Swali: CCM ni Chama Cha 'Mapinduzi' Yepi?

Mkuu umenena vyema kamanda wangu hii ndio CDM tunayoitaka IQ 700 juu zaidi, Maendeleo ndio msingi wa kila kitu baaaaaaaaaaaaaaaab.pipooooooooooooooooooooooooooooozzzz....
 
Wanabodi,
Wakati CCM ikijiandaa kusheherekea miaka 35 ya tangu kuzaliwa kwake hapo Februari 5 mwaka huu, hebu watetezi wa CCM humu jamvini nawaombeni mnielimishe, hivi hii CCM ambayo ni Chama Cha Mapinduzi, hivi kiukweli bila kutia chumvi , Jee CCM ni chama cha mapinduzi yepi?. Kimefanya nini kustahili kuitwa Chama cha Mapinduzi au ni jina tuu?!.

Angalizo!. Kama na wewe hujui CCM ni chama cha Mapinduzi ya kitu gani haswa naomba usijibu kitu wala usikibeze CCM, jinyamazie kimya ukisubiri wanaojua CCM ni Chama cha Mapinduzi yapi watuletee majibu!.

Wasalaam

Pasco (wa Jf).
 
Soma Azimio la Arusha.......
Ndipo utakapojua maana ya "Mapinduzi"

Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha,
na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya
tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi;
mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena
......
 
Ndugu yangu usianzishe mada halafu unaweka condition za kujibiwa au kutoa maoni, kwani hapo nyuma kabla ya CCM unakumbuka kama kulikuwa na TANU na ASP, sasa kama ASP ilipindua huko zanzibar kwa msaada mkubwa sana kutoka upande wa bara ambao ni TANU, huoni baada ya kuungana waliona ni bora iwe chama cha mapinduzi hayo ya Zanzibar ambayo kwa pamoja yakaleta Tanzania, ni mawazo tu.
 
Sobby Kwa mtazamo huo jee ni CCM iliyoyafanya hayo au ni TANU?.,CCM inayo legitimacy ya kujiita Chama cha Mapinduzi bila kufanya mapinduzi yoyote?.
 
Soby, nakubaliana na maoni haya lakini kwa mtazamo wa mapinduzi kuwa ni azimio la Arusha, basi wananchi walipindua halafu wakapinduliwa na mafisadi, mimi nina haki ya kusema tumepinduka pinduka mpaka tukapitiliza, kwani yanayofanyika na viongozi wa sasa yanaweza kuwa ni bora yaliyokuwa kabla ya Azimio la Arusha. ni Maoni baba.
 
Ndugu yangu usianzishe mada halafu unaweka condition za kujibiwa au kutoa maoni, kwani hapo nyuma kabla ya CCM unakumbuka kama kulikuwa na TANU na ASP, sasa kama ASP ilipindua huko zanzibar kwa msaada mkubwa sana kutoka upande wa bara ambao ni TANU, huoni baada ya kuungana waliona ni bora iwe chama cha mapinduzi hayo ya Zanzibar ambayo kwa pamoja yakaleta Tanzania, ni mawazo tu.
Namimih, lengo la zuio lile ni kuinusuru CCM na kashfa za jf, hapa kuna chama ukikitaja ni kusifiwa tuu kwa kwenda mbele na kuna chama ukikitaja kinakandiwa kwa sana. Lengo ni kwa watetezi wa CCM na sio wabondaji.

Kwa hiyo Chama cha Mapinduzi kumbe ni yale ya Zanzibar?. Hapa sasa naanza kuelimika!.
 
nyerere alisema kuwa jina mapinduzi halina tafsiri ya kiingereza" revolutionary."alisema chama cha mapinduzi ni jina la chama tuu na halina maana ya kuwa ni chama cha revolutionary!! hivyo unapouliza ni mapinduzi yepi, me ndo naona unamkosea heshima nyerere ! ni kama vile ile nembo ya simba ssc inayosema "simba yasonga mbele", halafu mwenyekiti wa simba awaambie mashabiki wa simba kuwa "yasonga mbele" haina maana maana simba inakuwa vizuri bali ni neno la utani wa jadi tuu!!!

