Sumaye azungumza na waandishi; ajibu maswali masuala ya kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye azungumza na waandishi; ajibu maswali masuala ya kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 14, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri Mkuu aliyekaa kwa muda mrefu zaidi katika nafasi hiyo nchini Bw. Fredrick Sumaye anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari saa nne asubuhi hapo Protea Courtyard Hoteli jijini Dar-es-Salaam. Bw. Sumaye alikuwa ni Waziri Mkuu katika kipindi chote cha utawala wa Rais Benjamin Mkapa na baada ya kuondoka madarakani alienda masomoni huko Marekani huku akiahidi kutotaka kuingia tena kwenye siasa. Hadi hivi sasa haijulikani Bw. Sumaye anataka kuzungumzia nini na hasa kama mkutano wake unahusiana kwa namna yoyote na joto la Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwakani au mgongano wa kifikra unaoonekana kukua ndani ya Chama cha Mapinduzi.

  TAARIFA YAKE HII:

  MKUTANO WA MHE. FREDERICK T. SUMAYE NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTELI YA COURTYARD, DAR ES SALAAM.

  14 MARCH, 2010

  ANGALIZO


  1. Mwaka huu wa 2010 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu katika nchi yetu. Na kawaida kipindi hiki mambo mengi yanahusishwa na uchaguzi unaokuja. Kwa sababu hiyo basi nawaomba ndugu zangu niwahakikishie ya kuwa, mkutano huu wa leo hauna uhusiano wowote na uchaguzi mkuu, kwa sababu zilizo wazi kwamba mimi binafsi sitarajii kugombea nafasi yoyote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaika huu.

  2. Leo nina agenda maalum tu, hivyo sitarajii kupokea maswali wala
  mjadala wenye mwelekeo wa kiasa hasa unaoelekeza kwenye Uchaguzi Mkuu, kwa sababu zilizo wazi na ambazo ninyi wenzangu ni wataalamu zaidi yangu.


  KUSUDIO LA MKUTANO

  Kusudio kuu la kuwaiteni hapa ni kukumbushana wajibu wetu kwa lengo la kuelewana katika wajibu na haki zetu.

  Vyombo vyenu vya habari vina majukumu mengi na ya muhimu sana katika jamii.

  Majukumu haya ni pamoja na kuelimisha umma juu ya mambo yanayotokea nchini na penginepo; kutoa taarifa na habari mbalimbali kwa jamii kuhusu mambo yanayotendeka yahusuyo au yenye athari kwa jamii husika; kuburudisha, na mengine mengi ya kijamii na kimaendeleo.

  Ninatambua kwa dhati ya kuwa kila chombo cha habari kina sera yake (media policy), na malengo yake katika jamii. Na hili ni jambo jema kabisa, lazima kila mtu awe na malengo na mwelekeo wake katika alifanyalo au alitakalo na ni vyema akawa na mwongozo wa kazi zake za kila siku.


  Katika kutekeleza wajibu na kufanya kazi zake, chombo cha habari kinaweza kikamwumiza mtu au kundi fulani la watu katika jamii kwa taarifa au habari waliyoiandika katika taarifa zao. Maumivu hayo yanaweza kutokana na taarifa kuwa ya kweli au ya uwongo.

  Pale taarifa inapokuwa ya uwongo, maumivu yake ni makali na mabaya zaidi, na huweza kumvunjia mtu heshima na kumshushia hadhi yake katika jamii kuanzia katika familia yake mpaka jamii nzima inayomzunguka. Aidha huweza kumchonganisha na kumjengea maadui katika jamii, serikali au kundi lolote alilohasimiwa nalo. Hivyo ni wajibu wa kila mwandishi kuwa makini na athari zinazoweza kutokea kutokana na habari anayoiandika. Kama mnavyojua, kalamu ina nguvu kubwa sana, kwahiyo ni budi kuitumia kwa uangalifu mkubwa pia.

