Sumaye: Mafisadi lazima watoswe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye: Mafisadi lazima watoswe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jul 8, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini, rushwa na ufisadi vinatishia mustakabali wa amani nchini na kusisitiza kuwa mafisadi ndani ya CCM lazima watoswe. Sumaye alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Soko la Pasua, mjini Moshi alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya chama cha TANU kutimiza miaka 57 tangu kuanzishwa kwake.

  “CCM ni chama cha wanyonge kwa maana yawafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wanaofanya biashara halali…. Lakini kuna dalili inayoonyesha kuwa CCM sasa kimeanza kutekwa na wachache wenye uwezo wa kifedha,” alisema Sumaye.

  Katika hotuba hiyo iliyovuta hisia za wananchi na wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo, Sumaye alisema japokuwa mambo hayo yanauma, lakini ni lazima WanaCCM waelezane kuhusu mwelekeo wa chama chao.

  “Mwelekeo huu ni hatari kwa chama chetu na kwa mustakabali wa taifa letu…,tusijidanganye ni lazima tujue kuwa Watanzania wengi wanaitegemea CCM, hivyo lazima ikae katika msingi unaoeleweka… Hatuwapigi vita wala kuwachukia matajiri ila wasikiteke nyara chama,”alisisitiza Sumaye.

  Jambo lingine alilosema ni hatari kwa mustakabali wa nchi, ni mgawanyo mbaya wa utajiri akisema katika nchi yoyote duniani, lazima watakuwepo matajiri na masikini, lakini tatizo ni pale kundi dogo linapohodhi utajiri wa nchi husika.

  “Tatizo hapa ni kundi la watu wachache wanapotaka kuhodhi utajiri wa nchi… Hali hiyo si salama kwa matajiri na si salama kwa masikini na wala si salama kwa nchi nzima,” alisema sumaye huku akishangiliwa na wana CCM na wananchi wengine.

  Aliongeza kusema”wale wasionacho kama ikitokea na dalili hiyo imeanza kujitokeza katika nchi yetu …wale masikini watapigana na wale walionacho bila kujali kama ulichonacho ulikipata kwa halali ama la”.

  Sumaye aliwataka Watanzania kutofikia huko na kudokeza TANU ililisimamia vizuri jambo hilo na CCM ni lazima nayo ilisimamie akisema taifa ni lazima lijenge mfumo utaohakikisha utajiri hauwi kwa watu wachache kwani hiyo ni hatari kwa amani.

  Kuhusu suala la rushwa ambalo limekuwa likipigiwa keleke nchi nzima, Sumaye alisema tatizo hilo limeanza kuota mizizi nchini na kwamba, kama Watanzania hawatakuwa na ujasiri wa kuikata basi utaiua CCM na nchi.

  “Tutaua chama chetu na hata nchi yetu….ni lazima tuwe na ujasiri wa kukata mizizi ya rushwa….tusiposimama kidete huduma za jamii zitakuwa zinapatikana katika kundi la watu wachache wenye uwezo wa kifedha,”alisema Sumaye.

  Sumaye alisema Ufisadi ni mbaya zaidi kuliko wizi akisema tatizo hilo lipo nchini na linaonekana kukua kwa kasi na kushika mizizi kwa nguvu.

  Kauli hiyo ya Sumaye ilionekana kuunga mkono tamko la Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) lililowataka wanachama wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi wakiwemo Wabunge, kujiuzulu wenyewe vinginevyo CCM itawawajibisha.

  Lakini mbali na tamko hilo, lakini kauli ya Sumaye ambaye anaonekana kuwa na nguvu ndani ya CCM imekuja wakati kuna sakata la ufisadi katika ununuzi wa rada ambapo Mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani, Andrew Chenge anatajwa.

  Vyombo vya habari jana vilimkariri katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dk. Wilbroad Slaa na Waziri kivuli wa sheria na mambo ya katiba, Tundu Lissu wakisisitiza upo ushahidi wa kumtia hatiani Chenge.

  Chenge mwenyewe mara zote amekanusha tuhuma hizo na jana alikaririwa akiwataka wenye ushahidi kuuwasilisha Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) huku akisema uchunguzi wa tuhuma hizo ulishafungwa.

  MWANANCHI
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  SUMAYE: CCM imetekwa na Matajiri wanataka kuisambaratisha waondolewe (TBC1)
  JK: Viongozi msipende anasa (Mwananchi) na Viongozi acheni kulindana (Majira)

  Ama kweli nyani haoni....., hata kama vitabu vya dini vinasema usifuate ninayotenda, fuata ninayosema, lakini viongozi wetu wanatakiwa waonyeshe mfano wa matendo ya yale wanayoyasema, JK acha anasa na kulindana ndipo uwaambie wengine.

