Lord Jesus. ..
Namshukuru mno mno Mungu wangu wa mbinguni, kwa kunipa neema ya kuiona siku hii, na kunipa kibali hiki cha kuweza kuandika maneno haya kwenu muda huu "AHSANTENI SANA"
Nilimpoteza baba yangu kipenzi mnamo tarehe 20/10/2016, and sincerely support niliyoipata kutoka JF, ni zaidi ya nilivyofikiria. Mmeninyenyekeza, mmeniheshimisha, mmenifariji mno mimi na familia yangu katika kipindi hiki kigumu. Nilikuwa na watu wa JF kuanzia ile asubuhi tumempeleka baba hospital, by the time mmepata taarifa za msiba, wengi walinitafuta kunipa pole, nimekuta PM's nyingi za pole, nimesoma comments za ule uzi wa Tanzia, aiseee mmenitia moyo watu wa Mungu.
Ahsanteni kwa walionipigia simu, texts, PM's, Ahsanteni kwa michango ya rambirambi, popote mlipotoa Mungu akawarejeshee maradufu , kwa waliofika msibani, hata kama hatukufanikiwa kuonana, ninashukuru sana kwa sababu mlikuwa sehemu ya majonzi yetu. Ahsanteni sana kwa maombi yenu, kwa sababu mwisho wa siku Faraja ya kweli inatoka kwa Mungu.
Ni yeye peke yake mwenye uwezo wa kuona ni kwa kiasi gani mioyo yetu imejeruhika, ilivyopondeka na kuumia. Na ni yeye pekee awezaye kuiganga mioyo yetu iliyoumia mno, na kutufunga mikanda ya sirini ili tuendelee mbele na safari yetu ya kwenda mbinguni
Sina hata cha kusema, maana kwangu bado ni kama ndoto, lakini Ninashukuru kwa hili pia, kwa sababu Mungu amesema tushukuru kwa kila jambo. Ingawa kwa udhaifu wetu wa kibinadamu, kuna muda na sisi tulikufuru, tulilalamika, tukatoa mapendekezo yetu wenyewe, labda ningetangulia mimi, Mungu itakuwaje sasa etc, badala ya kusema "AHSANTE MUNGU", hivyo tunaomba tu rehema.
Kweli mawazo na njia za mwanadamu si sawa na mawazo au njia za Mungu. Na Mungu ametuambia pia kuwa anayajua mawazo atuwaziayo sisi, si mawazo mabaya ni mawazo ya Amani + He works all things for his good. Kwa hiyo katika hili pia, Mungu ameambatanisha na mema yake pia, ambayo atayafunua tu kwetu Kwa wakati wake. Sisi inatupasa tu kushukuru, Kwa sababu hata tukifanyaje, hatutobadilisha ukweli kuwa baba yetu ameshatutoka na hakuna siku ambayo tungekuwa tayari kusema kuwa eti sasa hivi baba unaweza tu kwenda, nope.
Kama tungeweza tungeomba tuendelee tu kuwa wote milele. Ila ndo hivyo mpendwa wetu ameshatimiza kusudi lake hapa duniani. Tunamuombea tu apumzike kwa amani
Above all namshukuru huyu Mungu wa mbinguni Kwa neema hii kubwa. Huwa nasoma tu comments za watu humu wanavyoumia kuwa hawakuwahi kuwafahamu baba zao, Kwa kukataliwa au baba zao kufariki mapema n.k. Lakini mie HS hadi uzee wangu, nimekuwa pamoja na baba yangu.
Hakunipa tu damu yake, alinipa na jina lake na kila kitu chake ambacho aliweza kunipa (kuna comments kibao nilimuongelea baba yangu humu). Na yote hayo ni Kwa neema tu ya Mungu, wala sio kwamba nilistahili kuliko hao wengine. So namshukuru Kwa miaka hii ya Neema ya kuwa pamoja na baba yangu.
Even though a huge part of me has gone with him, bado nina kila sababu ya kushukuru Kwa sababu i have the best memories with him na bado ninaye baba yangu wa Kiroho, ambaye hatoniacha, hatonipungukia wala kufariki.
Kwa niaba yangu na familia yangu, tunasema tu "AHSANTENI SANA SANA". Mungu wetu wa mbinguni awabariki mno Kwa baraka zote za rohoni na mwilini, na kama mlivyonikimbilia HS, siku nyingine tukamkimbilie mwenzetu mwingine kumfariji. Mnisamehe tu kwa sababu nikisema nimtaje mtu mmoja mmoja ntajaza kurasa na kurasa. Ila mjue tu HS anawashukukuru na kuthamini kwa yote mliyomtendea katika kipindi hiki kigumu zaidi kwake.
Pops, we'll cherish you more, and mourn you less. May Your Gentle Soul Rest In Perfect Peace till the day we join you. Amen.
It is well. ..It is well with my soul.
[emoji120] [emoji120] [emoji120]