  Hata hivyo, kwa kuwa habari ina pande mbili, wakati mwingine hutokea upande mmojwapo kuumia. Itokeapo hali hiyo, mhusika hana budi kutafuta namna ya kusafishiwa jina lake na ukweli uelezwe kwa jamii husika ili sura hasi (negative) au uchafu uliojengeka juu yake urekebishwe na kwa kadri iwezekanavyo ufutike. Ziko njia mbalimbali na hatua mbalimbali za kufikia hatima hiyo.

  Mimi binafsi sina ugomvi kabisa na vyombo vya habari na ndio maana leo hii tuko pamoja kubadilishana mawazo, na ninavipongeza sana kwa kazi nzuri zinazofanywa na wanahabari wengi wenye kuheshimu maadili, ukiacha wachache waochafua jina zuri la vyombo vyetu vya habari.

  Mimi ni mmoja kati ya watu wanaopenda vyombo vyetu vya habari vifanye kazi yao kwa “uhuru na haki” ili umma ufahamu yanayotendeka nchini au penginepo bila kumharibia mtu heshima yake kwa kuandika habari za uongo kwa makusudi au kwa upungufu wa utafiti wa ukweli juu ya jambo lenyewe.

  Hakuna mmoja wetu anayependa kesi, na mimi binfasi sipendi kesi kwa sababu inapoteza muda ambao ungetumika kwa mambo yenye manufaa zaidi, na kesi huwa zina gharama kubwa. Aidha, kesi huzalisha maadui kuliko marafiki.


  YALIYONITOKEA

  Ukiwa kiongozi wa kisiasa unamulikwa saa zote, na jamii pia inakuangalia kwa makini sana. Jambo lolote likisemwa au kuandikwa juu yako kuna makundi mbalimbali ambayo kila moja inaweza kujenga tafsiri yake kwa jinsi itakavyoona inafaa.

  Nitoe mifano michache tu inayonihusu:-

  Ø Mwezi March/April, 2006, gazeti la “Tanzania Leo” liliniandika kuwa
  “Sumaye aonja shubiri ya ari na kazi mpya”, na kuwa akaunti zangu zilizoko nchini Uswisi zenye thamani ya shilingi trilioni kumi zimekamatwa. Hii ni habari nzito sana ya uzushi maana mimi sikuwa na akaunti yoyote nje ya nchi.

  Ikabidi nilishitaki gazeti hilo na wote wanaohusika na nikashinda kesi
  Mahakamani na kuamriwa kufidiwa.

  Ø Kumekuwepo na habari zingine nyingi ambazo si nzuri japo zina athari za uchonganishi ambazo nimeziacha bila kushtaki kwa sababu athari zake nahisi si kubwa. Mfano “Sumaye achochea wabunge kuibua hoja”, “Sumaye yuko Uingereza kufanya kampeni za CCM”, n.k.

  Ø Lakini, kuna gazeti moja la ChangaMoto la Julai 29 – Agosti 4, 2008
  liliandika “Sumaye, Kigoda na kashfa mpya.” Kashfa hiyo inasema sisi [mimi na Dr. Kigoda] tumepora shamba la Mamlaka ya Chai la Mlangali huko Lupembe lenye hekta 200 bila kulipia malipo yoyote serikalini. Hii ni kashfa kubwa na inavunja kabisa heshima ya mtu.

  Leo nimewaita kwa mambo mawili moja ni juu ya kashfa hii ya shamba la Mlangali na la pili nitalielezea baadaye.

  Kwangu mimi hii kashfa ni nzito inayonichafulia jina na kunishushia hadhi yangu katika jamii. Lengo langu si kuzungumzia kama hii kashfa ni ya kweli au ni ya uwongo. Hiyo itazungumziwa mahali pengine wasaa wake utakapofika.

  Lengo langu ni kuonyesa juhudinilizozichukua ili jambo hili lipate ufumbuzi mapema na ili kama habari hiyo siyo ya kweli, jina langu lisafishike.

  Nataka nirudie kuwa sina ugomvi wala uhasama na vyombo vya habari, wala wanahabari wenyewe, na wala sina lengo la kutafuta fedha kwa kushitaki magazeti au vyombo vya habari. Ndio maana leo nimewaita hapa ili tukumbushane mambo machache.

  Na hili linadhihirishwa na hatua nilizochukua dhidi ya Gazeti la *ChangaMoto *kunihusisha na shamba la Mlangali:

  · Niliwaona Wanasheria wangu kutoa malalamiko yangu juu ya kashfa
  hiyo, na kushauriana nao kuhusu hatua muafaka za kuchukua.

  · Tarehe 29 Oktoba, 2008, Wanasheria wangu waliwaandikia barua
  wahusika wote wa ChangaMoto yaani Mwandishi wa habari hizo, Mhariri Mkuu wa gazeti, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni inayolimiliki, na Wachapishaji wake juu ya taarifa hiyo kuwa ni ya uwongo.

  Wanasheria wangu, pamoja na mambo mengine, waliwataka wathibitishe taarifa hiyo, na kama siyo ya kweli, basi waifute katika gazeti lao. Pia, waliwataka waniombe radhi kwa maandishi, wanilipe kwa maumizu niliyoyapata na walipe gharama zote walizosababisha. Barua zote zilipokelewa na hakuna hata mmoja aliyejibu kwa wahusika wote hao.

  · Baada ya kusubiri kwa muda wa miezi mitatu na barua kutokujibiwa,
  tarehe 25 Februari, 2009, Wanasheria wangu walimwandikia Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kulalamika juu ya habari hiyo iliyoandikwa katika gazeti la ChangaMoto na juu ya wahusika kutokujibu lolote baada ya kuandkiwa barua. Wahusika walipewa nakala za barua hii na ofisi yao ilikiri kuzipokea, ila hakuna aliyejibu.

  · Tarehe 13 Machi, 2009, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari aliwaandikia wanasheria wangu kuwa wahusika wameandikiwa barua ili watoe maelezo.

  · Tarehe 6 April 2009, Katibu Mtendaji alimwandikia Mhariri Mkuu wa
  ChangaMoto kumkumbushia kuwa bado wanasubiri maelezo kuhusu kashfa iliyoandikwa katika gazeti lao ambazo nimezilalamikia.

  · Tarehe 30 April, 2009, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania alimwandikia tena Mhariri Mkuu kuwa kwa vile huonyeshi ushirikiano
  wowote juu ya jambo hili ili shauri hili limalizwe vizuri, sasa shauri hili
  linapelekwa kusikilizwa katika Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari
  Tanzania.

  · Tarehe 8 Juni, 2009 ofisi ya Wanasheria wangu ilimwandikia Katibu
  Mtendaji wa Baraza kuhimiza kuwa jambo hili lipangiwe tarehe ya kusikilizwa katika Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania haraka iwezekanavyo.

  · Tarehe 10 Juni, 2009, nikaandikiwa barua na Katibu Mtendaji wa
  Baraza la Habari Tanzania kuwa shauri limepangwa kusikilizwa tarehe16 Juni 2009, na kuwa niwepo mimi binafsi. Nikafuta safari zangu ambazo nilikuwa nimezipanga kabla. Hata hivyo shauri halikufanyika kwa sababu Mhariri alitoa udhuru kuwa atakuwa safarini Arusha.

  · Tarehe 8 Julai, 2009 Katibu wa Baraza alimwandikia Mhariri Mtendaji Mkuu aeleze muda ambao atakuwepo ili shauri hilo lipagwe kusikilizwa.

