Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa

Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa

Hivi huyu Frederico Tluway Sumaye atazinduka lini ndotoni aweze kufanya maamuzi magumu!? majuzi tu kule Hanang wakati wa chagizi za ndani ya Chama chake alienguliwa kwa njama hizo hizo za rushwa leo; kina Mary Nagu wakapeta, akalalamika saaaaana; leo hii anatwambia kwamba bado anasubiri kujiridhisha na kitu gani tena! hivi Sumaye anasubiri mpaka yeye mwenyewe alanguliwe kwa rushwa ndio azinduke kwamba CCM haina dawa; CCM ni rushwa, ufisadi, ukatili na ujangili mpaka ahera!
 
Rushwa izidi hapa iweje? Huyu nae ni mnafiki tu abaki huko huko na rushwa zao

Mkuu nakubaliana na wewe. Kipimo cha rushwa kuwa imezidi, ipo Kati au imepungua Ni nini! Yeye aliicha katika scale ipi. Rushwa kwani imekuwa chumvi au sukari kujaji kwa kulamba?
Alishughulika na kesi ngapi za rushwa wakati wake? Mambo ya ovyo mangapi ya ovyo yalitokea wakati wake? Leo anakuja kusema eti walifanya makosa kufuta michezo shule za msingi na sekondari. Na eti anayaona sasa hivi wakati akitafuta kugombea urais. Duh..... Twesha!
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Kipimo cha rushwa kuwa imezidi, ipo Kati au imepungua Ni nini! Yeye aliicha katika scale ipi. Rushwa kwani imekuwa chumvi au sukari kujaji kwa kulamba?
Alishughulika na kesi ngapi za rushwa wakati wake? Mambo ya ovyo mangapi ya ovyo yalitokea wakati wake? Leo anakuja kusema eti walifanya makosa kufuta michezo shule za msingi na sekondari. Na eti anayaona sasa hivi wakati akitafuta kugombea urais. Duh..... Twesha!

Kipindi chake watu walikula 10% ngapi ,za IPTL , RADA ,migodi na EPA uliyo kuja kugundulika mwishon . Au kwakuwa waandishi wa habari walifungwa midomo na vitisho ndo akafanikiwa kumalizia hizo awamu mbili
Eti anajiona msafi leo wakati mambo ya ovyo ovyo aliyasimamia yeye
Ache unafaki huu mzee
 
Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema iwapo misingi ya uchaguzi ndani ya CCM italalia kwenye rushwa, Hataendelea kuwa mwanachama na kuonya kuwa tatizo hilo limefikia pabaya na litakiangusha chama hicho.

Source: Mwananchi
 
Hana jipya huyo anasubiri ashindwe kwenye kura za maoni ndio atimuke ni kama anajiwekea akiba
 
na yule zero brain naye anatishia? 10 years kama PM amelifanyia nini taifa hili zaidi ya kuliibia na kujimilikisha mashamba huko morogoro na kwengineko ambako hata hayaendelezi. aende tu huko?

Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema kwamba ikiwa rushwa itazidi ndani ya chama chake chama cha CCM, atajiondoa kutoka chama hicho. Haikuweza kufahamika mara moja kama atahamia chama gani lakini kuna tetesi kwamba huenda akahamia CHADEMA.
 
Sumaye vipi Tena, CCM na rushwa si tayari ni mapacha, au Ana maanisha rushwa ikipitisha mgombea wa CCM urais mwakani?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Rushwa izidi hapa iweje? Huyu nae ni mnafiki tu abaki huko huko na rushwa zao

Noti mpya,

Hili ulilouliza ni swali langu hili.

Anyway, ya nini kugombea fito wakati tunajenga nyumba moja?

Itoshe kuwashangaa waandishi wa habari wa Tanzania, yaani hata kuuliza ufafanuzi wa nini anamaanisha kwenye hili neno? Tukijiaminisha ati Sumaye anabariki kiwango hiki cha rushwa tutakuwa tunakosea? Hivyo, iko wapi dhima ya 'zero torelance to corruption?'

Mbona majanga haya!
 
Mkuu Tipau, asante kwa taarifa hii!. Huyu naye?!, eti kama rushwa itazidi?!. Ndani ya CCM, anataka rushwa izidi mara ngapi zaidi ya hii rushwa iliyopo?!. Sumaye anataka ikizidi kufikia kiwango gani?, hapo ilipo ndani ya CCM, rushwa imeisha zidi hadi kufurika kitambo!, sasa huyu anayeulizia kama rushwa ikizidi, anaulizia CCM ipi?!.

