Support System...

kwa aibu zangu mimi,kwangu mimi,ni best option.kulooongaaa weeeee,nikamwaga kila kitu face to face,huwa siwezi.huwa inachukuwa muda mrefu,kumzoea mtu na kuunda urafiki
hapo red ni mbegu adimu kweli hiyo kwa kizazi cha leo! eniwei kuna baadhi ya issues hauwezi kuziongea kiuwazi face to face hata na mzazi wako. So nadhani social networking ni the best option ya kushare kwa baadhi ya kesi.
 
Ugumu wa maisha nao unachangia.
Mtu ana familia yakena tayari anahangaikasana kuwawekea kitu mezani alafu na wewe uende kwake kuomba msaada ?Inakua ngumu kwa kweli.
Lizzy aksante sana kwa hii thread ingawa inasikitisha sana. Poor kids jamani mbona wiki hii imeanza vibaya kwangu?? Hizi habari za ukatili kwa watoto zinaniweka kwenye wakati mgumu sana wapendwa. MUNGU tusaidie

Lizzy darling hii pia inachangiwa na kutokuwa na uchaji wa MUNGU na upendo kwa wenzetu. Hivi ulishawahijaribu kugawana kidogo ulichonacho na asiye nacho?? faraja unayoipata moyoni ni kubwa sana na pia unafungua milango ya baraka hebu watu tujifunze kusaidia watu wenye shida tuone.
 
...nice one lizzy, ....hatuwezi kumhukumu kwa haki huyo mdada hatujui ni kwa kiasi gani alisukumwa na kudhalilika kwa kiwango gani mpaka akafikia kuchukua maamuzi hayo kutokana na usongo wa mawazo.

...hata hapa jf wengi sana wanadiriki ku share machungu yaliyo maishani mwao kwa njia ya mtandao... tusiwadhalilishe na kuwakebehi. maisha ni zaidi ya tuyajuavyo, wengi hawana uwezo wa kufungua mdomo mbele ya ndugu, jamaa na marafiki...

mwenyezi mungu awape pumziko jema hao malaika.
 
Baada ya kuona maisha yamemshinda. Kuumbuka kumeshafikia kikomo, wafadhili wameshakata ufazili wao, marafiki wakimkimbia, hana cha kuuza tena, nauli ya kurudi kijijini imemshinda..............

Kamwanda akaamua kutafuta Suport toka kwa mai waifu wake...........

Usiku wamelala akamwambia mkewe: "Mke wangu tutaua watoto na kwashakoo wakati weye u bado kijana na mzuri namna hii?........ Huko mtaani hutongozwi?.........kama watongozwa, nimeridhia wakubalie wakupe hela tusiendelee kuumbuka namna hii............" Mwisho wa kunukuu.

Hii ndiyo Suport Sytem kwa mwanaume mwenye upendo na familia yake.

Anayetaka kujua kilichotokea baada ya hapo, anyooshe kidole juu.
 
Kwa system za maisha ya ulaya sidhani kama angeshindwa kuwakabidhi hao watoto kwa social security! Mimi nadhani ana personal issues ambazo zimempatia depression tu na akaamua kuuwa watoto kwa msukumo wa depression.
Au pia inawezekana amekosana na watu wa kwenye system na akajijua yeye yupo right hivyo ameamua kufanya hivyo ili system iwajibishwe. All in all mama yupo very wrong.

nakubaliana nawe dawa chungu...
huko ulaya ukijibana vizuri hukosi kazi hata
ya kubeba maboxi.. si lazima system yaonekana
yeye alikuwa ana "depend "sana kwenye hizo system na
alikuwa hana plan nyingine zikikataa..
 
Create your own support system...be someone else's support system.
Ukihisi mtu wako wa karibu ana kitu kinachomsumbua jaribu kuwa karibu nae usije baadae ukabaki kufikiria ''ningejua ningeweza kumsaidia''.

Lizzy don't you know that the only support system is the Christ Jesus.............read John 15:7 for further proof........................."If you abide in Me and My word abides in you; you will ask for whatever you desire and it shall be done for you."
 
Baada ya kuona maisha yamemshinda. Kuumbuka kumeshafikia kikomo, wafadhili wameshakata ufazili wao, marafiki wakimkimbia, hana cha kuuza tena, nauli ya kurudi kijijini imemshinda..............

