Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa

Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa

Sumaye anawajua CCM wana mafao yake nk hawezi kuingia upinzania na Sumaye hana courage ya kufanya maamuzi magumu never .
 
Kuna kuzidi rushwa tena zaidi ya hapa au mtu mzima anatishia nyau.
 
Atakubali kuachia %80 ya mshahara wa Pinda.?
 
Ana taka ifike kiwango gani? CCM ya leo sio ya mwl Nyerere, Nchi iliyo kosa moral authority kwa sababu ya rushwa na impunity attitude
 
Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema iwapo misingi ya uchaguzi ndani ya CCM italalia kwenye rushwa, Hataendelea kuwa mwanachama na kuonya kuwa tatizo hilo limefikia pabaya na litakiangusha chama hicho.

Source: Mwananchi
rushwa izidi hapo ilipofika ndio aachie ngazi! muongo huyu
 
Akina Shibuda hawataishaga Tz!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Daah! Ina maana ameridhika kabisa na rushwa iliyopo?

Sometimes ni bora kunyamaza kimya tu!

Awamu yao (Mkapa/Sumaye) Jaji Warioba aliwasilisha ripoti kuhusu masuala haya ya rushwa ndani ya TZ. Hawakuifanyia kazi hata tone - kwa hiyo ina maana waliridhika na rushwa kwa kiwango kile kilichotisha.

Anyway msameheni bure huyu kaka yangu. Ndani ya miaka miwili iliyopita amechanganywa sana na mama Nagu na team Lowasa ambao wamemtifulia kabisa ndoto/uchu yake ya kuutwaa uraisi.
 
Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema iwapo misingi ya uchaguzi ndani ya CCM italalia kwenye rushwa, Hataendelea kuwa mwanachama na kuonya kuwa tatizo hilo limefikia pabaya na litakiangusha chama hicho.

Source: Mwananchi

kumbe rushwa ipo ccm ila haijazidi!!
 
Kwamba hii inayotolewa sasa haitoshi ! Labda kama hataki kuhama.
 
ccm rushwa ndo sera yao kwani Sumaye alikuwa hajui
 
Huyu nae chadema wakimpokea watajishusha zaidi katika kipindi chake ndie aliyewahujuma wapinzani kuliko hata sasa alifika mahali akahoji uraia wa J .ULIMWENGU akitaka gazeti la rai lijieleze limepata wapi fedha za kuendesha shuguli zao kwakuwa tu lilikuwa linawachambua yeye na mkapa na serikali, akatoa kauli iliyosababisha serikali kukosa mapato kuwa UKITAKA MAMBO YAKO YANYOOKE WEKA BANDERA YA CCM kwenye biashara na kwenye magari wapitisha magendo wote waliweka na kweli mambo yaliwanyookea hakuna afsa wa TRA aliewasogelea
 
Sumaye vipi Tena, CCM na rushwa si tayari ni mapacha, au Ana maanisha rushwa ikipitisha mgombea wa CCM urais mwakani?


Sent from my iPhone using JamiiForums

Kulingana na habari hii,rushwa anayoiogopa Sumaye ni ya kwenye uteuzi wa mgombea wa urais CCM 2015.Kwamba ana wasiwasi jina lake halitapitishwa kwenye vikao vya chama vya mchujo,kwa vile washindani wake watamzidi katika kuhonga wajumbe.Na hili likitokea basi atajiondoa CCM na kutafuta chama kingine kitakachompa tiketi ya kugombea urais

Vinginevyo rushwa na ufisadi wote uliotamalaki katika nchi hii kwake si muhimu kabisa.Rushwa inayomkera yeye ni ile tu inayogusa maslahi yake,yaani inayokwamisha mipango na harakati zake za kuwa rais wa Tanzania

Nyie ndio mmeelewa anamaanisha nini! Bravo
 
Back
Top Bottom