Sumaye azungumza na waandishi; ajibu maswali masuala ya kitaifa

Kulikuwa na haja kweli ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari au ?

Si unajua tena Wanasiasa wabongo, akiona hajasikika siku nyingi basi ni lazima atafute namna ya kuropoka hata kama anachotaka kuropoka hakina maana yoyote ile kwa Watanzania.
 
Bahati mbaya siamini kwamba chochote kinachoweza kusemwa sasa kinaweza kubadili nyoyo za waandishi ambao tayari wameishakuwa 'mafisadi' wa uandishi. Kinachohitajika ni kuwachukulia hatua mmoja baada ya mwingine mara moja pale inapoonekana wameandika habari za uongo. Jukwaa la waandishi wa habari kama halina meno lipewe meno kwa ajili hiyo.
 
kwanza nampongeza sumaye kwa kuachia u-PM na kuachia u-MP na kwenda shule, kuacha siasa za chama at least for a while

namshauri pia aendelee na ukimya na upole huohuo kwani hali ya siasa sasa hivi ahiendani kabisa na furaha aliyo nayo kama raia wa kawaida na the longest serving PM
 
Huyo Billionea Sumaye hana Chochote zaidi ya kuwanunua waandishi wa HAbari,
swali ni kuwa kama lile gazeti la mwanzo lililomwandika kama ana Account nje mbona alilipeleka Mahakamani, lakini hili lingine mbona anaishia kwenye majukwaa tu.

anakuja mbele za watu kulialia ili aonekane rofa, kumbe ni tajiri wa kutupa, huyo Bwana ana boats za uvuvi na mpaka ndege yake mwenyewe katiak kiwanda chake cha samamki MAfia anamtumia mama mmoja wa kihindi,

na watu hawana habari, Buguruni karibu yote keshainunua kwa kutumia wanunuaji wake fake, muda si mrefu ataanza kujenga apartment zake hapo buguruni

hiyo ya Shamba na Kigoda ni la ukweli, kama anaonewa angeenda mahakamani

sumaye si bilionia propaganda dhidi yake zilikuwa fitna za uchaguzi zikiongozwa na waandishi walio kwenye payroll ya mtandao wa jk,lowassa na rostam....uliowaumiza wengi....,hata jeuri ya huyu mhariri kukataa wito wa baraza la habari inatokana na jeuri ya aliokuwa anawatumikia ambao saasa ndio wenye nchi!
 
Hii sheria ya kumtaka raisi awe na shahada ni sheria ya nchi (imo kwenye katiba) au ni utaratibu wa CCM tu?

Ule ulikuwa ni utaratibu wa muda wa kumzuia Mrema asigombee urais kupitia CCM. Imewekwa pending kama ikiotokea siku inaweza kutumiwa kwa watu wengine kama kina Guninita and alike, basi itasemwa hata ngazi fulani lazima at least uwe form 6.
Can you believe it, a rule against one person.
 
Kajichafua mwenyewe, hivi asharudisha mashamba ya kule Kilombero kwa wananchi? Ni fisadi tu!
 
Ameleta mchango wake kwa jukwaa la wahariri wa shilingi ya milioni 5. Anasema anatimiza ahadi yake aliyoitoa kwa jukwaa la wahariri..

Huu mchango kwa nini asiupeleke "dogodogo centre". This is benefit inkind anataka kuwaziba mdomo wahariri. TAKRIMA PERIOD, Nawashauri Jukwaa la Wahariri waukatae kwani una undue influence kuhusu kusudio lake la kumshitaki Mhariri mwenzao.

Angekuwa amefanya la maana kama angesema fidia atakayoidai toka kwenye shauri hili atasaidia kuilipa yeye kama mchango wake kwa jukwaa la wahariri. Ili mradi atakuwa ameshasafisha jina mahakamani
 
WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameonesha wasiwasi kuhusu sheria inayotarajiwa kutungwa ya kutenganisha siasa na biashara, huku akipendekeza kurudishwa kwa misingi ya Azimio la Arusha kwani itasaidia nchi kurudi katika maadili.

Licha ya kuweka wazi utenganishaji huo kuwa ni jambo jema na kuliunga mkono, alisema utekelezaji wake utakuwa mgumu kutokana na kutokuwapo mipaka ya biashara na ya maadili.

“Tukitaka kufanikiwa kwa kutenganisha siasa na biashara, turudi kwenye maadili na turudishe Azimio la Arusha,” alisema Waziri Mkuu huyo aliyekaa madarakani kwa miaka 10. Azimio la Arusha lilianzishwa mwaka 1967 ambapo misingi yake ilikuwa kujenga usawa baina ya watu, kuweka maadili katika uongozi kwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa rushwa katika uongozi. Lilizikwa mwaka 1992 Zanzibar.

Katika hotuba yake ya kila mwezi ya Januari mwaka juzi pamoja na kurudia mara kwa mara, Rais Jakaya Kikwete alieleza nia ya serikali ya kupeleka muswada bungeni wa kuanzishwa kwa sheria ya kutenganisha siasa na biashara, kwa kile alichokieleza kumekuwapo na mgongano wa kimaslahi.

Aliwataka mawaziri na wabunge kuchagua siasa au biashara, lakini si vyote kwa wakati mmoja. Sumaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa Sh milioni tano kwa Jukwaa la Wahariri jana Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa mafunzo ya maadili kwa waandishi wa habari.

Waziri Mkuu huyo mstaafu aliwahi kuahidi kutoa fedha kwa wanahabari wapewe mafunzo kutokana na fedha alizokuwa akidai mahakamani dhidi ya gazeti la Tanzania Leo ambalo alilishitaki kwa madai ya kumdhalilisha.

Fedha hizo ni sehemu ya malipo hayo. Aliunga mkono hatua ya wanachama mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumpigia debe Rais Jakaya Kikwete aweze kuendelea kuiongoza Tanzania katika kipindi cha pili.

Hata hivyo, Sumaye ambaye aligombea urais pamoja na Kikwete mwaka 2005 na kutopitishwa na chama chake, alisema si vibaya watu wengine wakajitokeza kugombea urais na kupigiwa debe huku kwa upande wake, akiweka wazi kutogombea nafasi yoyote katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Alipoulizwa juu ya kuwepo makundi ndani ya CCM, alisema “suala hilo halininyimi usingizi kwani CCM ni chama kikubwa makundi lazima yawepo, lakini CCM ina utaalamu wa kutatua matatizo yake, hivyo tutakwenda katika uchaguzi vizuri.” Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), alipongeza kupitishwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi, akisema sasa wagombea wasiokuwa na fedha, lakini wanapendwa na wananchi watashinda.

Mwanasiasa huyo alitetea kuwepo kwa mgombea binafsi, lakini akasema kwa Tanzania haitawezekana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutokana na marekebisho ya sheria kuchukua muda mrefu.

Akizungumzia sakata la ununuzi wa rada, alisema uamuzi wa serikali ulikuwa sahihi ila matatizo yalitokea kwenye utekelezaji wake.

“Kuna wakati ndege ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ilitaka kuanguka hapa nchini kutokana na kutokuwa na rada, mataifa mbalimbali yalishatishia kusimamisha ndege zao kuja nchini hivyo ilitulazima kununua rada,” alifafanua Sumaye aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wote wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye sakata hilo la rada lilitokea wakati wa utawala wake, alisema waliosimamia ununuzi huo walileta matatizo, lakini sasa wanachunguzwa hivyo uchunguzi ukikamilika wafikishwe mahakamani.

Miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kupokea rushwa katika ununuzi huo na kuilazimu serikali kununua kwa gharama kubwa kuliko gharama halisi ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Andrew Chenge.

Kwa upande wa suala ya wizi katika fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Sumaye alisema suala hilo halifahamu na wakati wake serikali isingeweza kuingilia mambo ya ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwani ilikuwa na Bodi ya Wakurugenzi waliokuwa wakifanya uamuzi.

Kuhusu kutangaza mali zake, Sumaye alisema kwa sasa haoni sababu ya yeye kutangaza na kusisitiza, “nilipoingia madarakani kila mwaka nilikuwa natangaza na baada ya kumaliza muda wangu nilitangaza, sasa nimeshakaa miaka mitano kama raia sihitaji kutangaza labda kuwe na tuhuma, nako si kuwaambia ninyi, bali vyombo vya usalama."

Alipotakiwa kuzungumzia mapigano yanayotokea katika maeneo ya Hanang mkoani Manyara na Tarime, Mara, alisema, “Tangu enzi za Mwalimu Nyerere (Julius), Tarime kumekuwa na mapigano ingawa sasa yamezidi hii inaonesha mmomonyoko wa maadili, Hanang tatizo si kubwa, viongozi wanaweza kushughulikia.”

Awali, alieleza kusudio lake la kulishitaki gazeti la Changamoto mahakamani kwa kumshushia hadhi yake, kwa kuandika habari inayoeleza kuwa akishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji, Dk. Abdallah Kigoda, walipora shamba la Mamlaka ya Chai la Mlangali Lupembe, mkoani Iringa lenye hekta 200 bila kulipa malipo yoyote serikalini.
 
sumaye si bilionia propaganda dhidi yake zilikuwa fitna za uchaguzi zikiongozwa na waandishi walio kwenye payroll ya mtandao wa jk,lowassa na rostam....uliowaumiza wengi....,hata jeuri ya huyu mhariri kukataa wito wa baraza la habari inatokana na jeuri ya aliokuwa anawatumikia ambao saasa ndio wenye nchi!

HAKUNA HAJA YA KUBISHANA NA WEWE, LAKINI HUO NDIO UKWELI, hebu jaribu kufatilia hizo sehemu nilizobandika hapo ili ujilizishe,
 
FTS amenifurahisha kutogombea chochote kwa sasa. Nadhani hii ni sahihi kwa sasa. Aendelee tu kula pensheni yake ya Uwaziri Mkuu ambayo ni kubwa sana kwa sheria ya sasa ya mafao ya viongozi wastaafu wa kitaifa. Mbali na utiifu usiokifani kwa Mkapa hana alilofanya la kukumbukwa na WATANZANIA.
 
15/3/2010

Sumaye aikana CCJ, atoboa siri ununuzi wa rada na ndege ya Rais

Sadick Mtulya na Ramadhan Semtawa

WAZIRI mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema: "mimi si CCJ (Chama cha Jamii); siijui na wala sihusiki nayo."

Sumaye alisema hayo baada ya kutakiwa kutoa msimamo wake kuhusu chama hicho ambacho kimekuwa kikihusishwa na makada wa CCM ambao wanapingana na mwenendo wa chama hicho tawala kwa sasa na ambao wanadaiwa kusubiri wakati muafaka wajitangaze rasmi.

"Mimi si CCJ, siijui na wala sihusiki nayo,"alisema Sumaye: “Duniani kote wanachama wa chama kilicho madarakani hawampingi rais aliyeko madarakani na ukifanya hivyo unajimaliza kisiasa na mwaka huu sitogombea nafasi yoyote hata ile ya udiwani."

CCJ imekuwa ikikanusha kuhusishwa na vigogo wa CCM, lakini haijaweza kutuliza habari zinazokihusisha chama hicho na makada wa chama hicho tawala.

Tayari vigogo kadhaa wameshakanusha habari za kuhusishwa kwao na CCJ, akiwemo Spika Samuel Sitta, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, mawaziri wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na John Malecela.

Kwa sasa CCJ ina usajili wa muda ilioupata Machi 2 na inahaha kusaka angalau wanachama 2,000 kutoka Bara na Visiwani katika kipindi cha miezi sita ili kiweze kupata usajili kamili. Lakini katika muda mfupi, chama hicho kimeshatangaza kuwa kimevuna wanachama 7,700 katika mikoa 11.

Sumaye hakutaka kuzumzia zaidi kuhusu chama hicho ambacho kilitamba kwenye habari kubwa za magazeti mara kabla na baada ya kutangaza rasmi kuanzishwa kwake.

Katika hafkla ya kukabidhi hundi ya Sh5 milioni kwa Jukwaa la Wahariri, Sumaye alizungumzia mambo kadhaa likiwemo suala la mgombea binafsi ambalo linaonekana kupingwa na serikali baada ya Mahakama Kuu kubatilisha sheria inayozuia mgombea wa aina hiyo.

Akizungumzia suala hilo, Sumaye alisema kuwa haoni sababu ya kuzuiwa kwa wagombea binafsi katika uchaguzi.

"Kwa kuwa suala la mgombea binafsi lipo kikatiba, hivyo halina tatizo lolote. Na uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mzuri," alisema Sumaye.

Alisema kinachotakiwa kwa sasa katika suala la mgombea binafsi ni kuwepo kwa sheria ambayo itatumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Kuhusu mpango wa kuwepo kwa sheria ya kutenganisha siasa na biashara pamoja na muswada wa sheria ya udhibiti fedha katika uchaguzi uliopitishwa hivi karibuni na Bunge, Sumaye alisema kwamba nia ya uanzishwaji wa sheria hizo ni njema lakini tatizo litakuwa ni katika utekelezaji wake.

"Nia ya kutaka kuwepo sheria itakayotenganisha siasa na biashara pamoja na kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi ni nzuri, lakini utekelezaji wake utakuwa ni mgumu kulingana na mazingira yalivyo," alisema Sumaye.

Katika utenganishwaji wa siasa na biashara, Sumaye, ambaye aliwahi kushauri wafanyabiashara wajiunge na CCM kama wanataka mafanikio, alisema utekelezaji wa suala hilo utafanikiwa endapo maadili ya Azimio la Arusha yatarudishwa.

'Labda tu maadili ya Azimio la Arusha yarudi ndio tutaweza kutenganisha siasa na biashara," alisema Sumaye.

Akizungumzia makundi ndani ya CCM, Sumaye alisema hali ya kuhitilafiana na kupishana kimtazamo ni lazima iwepo katika masuala ya kisiasa na kwamba matatizo hayo yatakwisha.

