Sumaye: Mafisadi lazima watoswe

Don't be silly, msitumiwe na mafisadi halisi (Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) kupoteza mwelekeo. Sumaye si fisadi, ni waziri mkuu mstaafu anayeishi maisha ya kawaida tu. Alikopa 50m/- PPF si NSSF na alizirudisha pesa hizi. Ni mkulima tu ana mashamba na mifugo ya kawaida sana.

Ukimfananisha na Lowassa na Chenge, Sumaye ni masikini sana. He has moral authority kuwanyooshea vidole mafisadi.
 
Don't be silly, msitumiwe na mafisadi halisi (Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) kupoteza mwelekeo. Sumaye si fisadi, ni waziri mkuu mstaafu anayeishi maisha ya kawaida tu. Alikopa 50m/- PPF si NSSF na alizirudisha pesa hizi. Ni mkulima tu ana mashamba na mifugo ya kawaida sana.

Ukimfananisha na Lowassa na Chenge, Sumaye ni masikini sana. He has moral authority kuwanyooshea vidole mafisadi.

mnataka kuwatosa baada ya kuwatumia vilivyo kupata ushindi mwaka 2005? hapa ndipo kwenye tatizo na ndiyo maana tunasema kama ufisadi basi ni wenu nyote na si hawa 3 tu wawe mbuzi wa kafara.
 
Nahisi kama Ex - Pm ameanza kampeni mapema!!! tete teteh ,lakini hapa anajaribu kutumia upepo wa kisiasa kusafisha njia yake, Na mpinzani wake ndio anataka atoswe!!! Ongeza Bidii, Je akiswa wewe utapata?
 
Mheshiwa rais jana umeelekeza watumishi ndani ya chama waache anasa- saafi,swali linalotusumbua wengi ni kwanini walio chini yako hawayaishi/kuyatekeleza maagizo yako? au hawajui kuwa uliwahi kuwa mjeshi...Mheshimiwa Sumaye no matter kama shutuma dhidi yako zina ukweli au la, ila jana huko moshi umesemaa!; Ya kwamba gap kati ya walio nacho na wasio nacho sasa ni hatari kwa usalama wa nchi) siku zote vita ya walio nacho na wasio nacho ni mbaya na tena ni bayana kati ya UMMA na wachache.., mara kadhaa nimewasikia waheshimiwa tena bungeni kwamba wao watakimbia na watakao athirika ni kina mama na watoto(wananchi au' watu wa kawaida') sijui wanapata wapi ujasiri wa kusema hivi tena ndani ya jengo la wananchi,msijidanganye ninyi ni wachache ktkt ya wengi, hili jambo ni kumwomba sana Mungu litupishe mbali. CHUKUENI HATUA,BADILIKENI sasa, kwa MUNGU hutaulizwa ulikuwa nani au ulimiliki nini duniani...mobutu yuko wapii..
 
Japo yeye kasema,Kuna mawazili wakuu wengine ambao jamii ina waheshimu kweli kweli,lakini wamekaa tu kimya hawataki kusema na kujitanabaisha kuwa wako wapi upande wa umma au upande wa Mafisadi?Ndio maana hata walipopakaziwa kuwa ni Vijana wa HIZBU wakati sio kwa kuwa HAWAKUJITANABAISHA NA JAMII,jamii haikujua ni vipi kuwatetea.

Kujitanabaisha kunaondoa wingu na jamii inajua kuwa huyu yuko upande upi. Tanzania kama Taifa uwa linajitanabaisha kuwa HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE,sembuse wewe binadamu.Kujitanabaisha ni nguzo hata pale utakapo onewa jamii yako inajua wewe ni wa mrengo upi.


Judge Joseph Sinde Warioba,alishajitanabaisha,Spika wa Zamani Samweli Sitta nae alishajitanabaisha na hata ilipotekea kutendewa ndivyo sivyo jamii ilisimama nae na kuakikisha kuwa yeye na wafuasi wake waliosimamia upande uliojitanabaisha wanapata heshima yao kwenye jamii.Sio siri ili liwazi kitokee cha kutokea Spika huyo apigwe chini sasa hivi uone kifuatacho ITV.Yote hiyo ni msimamo wako kueleweka ndani ya jamii,aijarishi una mamlaka au la bali kwa heshima ambayo jamii imeshakupa unastahiki kutoa msimamo wako,vinginevyo ni kuhujumu Taifa.

Mfanyabiashara maarufu mwenye heshima kwenye jamii alishajitanabaisha toka miaka hiyo na ndio maana chochote kinapotekea kwake kwa nia ya kumuhujumu kwa kuwa jamii hiko nyuma yake na inamjua inamlinda na kuhakikisha hafanyiwi mchezo mchafu.

Hata waziri mkuu wa zama hizo Mzee John Malecela na Mzee David Cleopa Msuya wote hao walishajitanabaisha,hata marehemu tunu ya mwisho mwisho kwa Watanzania, Simba wa vita Marehemu Mzee Kawawa nae alijitanabaisha kuwa yuko upande gani.Tabia za viongozi wa zamani na wasasa kukaa kimya bila ya kujitanabisha mwisho wa yote uwa inakula kwao kwa kuwa siku wajanja wakitumia nafasi ya usafi wako kukuharibia pale unapotaka mambo mazuri ya kuchangia kwenye Taifa lako kwa dhamila ya dhati wanatia kitumbua mchanga.Na kwa kuwa UKITANABAISHA KWA UMMA wewe ni mtu wa aina gani,umma utakujaji kwa jinsi ulivyoharibiwa,na kwa kuwa ni desturi yako kukaa kimya ndio Taifa linabeba sumu hiyo kuwa wewe u mtu wa namna hiyo maadui zako walivyofanikiwa kukuhukumu kwa umma.