  · Baada ya kutopata majibu yopyote kutoka kwa wahusika wa gazeti la
  Changamoto, tarehe 23 Julai, 2009, Katibu Mtendaji wa Baraza alimwandikia Mhariri Mtendaji wa ChangaMoto kwa kutokuridhishwa na ushirikiano wake, akisema:

  *“Kwa kuwa hujaonyesha nia ya kutaka shauri hili litatuliwe kwa njia ya
  usuluhishi kiungwana na kwa maafikiano, Baraza linapenda kukuarifu kuwa limemuandikia barua mlalamikaji Mhe. Sumaye likimshauri kuchukua hatua nyingine atakazoona zinafaa kuweza kutatua shauri hili, ikiwa ni pamoja na kulifikisha mahakamani kama ataamua hivyo”. *

  * *

  Pamoja na barua hiyo iliyopelekwa ChangaMoto, Katibu huyo wa Baraza aliniandikia barua siku hiyo hiyo akinieleza hivyo.

  Nimeeleza haya yote siyo ili nipate huruma fulani bali muone jitihada
  tunazozifanya ili mambo kama haya yaishe kwa njia ya usuluhishi zaidi badala ya kutumia njia za Mahakama ambazo, kama nilivyosema awali, ni za gharama kubwa. Lakini juhudi hizo zikigonga ukuta, na pale inapobidi tutafanya hivyo ili kulinda heshima, utu na hadhi ya mhusika katika jamii. Kwahiyo nia yangu ya kwanza ni kuwaeleza kuwa ninakusudia kufanya kama ambavyo nimeshauriwa na Katibu wa Baraza la Habari Tanzania na kulifikisha gazeti la ChangaMoto mahakamani.


  JUKWAA LA WAHARIRI

  Sababu ya pili ya kuwaita ni kutimiza ahadi yangu niliyoitoa mwezi Mei, 2008 wakati wa kutoa maelezo kwa waandishi wa habari yaliyotolewa na mmliki wa gazeti la Tanzania Leo. Nilisema kuna tatizo kubwa la kutokuzingatiwa kwa maadili ya uandishi wa habari. Tatizo hilo hata leo tunaliona likiendelea.

  Hivyo ninataka kutimiza ahadi yangu kwa Jukwaa la Wahariri na kutoa Shilingi Milioni Tano ili zichangie katika harakati zao mbalimbali hasa zile zinzohusu kukumbushana maadili, wajibu na haki ya uandishi wa habari, na waandishi wenyewe.

  Naamini Watanzania wenzangu wataniunga mkono badala ya kutumia uwezo na nafasi zao kuchafua maadili ya waandishi na vyombo vya habari kwa maslahi yao binafsi.


  Asanteni sana kwa kunisikiliza.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Anataka na yeye kwenda magogoni huyu i guess.
   
 3. D

  Donrich Senior Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  I guesss,atazungumzia hali ya siasa na muelekeo wa nchi kuelekea october 2010,zidhani kama atatangaza tena kugombea uraisi...
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Atashangaaa muache aropoke apotezwe!!
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  That is my 2nd guess. My 1st is that Mkulu JK kawaomba Sumaye na Mkapa wampigie debe.

  Ebu tusubiri tuone na tusikie kitakojiri
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu inaweza isiwe guess

  maana ilipopitishwa sheria kuwa raisi lazima awe na KA-NYUZI (degree), jamaa akakimbia Marekani fasta, sijuhi kununua au alikaa kitako, lakini mwisho wa siku alirudi nayo na yupo tayari kwa mapambano ya kwenda Magogoni
   
 7. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Atangaze? Kwani hamwogopi Hussein? Au atapitia CCJ?
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,589
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Naamini atatagaza nia ya kugombea uraisi, Nakumbuka enzi zake Mtikila alimkomalia sana.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yupo namsikiliza hapa.. naona amewajia juu gazeti la Changamoto kwa kuandika juu ya kile ambacho gazeti hilo linadaiwa kuandika habari kuwa Sumaye alikuwa amepora shamba akiwa madarakani. Baada ya sekunde chache nitaweka statement yake kwenye posti ya kwanza.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hii sheria ya kumtaka raisi awe na shahada ni sheria ya nchi (imo kwenye katiba) au ni utaratibu wa CCM tu?
   