  Hivi na wewe Sumaye ni masikini? acheni kutuyumbisha na kauli zenu zilizokaa kikampeni kampeni.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,350
  Likes Received: 22,204
  Trophy Points: 280
  Ataje orodha ya mafisadi ya tangu mwaka 1995 hadi leo, na kisha tuwapeleke mahakamani.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  vitabu vya dini gani vinasema hivi? unatupotosha nahisi..
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sumaye ni mnafiki saizi ndio anajifanya kutaja mafisadi? Huyo Sumaye si ndio alisema kama mfanyabiashara yoyote anataka mambo yake yaende vizuri ajiunge CCM
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hizi kelele ni kila siku..lakini hakuna mwenye ujasiri wa kutaja list ya mafisadi kwa majina

  hii ni kuwahadaa watanzania
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Sumaye anacheza kamari tupu......................kashfa nyingi za ufisadi zilipikwa wakati yeye ni PM......swali ni je alichukua hatua zipi? Hivi kwa miaka kumi ya U-PM wake anaweza kutueleza ni kesi ngapi ambazo watuhumiwa wa ufisadi akiwemo yeye na Mkapa waliwahi kuhojiwa na Takukuru au polisi.................

  Tunajua Sumaye anawaniwa U-Raisi lakni asichojua ni kuwa historia hujirudia yenyewe ukimwondoa Nyerere tu hakuna ex-PM alifanikiwa kuwa Raisi....hivyo yeye na EL.......waandike maumivu makali........mwulizeni Warioba, Malecela, Kawawa, Msuya, Salim Ahmed Salim n.k...................
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  lile shamba la kibaigwa alilokuwa analima kwa nguvu huku magereza wakidai ni eneo la magereza alishawarudishia huyu sumaye ?
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Jingine ni kuwa na hili ni la kisaikolojia.........................Sumaye anafikiri kwa kukemea ufisadi akiwa nje ya madaraka wale waliopo madarakani watamwogopa na kusahau ufisadi wake binafsi wa kujirundikia mashamba na mali za umma....ukweli ni kuwa wakizidiwa hawa waliopo madarakani watamtoa yeye kafara.........................
   
 10. Chaser

  Chaser Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhe. Sumaye nimejaribu kukupigia bila mafanikio. Nadhani katika harakati za kuimarisha chama chetu, tulipewa maelekezo ya kuacha kukurupuka na kutoa lawama nje ya vikao. Hii, bila shaka, inawapa nguvu hawa watu wa JF kuendeleza haka kamtandao kao na kukifanya chama kionekane kinadorora. Kama kada wa chama, aghalabu huwa napata shida ninapofika vijijini na kuulizwa maswali juu ya misimamo inayokinzana ya baadhi ya viongozi wetu wastaafu. Mhe. unajua hata kukaa kimya muda mwingine ni kelele tosha.
   
 11. s

  sanjo JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Sikio la kufa halisikii dawa. Matatizo ya kupoteza maadili ndani ya chama cha magamba ambayo yamewagharimu sana watanzania hayawezi kumalizwa ndani ya chama chenyewe. Hilo lazima Watanzania walijue na wakabiliane nalo.
   
 12. 2

  2nd edition Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na lile la kilosa alilolitelekeza hadi wankijiji wakalichukua then akaenda kuwatoa vp ataliendeleza lini au ndio land grabing and holding technique? na je hiyo haimfanyi na yeye kuwa fisadi? au nyani haoni k......nd...le
   
 13. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Teh teh teh sasa watatoswa lini jamani!!!!!!!!
   
 14. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hizi ni kauli za kutia moyo sana na pengine zinalenga kukiokoa chama. Hata hivyo mzee uwe unayazungumza haya kwa hisia hizo hizo wengine wanapoongea kwenye vikao vya chama, maana wale wanaoongea wanaonekana wana chuki binafsi na mafisadi au wanautaka urais wa 2015.
   
 15. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  “CCM ni chama cha wanyonge kwa maana yawafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wanaofanya biashara halali…. Lakini kuna dalili inayoonyesha kuwa CCM sasa kimeanza kutekwa na wachache wenye uwezo wa kifedha,” alisema Sumaye.

  Mheshimiwa hawa kwenye red mmewaongeza lini? Hata kwenye bendera bado Nyundo na Jembe vinapepea.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nakumbuka kabisa aliwahi sema hivyo...
  Nadhani nae yupo kimaslahi vilevile...
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sio wastaafu tu hata waliopo nao pia misimamo yao haieleweki, leo Nape kasema hiki, kesho Mkama anamkana.....
  Hili ni tatizo....
   
 18. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Je tujiulize SUMAYE YEYE NI MSAFI KWELI AU ANAJIPENDEKEZA. Mfano wa kule NSSF, Mashamba ya Turiani.
   
 19. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ngoja niwachukulie zoezi
   

  Attached Files:

 20. M

  Marytina JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  shamba lililokuwa linazungumziwa ni hili la Kibaigwa

  in short ni mtandao wa JK uliomchafua SUMAYE 2005 KWA KUMZUSHIA MAMBO KEDEKEDE
  but tupe details za NSSF na ushiriki wa SUMAYE?
   
Loading...