Kamwanda akaamua kutafuta Suport toka kwa mai waifu wake...........

Usiku wamelala akamwambia mkewe: "Mke wangu tutaua watoto na kwashakoo wakati weye u bado kijana na mzuri namna hii?........ Huko mtaani hutongozwi?.........kama watongozwa, nimeridhia wakubalie wakupe hela tusiendelee kuumbuka namna hii............" Mwisho wa kunukuu.

Hii ndiyo Suport Sytem kwa mwanaume mwenye upendo na familia yake.

Anayetaka kujua kilichotokea baada ya hapo, anyooshe kidole juu.

Hahahha nacheka wakati inasikitisha. Wewe Asprin wewe ah. Kwa hiyo unataka kusema hata iwe vipi, lazima kuna mlango wa kutokea si ndio?
 
Hahahha nacheka wakati inasikitisha. Wewe Asprin wewe ah. Kwa hiyo unataka kusema hata iwe vipi, lazima kuna mlango wa kutokea si ndio?
Sitakujibu kwa sababu hujanyoosha kidole.......una tabia mbaya.

Jibu la swali lako ni NDIO. Mlango wa kutokea upo, hata kama kuna maumivu kuutokea. Maisha lazima yasonge mbele, siyo vifo vitangulie maisha.
 
Lol mwalimu mwenyewe mkali kila mwanafunzi anahofia kunyoosha kidole....mie najitosa unaninanga!!

..........Ni kweli kama unavyosema lakini kama nimemwelewa vema Lizzy ni kuwa inawezekana kabisa kuwa hizi option huyu dada hakuziona kutokana na ile hali ambayo mpaka sasa hatujaijua bado, iko ndani yake mwenyewe.
Mwalimu Lizzy sema kama nimepatia !
 
Hako ni kadalili ka kutaka kuanza umbea lol
 
kwa tunaoishi africa lifestyle yetu ni support system kubwa

ofisini mnaongea yote,kijiweni the same....wadada wakienda saloon ndo usiseme

kwenye daladala wakati wa foleni.watu wanabwabwaja tu mambo yao.....

uswahilini,wapangaji wenzio na kadhalika......ndugu,mjomba,shangazi....

sometimes ukiishi kizungu kwa hapa africa unapata hizo risk za depression....

ingawa siwalaumu wanaoishi hivyo but nimeona saana

the boss wapo wanaoweza kuongea matatizo yao japo madogo na bado hawapati support.
Kuna siku kwenye mgahawa flani alipita mtu amechafuka sana akaenda meza ya jirani. Baada ya muda yule mtu akawa anaondoka akatupita meza yetu, mdada wa meza ya jirani alikuwa amekaa na wakaka wawili akawa anacheka kwa dharau huku anasema "huyu jamaa vipi, eti naombeni mia mbili, sijui katokea wapi anafikiri watu wana hela za mchezo"
wakati nataka kulipa hela ya msosi mkaka mmoja wa pale akaniambia nisilipe atatulipia.
Hebu imagine watu walivyo na roho ngumu yaani watu wamekuwa na utaratibu wa kusaidia wanaojiweza.
 
Usitoke nje ya mada lol .............Elezea milango ambayo angeitumia huyu dada (kama kweli alichoshwa na hali ngumu ya maisha kama huyo kamwanda wako)
Ni hivi: Kazi amekosa, kila akitafuta hapati. Seriklini pia amekwama. Labda nauli ya kurudi kwao Kenya pia kakosa. Watoto wanalia njaa...........Angefanyaje zaidi ya kufanya ile biashara kongwe zaidi kupata kutokea duniani?............Hata Mungu asingemhesabia dhambi naamini.

Haya nigongee LIKE nipate appetite ya kula ugali mchana.
 