Kama mwanadamu lazima uwe na msimamo wako na ambao wanajamii zako wanakubalina nao hata kama hauwafurahisha baadhi lakini huo ndio ukweli kuwa uto wapendeza wote.

Mwalimu pamoja na ustaafu wake halipoona mambo hayako sawa kwa Watawala, Mwalimu aliita waandishi wa habari na kusema yaliyoko moyoni mwake kama Mtanzania huru na vilevile kama kiongozi mwenye uzoefu katika kuongoza Nchi.Huo ndio ubinadamu timilifu haijarishi uliongoza vibaya ama vizuri.

Vinginevyo kushindwa kutoa mawazo wakati Taifa liko katika hatihati zaa mitafaruku ya malumbano haya na yale ya wazi na yenye mijadala mizito iliyo wazi kwa kila Mtanzania na wewe,kama kiongozi uwe mstaafu au madalakani kushindwa kutoa msimamo wako kwa vigezo vya maamuzi ya pamoja [Collectively Responsibility] na uwanadiplomasia hata kwenye maslahi ya Taifa,ni matumizi mabaya ya utawala bora na ustawi wa Taifa na hayana budi kuhojiwa mbeleni kunani?

Kuna watu jamii,inajua wanajua na wana uwezo wa kutukwamua kwenye maisha haya yasiyoeleweka kesho itakuwaje,kutuondoa kwenye utayarishaji wa mabomu ya vijana wasio na kazi, kila siku ya Mungu kutokujua kesho itakuwa vipi wamekaa kimya tuli ka maji ya mtungini na kinachoendelea ni kama hakiwahusu,wakiangalia Taifa linavyoyumba wanasubiliwa kkupigiwa magoti kuitwa wasaidie.

Mzee Sinde Warioba hakuitwa amekuwa akipiga kelele huko aliko,hata Jakaya Kikwete anajua Sinde ni aina gani ya Mtu.Mkuu wa kwanza wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Mzee Salakikya hakuitwa, alipiga kelele huko huko aliko "jamani eeehh mlio huko ofisini huku site mambo si shwali",na mwangi wake umesikiwa na kila mmoja amejua Mzee yule amesema nini katika utu uzima wake ule.

Haijarisha Sumaye alikosea hau aripatia cha msingi nimejifunza kuwa bado unayonafasi ya kujitanabaisha kwa jamii ukizingatia mtu aliyepata kuwa kiongozi wa Taifa hili na kumiliki Madalaka makubwa ya maamuzi.Hata Rais Kikwete isingekuwa HAIBA YAKE YA KUJITANABAISHA angekula za uso,lakini Mungu saidia dakika za mwisho ni lazima kieleweke sifa kumi na tatu [13].

Japo na mapungufu ya Lowasa,lakini napenda jinsi anavyosimamia KUJITANABAISHA,anajulikana dhahili kwa kila kiongozi,mpaka Mwalimu mwenyewe anazikubali jeuri [guts] za Lowasa.Tatizo halikuwa kwa Lowasa tatizo liko kwa wale wanaohidhinisha nani awe nani,walipokuwa wanamtizama waliangalia tu tabia yake ya uthubutu [Aggresiveness] pasi kuanglia mipaka ya hiyo uthubutu wake.Walipaswa kujiuuliza jamaa huyu pia anatabia za ujasilimali je akiwa kiongozi akatumia uthubutu wake huo huo kupitia kutumia mamlaka yake pamoja na uthubutu kujitajirisha itakuwaje.Hayo ndio natumaini maswali ambayo Mwalimu alikuwa akijiuliza na kumuondoa kwenye listi yake ya uongozi kwa wakati huo kama kijana.

Tufike sehemu viongozi wasiojitanabaisha tuwamwage yanini kuwa na viongozi wanafiki.
 
Mhe. Sumaye nimejaribu kukupigia bila mafanikio. Nadhani katika harakati za kuimarisha chama chetu, tulipewa maelekezo ya kuacha kukurupuka na kutoa lawama nje ya vikao. Hii, bila shaka, inawapa nguvu hawa watu wa JF kuendeleza haka kamtandao kao na kukifanya chama kionekane kinadorora. Kama kada wa chama, aghalabu huwa napata shida ninapofika vijijini na kuulizwa maswali juu ya misimamo inayokinzana ya baadhi ya viongozi wetu wastaafu. Mhe. unajua hata kukaa kimya muda mwingine ni kelele tosha.

Namuomba Allah anipe uhai ili nione mbio za uRAIS 2015!! Hakika mtatoana macho!!!!
Hivo vikao vya chama unvyosema vipo tena!?? Si mmebaki manyang'au tu huko!!

HAkuna wa kumpiga breki mwenzake, mnapigana vikumbu tu kwa ulafi!!!!

Hakika, hukumu yenu itakuwa viwanja vya jangwani!!! Tutawawambwa mtini mlipie dhambi zenu hizi...
 
Huyu naye anataka mafisadi wafukuzwe? Yeye amejiweka kundi lipi? Amejipima? Tunaweza kuzungumzia ufisadi nchini na kumuweka nje Sumaye? Kweli Nyani haoni kundule!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom