Mpevu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 1,803
- 178
Well, nilipitia Chipukizi miaka hiyo - bado ninazielewa itikadi za CCM. Mapinduzi yako ya aina nyingi na siyo lazima yawe ya kuuondoa uongozi fulani na kuweka uongozi mwingine kwa nguvu.
Chama cha Mapinduzi ni chama kilichoanzishwa ili kuleta mapinduzi ya kilimo na viwanda nchini (jembe na nyundo). Tulianza kuongeza nguvu za kupambana na adui zetu watatu wa maendeleo na kujenga viwanda ikiwa ni pamoja na kuimarisha mashirika ya umma kama MECCO, ATC, TTCL n.k Katika kipindi hicho tulijenga viwanda vingi na kuongeza tija ya kilimo na mazao yatokanayo na kilimo au mifugo kama ngozi n.k
Kwa ujumla mapinduzi yanayoelezwa katika chama (CCM) ni mapinduzi ya kifikra na kiutendaji kwa maana ya kuweka misingi sahihi ya kujitegemea kama nchi. Tulikuwa na dira, dhamira na nia safi ya kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii. " Wenzetu wako mbali hivyo kama wanatembea sisi inabidi tukimbie" - J.K Nyerere. Tuliangalie neno mapinduzi kwa maana hiyo ... kuwa ni chama kitakachotuongoza katika kubadili mfumo tuliourithi toka kwa wakoloni na kuweka mfumo mpya wa haki, usawa na maendeleo ya kisayansi na Teknolojia kwa mwelekeo wa kujitegemea. Hayo ndo mapinduzi yanazozungumzwa na chama (CCM).
Well, naomba nisiulizwe maswali tena kuwa nini kimetokea katika hizo dhamira, nia n.k.... Chama kilibadili haya mambo mwaka 1992 katika azimio la Zanzibar. Sijui kinachoendelea maana si mwanachama tena baada ya mabadiliko hayo!!
JEMBE NA NYUNDO,
KILIMO KWANZA...MAPINDUZI YA KIJANI
UHUISHAJI WA VIWANDA VILIVYOBINAFSISHWA...itafatia
Loh!