Nakumbuka tulipokuwa wadogo tulikuwa na majirani ambao kidogo walikuwa hawana uwezo; you can't imagine baba alikuwa akinunua gunia la sukari basi jua hata kilo kumi zinaenda kwa jirani. Yani kuomba chumvi ilikuwa si shida. But these days we are more westernized; (sijawahi kuona mtu anaomba chochote kwangu wala mimi kuomba kwa mtu).
NK hapo kwenye mabano umenikumbusha kaka yangu. Tulikuwa tunapatana sana kupita kiasi. Kuna kipindi nilimwomba anisupport issue flani akakubali. Huwezi amini nikawa nikimpgia simu hapokei, nikajaribu siku kumpigia kwa namba nyingine akapokea. akakata mawasiliano ikabidi na mimi niuchune. Tangu mwaka juzi nimekuja kuonana nae mkoani last week ananilaumu nimekuwa kimya.
Nimegundua unaweza wapoteza wapendwa wako kwa sababu umewaomba msaada.
. Sishangai kuona mtu anauwezo ila hassuport ndugu au jamaa zake. Binafsi kuna ndugu ambao nilijitahidi kuwapa support lakini waliishia kuniumiza, nahisi hata nikiwa na mabillioni nitakuwa nawaangalia tu.
 
Lizzy aksante sana kwa hii thread ingawa inasikitisha sana. Poor kids jamani mbona wiki hii imeanza vibaya kwangu?? Hizi habari za ukatili kwa watoto zinaniweka kwenye wakati mgumu sana wapendwa. MUNGU tusaidie

Lizzy darling hii pia inachangiwa na kutokuwa na uchaji wa MUNGU na upendo kwa wenzetu. Hivi ulishawahijaribu kugawana kidogo ulichonacho na asiye nacho?? faraja unayoipata moyoni ni kubwa sana na pia unafungua milango ya baraka hebu watu tujifunze kusaidia watu wenye shida tuone.
MJ1 huu mwezi umekua mbaya sana kwakweli. Habari mbaya kila upande...

Binafsi najua raha ya kumpa kidogo unarona anahitaji...ila kwa case kama ya huyu dada angesaidiwa vipi na mtu/rafiki wakati hamna aliyejua kwamba mambo yamemzidia kupitiliza?! Naamanisha kwamba ni rahisi kumspot mtu anaehitaji pesa ya lunch pale posta akiwa anaomba omba ila unajuaje kwamba hata aliyevaa vizuri kama wewe nae anahitaji msaada wa aina yoyote ile?!
 
nakubaliana nawe dawa chungu...
huko ulaya ukijibana vizuri hukosi kazi hata
ya kubeba maboxi.. si lazima system yaonekana
yeye alikuwa ana "depend "sana kwenye hizo system na
alikuwa hana plan nyingine zikikataa..
Dada alishapoteza “box“ lake bwana...na kupata kazi kuna sehemu ni ngumu sana kwakweli.

Mbu you are right..,ni ngumu kweli kumhukumu huyo dada bila kujua nini kilikua kinaendelea kichwani kwake.

Babu nanyoosha mkono kujua kilichoendelea...
 
Namsikitikia sana huyo dada na watoto waliondoka duniani kwa makosa ambayo sio yao
Ila niseme bado sana hii issue ya kuwaambia watu matatizo yako au kushare mambo ya muhimu au matatizio yanayotukabili bado sana
Watu wako tayari kufa na tai shingoni kuliko kusema kile ambacho kiko moyoni mwake
Na kuwepo kwa unafiki mwingi kwani hakuna ule urafiki haswa yaani ule ambao naweza nikakuambia tatizo langu na wewe ukalifanya lako na ukakaa nalo moyoni mwako au ukanipa ushauri ambao unanisaidia

Watu wanaogopana maana naweza nikakueleza jambo langu na baada ya kukuambia linakuw ataarifa ya habari kwa kila mtu wa mtaaani au unakofanyia kazi wewe ukalijua
So ili kuepuka kuonekana kituko mbele za watu ndo maana watu wanaamua kukaa na mambo yao moyoni mwao.
Na ndo maana bado kuna rate kubwa ya watu wanaojiua na kuacha ujumbe kuwa nimesongwa na mawazo au sijui ni ugonjwa fulani umenisumbua muda mrefu nimeona bora nijuiue ila angekuw ana mtu wake anayemwamini akaakaa nae akamweleza hali halisi na akapata ushauri sidhani kama kungekuwa na haya mambo ya kuua familia au kujiua
 
Back
Top Bottom