CCM kama Chama si kibaya, walio wabaya ni watendaji na viongozi wake. Ni viongozi na Watendaji ambao wamekidhalilisha Chama cha Mapinduzi na kukifikisha mahali kilipo. Kama tunavyoongelea Chadema na Ukabila, Chadema kama chama si cha Kikabila, ila ni uongozi ambao umefanya kionekane kuwa ni cha Kikabila, same with CCM na Ufisadi. Viongozi na watendaji wengi wa CCM, hawafuati kwa undani imani ya Chama chao, ndio maana kinaonekana kupoteza mwelekeo. Kinachoipa CCM nguvu ni wanachama wakweli, Wakulima na Wafanyakazi ambao wamekuwa katika chama na kushuhudia uimara wake, na bado wanasubiri siku ya nuru ambapo kitarudia hadhi na heshima yake.