Wachangiaji wengi humu naona hawasomi contents, isipokuwa wanajibu kwa kusoma headline tu.
Kwenye tangazo lake alitangaza mambo ambayo atayazungumzia, badala ya kuzungumzia hayo watu wanaanza kuguess, wakati ashasema atakachozungumza.
Ameanza kuchangia million tano, wengine muungeni mkono katika kuliwezesha jukwaa la wahariri au kitu kingine kitakachofanya waandishi wetu waive katika fani yao.
Atashangaaa muache aropoke apotezwe!!
Hivi alikuwa wapi siku zote hizo kuzungumza haya?why now?
Ni kwamba pamoja na kwamba mtandao ulimtumia magezeti kumchafua kwa ukweli na uwongo, JK kamuomba amuunge mkono na kumpigia debe. labda na yeye atapigiwa debe 2015.
Ndiyo sababu kaja muda huu.
kwa sasa kutangaza sio raisi sana kwa sababu mwelekeo wa Mkulu bado haujajulikana na Mkwara wa UWT (Usalama wa Taifa), kupitia Sheikh Yahaya kwamba Damu lazima imwagike mtu akimpinga JK katika njia ya Magogoni,
kwa hiyo atakuwa na kauoga fulani, lakini nadhani 2015 lazima atajitosa
Haya yanayotokea leo ya watu kuchafuana ni matokeo ya wao wenyewe kutumia vyombo vya habari kujijenga kisiasa kwa kuchafua wenzao. Waandishi wengi wa habari wapo tayari kufanya lolote la kishetani endapo fedha itatangulizwa. Wote tunakumbuka kuelekea uchaguzi wa 2005 watu walivyokuwa wananunua vyombo vya habari kuwachafua wenzao.
Huyu Sumaye alikuwa wapi katika miaka yake mingi ya uwaziri mkuu kukemea na kusisitiza maadili katika vyombo vya habari? !!