Sumaye aseme tuu, baada ya UKAWA kukosa mgombea mmoja wa 2015, wamemuomba yeye agombee and in principle atakuwa kakubali, sasa anatafuta pa kutokea CCM, ili aeleweke na jamii imuelewe!. Tena namshauri afanye hivyo mapema, kabla jamaa zake hawajabadili ile sheria ya viongozi wakuu wastaafu na kuongeza kipengele "kiongozi mkuu mstaafu atalipwa mafao na marupurupu stahiki" only if hatajishughulisha na siasa basada ya kustaafu!" kwani kuendelea kujishughulisha na siasa nayo ni ajira!.

Hajajifunza tuu kwa wenzake!, Mwalimu Nyerere Foundation, Benjamin Mkapa/IOTF, sasa JMK Foundation/WAMA on the making, na yeye aunde NG'0 yake!, hive ile HOPE FOUNDATION imeishia wapi?!.

Thanks.
Pasco.
mkuu nimeipenda sana hii hoja yako. ni kweli kabisa tena hili lingekuwepo kwenye katiba kuwa mtu asipate masurufu yake kama bado yupo kwenye siasa.
 
Mzee Sumaye sijakupata vizuri, unasema Rushwa IKIZIDI unaondoka CCM mara moja - key word hapa in KUZIDI.

kwa mantiki hiyo unakubali kwamba rushwa ndani ya CCM ipo na imeota mizizi, ila kama itapitiliza basi utaondoka, lakini kama itabakia kwa kiwango hiki hiki basi utaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama, tunataka ufafanuzi kwenye kipande hiki.

Tunanavyo:

Kama umeafiki kwamba Rushwa ipo ndani ya CCM , kwa nini sasa usichukue hatua muda huu huu ili kizazi cha sasa na kichacho kikukumbuke kwa ujasiri wako wa kuipinga rushwa kwa vitendo?, anza wewe na wengine watakufuata kwani rushwa ndani ya CCM haiwezi kwisha sababu ni ya kimfumo - tunataka vitendo Mheshimiwa.

Tunakusubiri n'gambo ya pili.
 
Waache wafu waziKe wafu wenzao.Kama inatoka moyoni hongera sana kwa ufunuo mpya.Kwani hujui kwa nini sisi tunapenda kupokea CHOPA? Yalishatushinda zamani.Wewe unaona wapi mwizi wa kuku anafungwa miaka mitatu mwizi wa EPA na ESCROW anakaribishwa ikulu na anapewa juisi kama naye ni Profesa Lipumba au Dk Slaa? Prof na Dr wakienda ikulu huwa wamebeba machozi mazitto ya walalahoi kwa machungu hata juisi huwa hawanywi.Wanamwachiaga Lukuvi na WASIRA.UKIIJUA KWELI ITAKUFANYA HURU na hapo utaombea UKAWA TUMAINI LETU idumu milele
 
Anataka rushwa izidi kwa kiasi gani wakati CCM hupati kitu chochote bila kutoa rushwa.CCM siyo kimbilio la wanyonge tena kimekuwa chama cha mnyonge njoo ni kunyonge,nipe nikupe,mkono mtupu haulambwi.
 
Kulingana na habari hii,rushwa anayoiogopa Sumaye ni ya kwenye uteuzi wa mgombea wa urais CCM 2015.Kwamba ana wasiwasi jina lake halitapitishwa kwenye vikao vya chama vya mchujo,kwa vile washindani wake watamzidi katika kuhonga wajumbe.Na hili likitokea basi atajiondoa CCM na kutafuta chama kingine kitakachompa tiketi ya kugombea urais

Vinginevyo rushwa na ufisadi wote uliotamalaki katika nchi hii kwake si muhimu kabisa.Rushwa inayomkera yeye ni ile tu inayogusa maslahi yake,yaani inayokwamisha mipango na harakati zake za kuwa rais wa Tanzania
 
Daah! Ina maana ameridhika kabisa na rushwa iliyopo?

Sometimes ni bora kunyamaza kimya tu!
 
Anafaa kumpigia kampeni dr Slaa
Karibu kamanda Sumaye

karibu sana cdm huku kwetu ruhusa ya kuropoka haipo utatengenezwa ukae kimya kwetu kazi moja tuu kuunga mkono maovu yote ya viongozi ukiropoka tutakubambika kuwa msaliti karibu kamanda
 
Sumaye bana utafikiri yeye hakuwa akipokea rushwa ama kweli watanzania sisi ni wanafiki sana. Mwambie ajiondoe mapema kwani akiendelea kukaa atajizidi kuumia roho kwani naye pia ni FISADI TENA PAPA!!!!!
 
Back
Top Bottom