Kweli marehemu hemedi manenti alisema___" twafuma kutali chilukutaa!!" tumetoka mbali ujingani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sobby Kwa mtazamo huo jee ni CCM iliyoyafanya hayo au ni TANU?.,CCM inayo legitimacy ya kujiita Chama cha Mapinduzi bila kufanya mapinduzi yoyote?.
Mkuu, TANU ndiyo CCM.
Kama sunderland (ya bongo) ilivyokuwa Simba.
Huwezi kusema ulikunya tu, ila hukukojoa....
Huo utakuwa ni uongo.
 
Waliazimia kufanya mapinduzi lakini bado hayajafanyika kama leengo la Mwl na hii ni dream ya NAPE kuwa kuna siku CCM itakuja kufanya MAPINDUZI makubwa nchini ya; kilimo, utawala bora elimu, afya, madini, nishati nk
 
CCM= TANU + ASP. ASP = Chama kilichopindua uongozi wa Zanzibar hence CCM = Chama cha mapinduzi (yale ya Zanzibar).
Wanabodi,
Wakati CCM ikijiandaa kusheherekea miaka 35 ya tangu kuzaliwa kwake hapo Februari 5 mwaka huu, hebu watetezi wa CCM humu jamvini nawaombeni mnielimishe, hivi hii CCM ambayo ni Chama Cha Mapinduzi, hivi kiukweli bila kutia chumvi , Jee CCM ni chama cha mapinduzi yepi?. Kimefanya nini kustahili kuitwa Chama cha Mapinduzi au ni jina tuu?!.

Angalizo!. Kama na wewe hujui CCM ni chama cha Mapinduzi ya kitu gani haswa naomba usijibu kitu wala usikibeze CCM, jinyamazie kimya ukisubiri wanaojua CCM ni Chama cha Mapinduzi yapi watuletee majibu!.

Wasalaam

Pasco (wa Jf).
 
Mwalimu alikuwa na mawazo mazuri sana na ndio maana akatilia mkazo mapinduzi katika viwanda, kilimo, elimu n.k
Katika miaka ya 90 mambo yakaanza kubadilika waliochiwa madaraka wakaleta mapinduzi katika kuuza viwanda na rasilimali za nchi.

Huyu brotherman akaenda mbali zaidi mapinduzi yake kura zooote za wapinzani pindua weka kwake. wanyama uza wote watalii wasipate tabu ya kuja kuwaona. akaamua kupiga headphone hakuna kusikia kelele zao.
 
Mapinduzi ya maoni ya watanzania walio wengi, kama walivyokuwa wanapindua maoni ya wazanzibari kwa kuchakachua kura tangu mwaka 1995 hadi MS akasalimu amri ,na pia mwaka 2010 walivyochakachua kura na kumtangaza JK kuwa mshidi kwa msaada wa JWTZ,TISS,POLISI chini ya usimamizi wa NEC ya Lewis Mkame.Hayo ndiyo mapinduzi bana au unasemaje Pasco?
 
Kwani chama hiki kimeitwa Chama Cha Mapinduzi? Kilipindua nini? Kilimpindua nani? Hapa kuna siri iliyonyuma ya pazia,jina hili halikuja bure tu bali lina maana fulani. Kama ni mapinduzi Zanzibar! Huku bara kinahusika vipi? Kilipindua nini? Nini siri ya Nyerere?
 
Kilipindua akili za watanzania wakawa mazoba na kuibiwa raslimali za nchi mchana kweupe
 
mara nyingi tumekuwa tukiiongelea ccm katika hali mbalimbali ,ninafahamu ukitafuta historia ya ccm huwezi kuitenganiasha na tanu,katiba ya tanu imebeba madhumuni yote ya azimio la arusha ambalo ni azimio la utu swali,je unakuweje ccm inaitwa chama cha mapinduzi baada ya kukiuka misingi ya azimio la arusha misingi ya utu? au ni mapinduzi gani haya?
 
siwameshapindua misingi ambayo chama chao kilijengwa,kile kitendo cha kukiuka misingi tu ya chama kuwa cha WAKULIMA NA WAFANYAKAZI hadi kuwa cha WAFANYABIASHA WAKUBWA,hayo yanatosha kuitwa mapinduzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom