapinduzi ni harakati za kuleta mabadiliko ya haraka katika kuondoa ujinga, maradhi na umasikini miongoni mwa jamii ya watanzania. Kumbuka pia kauli; Tomeonewa kiasi cha kutosha. tumepuuzwa .... kwa hivo lengo lilikuwa jema kabisa yaani kuleta maendeleo ya haraka.Yaliyotokea baadaye ni tamaa za viongozi wachache wenye uchu na viongozi wabovu ambao wamesababisha nchi kudorora kwa kuendeleza ufisadi wa kila aina. Matokeo yake wananchi wameendelea kuteseka na mapinduzi kugeuka kuwa tabu kwa wengi na raha kwa wachache. kwa hivo sasa tunataka mapinduzi ya kweli yatakayowanufaisha walio wengi au wote. swala ni kina nani wako tayari na wamejibainisha wazi kuleta mapinduzi ya kweli.
   
 20. bona

  bona JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  walishinikizwa na wahafidhina wa asp wakina kambi ya karume waliotaka identity ya mapinduzi isipotee ktk historia ili chuki izidi kupandikizwa kizazi kwa kizazi! kina bilal ndio waliokua wamebakia naona wanamaliziwa, nyerere kwa vile alisoma akaona kua haman haja ya kuwapinga, akawapa walichotaka!
   
Loading...