"Haya matatizo ya makundi pamoja na mambo mengine ndani ya CCM hayaninyimi usingizi na kwa kuwa CCM ni bingwa wa kutatua matatizo yake, haya yote yatakwisha na tutaingia katika uchaguzi tukiwa pamoja,"alisema. Kuhusu tuhuma zinazomkabili rais mstaafu Benjamini Mkapa, Sumaye alikataa kusema lolote kwa madai kuwa limekwishatolewa maelezo na Rais Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 
Kama kuna mtu ana simu yake naomba mnipatie ili nimuulize maswali ambayo hakuulizwa juzi.
 
Viongozi wakishatoka madarakani ndio wanajifanya wanafahamu matatizo ya WTZ, aibu, walipokuwa kwenye madaraka kwa nini hawakutekeleza yale ya manufaa kwa jamii? Kumbuka Mzee rukhsa hata baada ya kupewa fagio la chuma ambalo aliliuza pale magogoni sijui ataweza vipi kushughulikia mambo ya Chama Cha Majambazi.
 
SIKU moja baada ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kuibuka na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa, kauli zake zimeonekana kukitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Moja ya kauli ya Sumaye ambayo inaonekana kuitikisa CCM, ni suala la kuwepo mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati, alisema suala la kuwepo na mgombea binafsi kwa wakati huu bado ni tete kwa kuwa liko mahakamani.
“Nimemsikia amezungumzia mambo mbalimbali ya kitaifa yakiwemo ya chama chetu, lakini hoja ya kuwepo na mgombea binafsi bado kwa vile suala lenyewe liko mahakamani…Pili nasema huo ni msimamo wake wala si wa CCM kwa vile hatukumtuma kuzungumza… ana haki ya kufanya hivyo,” alisema Kapteni Chiligati.
Alisema msimamo wa CCM uko pale pale hadi mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho, na si kutumia shinikizo la watu wachache.
“CCM siku zote haifanyi mambo kwa kukurupuka, suala la mgombea binafsi liko mahakamani, sisi hatuwezi kuhukumu kabla ya mahakama… tunasubiri sheria ifanye kazi yake na hapo ndipo tutapata majibu,” alisema Chiligati.
Alisema Sumaye akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, ana haki ya kutoa mawazo yake kwa vile katiba ya nchi inamruhusu kufanya hivyo.
“Unajua ndani ya chama kila mwanachama mmoja mmoja ana haki ya kuzungumzia suala lolote ambalo anaona haliendi sawa, hayo ametoa mawazo yake tu.
“Tukiwa kama taasisi hatuwezi kukubali kirahisi tu, tusubiri mamlaka zinazohusika zitatupatia majibu kuhusiana na masuala haya,” alisema Kapteni Chiligati.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema hapingani na uamuzi wa Sumaye kujitokeza na kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa, ingawa kuna mambo ambayo yanastahili kushughulikiwa.
Alisema kazi ya kwanza ambayo Sumaye anapaswa kuifanya ndani ya chama chake ni kubadili mfumo wa utawala uliopo ambao unaonekana kukandamiza Watanzania wengi.
“Tukubali tusikubali mfumo wetu wa uongozi unatukandamiza sana, tunapaswa kukaa kitako ili tuifanyie marekebisho katiba yetu ambayo inaonekana kuwa kichaka cha ufisadi.
“Tunamuomba Sumaye haya anayoyasema ayasisitize ndani ya CCM ili waone hali halisi iliyopo… tangu kuuawa kwa Azimio la Arusha na lile la Zanzibar hali ya mambo imekuwa ikibalidilika mno,” alisema Mbatia.
Juzi, Sumaye alikutana na Jukwaa la Wahariri na kuzungumzia mambo mbalimbali ambapo alisema moja ya mambo anayoona yanafaa ni kuwepo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mbali ya hilo, alizungumzia pia madai ya kuwapo kwa tuhuma za rushwa katika zabuni za ununuzi wa rada na ndege ya rais, ambapo alisema iwapo kuna watu waliojihusisha na vitendo vya rushwa, wanapaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kukabiliana na tuhuma zinazowakabili.
Hata hivyo alisema pamoja na kuwapo kwa tuhuma za rushwa, uamuzi wa serikali wa kununua rada kwa ajili ya kuongozea ndege na ule wa kuagiza ndege ya rais kuwa ulikuwa ni wa lazima na muhimu na kwamba mambo hayo hayapaswi kuchanganywa. “Hapa napenda kuliweka hili sawasawa, nilishalisema na nalisema tena kwamba uamuzi wa kununua rada na ndege ya rais ulikuwa ni wa lazima…Hata hivyo kama kuna watu waliingiza mikono yao na kupata rushwa hilo ni suala jingine, wanapaswa kushughulikiwa,” alisema.
 
Back
Top Bottom