 11. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  kwa sasa kutangaza sio raisi sana kwa sababu mwelekeo wa Mkulu bado haujajulikana na Mkwara wa UWT (Usalama wa Taifa), kupitia Sheikh Yahaya kwamba Damu lazima imwagike mtu akimpinga JK katika njia ya Magogoni,

  kwa hiyo atakuwa na kauoga fulani, lakini nadhani 2015 lazima atajitosa
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ameleta mchango wake kwa jukwaa la wahariri wa shilingi ya milioni 5. Anasema anatimiza ahadi yake aliyoitoa kwa jukwaa la wahariri..
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  What new can Sumaye bring in Tanzania? Anapapatika tu kama kuku.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ameleta mchango wake kwa jukwaa la wahariri wa shilingi ya milioni 5. Anasema anatimiza ahadi yake aliyoitoa kwa jukwaa la wahariri.. anajiandaa kupokea maswali sasa hivi:

  Wanamuomba kuzungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa zaidi ya hayo ya mambo ya magazeti.. anawaambia atajiepusha na maswali wanayotaka kumuuliza. Hawa waandishi sijui vipi badala ya kuuliza maswali wanamuomba kibali kama atakuwa tayari kuulizwa maswali..

  Kawaambia kuwa akiona swali hataki kulijibu ataliacha: (yaani wanamuuliza maswali kwa ujumla halafu atayajibu kwa mpigo)

  swali: Wanamtaka atangaze mali zake hadharani hasa kwa watu wanaodhania kuwa yeye ni bilionea:

  swali: wanamuuliza kuhusu pia suala la sheria mpya ya gharama za uchaguzi
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Majibu yake:

  Amekataa kutangaza mali zake kwani yeye ni mtu wa kawaida sasa.

  kuhusu wafanyabiashara na siasa inaonekana anakubaliana na Kikwete. Maoni yake hata hivyo anasema wazo ni zuri lakini utekelezaji ni mgumu. Anasema wataweka mipaka wapi, anasema labda kama maadili ya Azimio la Arusha yatarudishwa kama kweli wanataka kufanya hilo. Anahoji mpaka utakuwa wapi? anayefuga kuku 1000 au mwenye dalala 2 asiruhusiwe kushiriki siasa?


  Anakubaliana na suala la sheria mpya in principle, lakini anasema kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wake.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  amekataa kuhusishwa na CCJ

  Kwenye suala la mgombea binafsi anakubali kuwa suala hili halina tatizo na analiunga mkono kwani Katiba inaruhusu. Anaunga mkono suala la mgombea binafsi. Sasa kama muda wa kubadili Katiba upo anasema yeye hajui kwani hayuko serikalini.

  Anasema uchaguzi wa mwaka huu "utakuwa mzuri sana"..
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Anazungumzia suala la ununuzi wa rada. Anautetea uamuzi wa kununua rada lakini anasema kuwa kama kuna wizi au rushwa ni lazima lifuatiliwe na wahusika waadhibiwe..

  Anaulizwa kama ana akaunti nje ya nchi lakini anawauliza kama ina faida gani.Anasema alipokuwa madarakani hakuwa na akaunti nje ya nchi hadi alipoenda kusoma madarakani.

  Suala la Tarime anasema kuna tatizo na ni lazima litatuliwe. anasema matatizo ya Tarime tangu enzi ya mwalimu lakini sasa hivi mzizi umekuwa mkubwa. Anaamini serikaili itatafuta namna ya kushughulikia. Suala la Hanang anaona nako kuna tatizo katika handling.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Mar 14, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na haja kweli ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari au ?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  anaendelea..
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mi nafikiri anaanza PR mapema tumzoee kwene vyombo vya habari na pia kujenga ka-uhusiano na wanahabari. Kabla ya Oktoba tutashuhudia mengi.
   
Loading...