BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,840
Chichewa Language: Samaleko = kuwa mwangalifuSamaleko!
Ila mkuu majina ya surah sio kwamba ya litoka kwa Allah, hapana haya majina ya surah imetumwa na maswahaba na khalifa Abubakar( ra) kwahoyo sioni cha ajabu chochote hapo.Hiii ndio Sura (ufunuo) pekee katika Qur'an iliyopewa jina la mwanamke maalumu anayejulikana, ingawa ndani ya sura hii kumetajwa manabii wakubwa wakubwa kama vile Nabii Yahya, Zakaria, Ibrahim, Is-haq, Yaquub, Idriss, Ismail, n.k. Wote wametajwa ndani ya sura hii.
Kisa cha Bi Maryam katika kumzaa Nabii Issa, ilikua si tukio la kawaida ni miujiza ambayo ilistahiki kubakishwa na ndipo Mwenyezi MUNGU akalitumia jina la Marym katika sura hii.
Sura hii imeitwa kwa jina la mwanamke msafi, ambaye aliishi maisha yake yote katika hali ya kiimani kuanzia utoto wake hadi katika ujana wake.
Malaika walimwambia, 'Ewe Maryam, hakika Mwenyezi MUNGU amekuchagua wewe na akakutakasa, na akakuteua kuliko wanawake wa ulimwengu wote.
Sifa za Maryam
-Aliweza kulinda uke wake, hakufanya machafu ya aina yoyote, aliudhibiti uchi wake, hakufanya uchafu wowote wa zinaa, ni mwanamke ambaye alilinda nafsi yake. Lakini Mwenyezi MUNGU alimtia roho Maryam, yaani Nabii Issa.
Sura hii imeitwa Maryam kwa lengo la kubakisha historia ya mazazi ya kimiujiza,
Suratu Mariam ni sura ya 19 katika sura 114 za Quran, pia ipo juzu la 16 katika majuzu 30 ya Qur'an. Sura hii imechukua aya 98 katika aya 6666 za Qur'ani Tukufu.
Suratu Marym imeshuka katika mji wa Makka, ispokua aya mbili tu ndio zimeshuka Madina. Aya 96 zimeteremka Maka. Aya mbili zimeshuka madina ambazo ni aya ya 58 na aya ya 71.
View attachment 2989196
Imeitwa Surat Al-Jin kutokana na mada yake, kwani ndani yake tukio la Majini kuisikia Quran na kuukubali uilsamu kisha kurudi kwa wenzao kwenda kuwahubiria Uislamu.Na Surah Al Jin kwenye Kuruani Kwa Nini hiyo Sura imepewa jina la Majini
Nadharia kama nadharia nyingine tu za upande wa pili ila cha umuhimu kufahamu ni MUNGU yupo na sisiImeitwa Surat Al-Jin kutokana na mada yake, kwani ndani yake tukio la Majini kuisikia Quran na kuukubali uilsamu kisha kurudi kwa wenzao kwenda kuwahubiria Uislamu.
Mtume Muhammad (S.a.w) alikuwa akisafiri kutoka Makka kuelekea soko la `Ikadh huko Taif ili kuwaalika watu wengi waliokuwa wakimiminika huko ili awafikishie ujumbe wa Uislamu. Hata hivyo katika mkusanyiko huu, hakuna hata mmoja wa wale waliohudhuria aliyekubali mwaliko wake. Watu watukufu wa Taif walimkadhibisha vikali na wakamrushia mawe Mtume kiasi kwamba damu zilikuwa zikimtoka mwili mzima
Akiwa amechoka na kufadhaika, alisimama karibu na bustani. Mahali hapo, alikutana na mtumishi wa mwenye shamba jina lake Adas. Mtumwa huyu alikubali mafundisho ya Uislamu na baada ya hayo, Mtume aliendelea na safari yake ya kurejea nyumbani Makka.
Akiwa njiani kurudi, Mtume (S.a.w) alifika sehemu iliyoitwa Bonde la Majini. Alikaa hapo kwa muda wa jioni na akazama katika usomaji wa Qur'ani Tukufu. Kundi la Majini, waliokuwepo na kumsikiliza, mara moja waliikubali imani ya Uislamu. Baada ya hapo, walirudi kwenye kundi lao ili kueneza na kueneza mafundisho waliyoyakubali kutoka kwa mtume.
Wakati wa usiku huo, alifika karibu na msitu wa miti na akiwa anashughulika katika Swala, kundi la Majini kutoka eneo la Yemen lililotokea eneo hilo lilisikia kisomo cha Qurani ya Mtume (s.a.w.w.) katika Swala yake ya al-Fajr na wakakubali mafundisho ya Uislamu hapo hapo.
Upo sahihi,Ila mkuu majina ya surah sio kwamba ya litoka kwa Allah, hapana haya majina ya surah imetumwa na maswahaba na khalifa Abubakar( ra) kwahoyo sioni cha ajabu chochote hapo.
Imeitwa Surat Al-Jin kutokana na mada yake, kwani ndani yake tukio la Majini kuisikia Quran na kuukubali uilsamu kisha kurudi kwa wenzao kuwahubiria
Kwa hiyo Yako majini maislamu ambayo huswali na waislamu wakati wa swala misikitini?Akiwa njiani kurudi Makka, Mtume (S.a.w) alifika sehemu iliyoitwa Bonde la Majini. Alikaa hapo kwa muda wa jioni na akazama katika usomaji wa Qur'ani Tukufu. Kundi la Majini, waliokuwepo na kumsikiliza, mara moja waliikubali imani ya Uislamu. Baada ya hapo, walirudi kwenye kundi lao ili kueneza mafundisho waliyoyakubali kutoka kwa mtume.
Wakati wa usiku, Mtume alifika karibu na msitu wa miti na akiwa anashughulika katika Swala, kundi la Majini kutoka eneo la Yemen lililotokea eneo hilo lilisikia kisomo cha Qurani ya Mtume (s.a.w.w.) katika Swala yake ya al-Fajr na wakakubali mafundisho ya Uislamu hapo hapo.
Sio msikitini tu hata makanisani majini yanaingia ila maovu na ndio maana unaona huko watu wanadondoka.Kwa hiyo Yako majini maislamu ambayo huswali na waislamu wakati wa swala misikitini?
Mbona kama vile Roho inakuuma sana, kuna shida gani?Dini ni upuuzi furani hivi,mud aliibi kisa cha mariamu myahudi mamake Yesu,akakiingiza kwenye story zake za kuunga unga.
Kimsingi hakuna jipya ukitaka storia kamili lazima ukasome biblia ndio utapata historia kamili sio kurwani mana visa vya kurwani ni story za kukuungaunga kutoka kwa story za wayahudi.
Tuambie huyo mariam alikua kabila gani,na kisa kilitokea wapi..?haya majibu lazima uende kwenye biblia ndia utayapata,kurwani huwezi pata jibu lolote.