Abu Ubaidah Commando
JF-Expert Member
- Sep 8, 2016
- 7,590
- 6,956
Tanzania inawabania mno,,misaada mingi inayotoka nje haiwafikii wazanzibar.
Mkuu fikilia tena kidogoNew city,,,yupo sahihi Mkuu. Znz Itakuja geuka kuwa half london.
Kweli kabisa mkuu....Mbona povu babaaa!?? Utakufa ujue.
By the way kuna mawaziri humo ni wazenji.
Na siku Zanzibar ikiruhusiwa kujitegemea ndani ya miaka mitano hata vumbi lao hatutoliona.
Mkuu fikilia tena kidogo
We are planted this issue in our mind so it's Ok but I am not seeing any changes through ArabiaNifikilie mara ngapi Mkuu. Oman ni wa2 wa aina yake katika huu ulimwengu 2naoishi na ni wa2 wema na wakarimu mno kuliko nchi yoyote babaa,,,,na kama itajitenga basi tutarajie new ZNZ kwa msaada wa Oman,,,,na uchumi wao utainuka. Tatizo nchi yetu inawabania.
Kilikuja na meli kwakweli...We are planted this issue in our mind so it's Ok but I am not seeing any changes through Arabia
Miaka 50 ilopita Tanzania na Oman zote zilikua nchi Masikini.....Yaani Oman wanaweza kufanya Zanzibar vumbi lake lipotee? Mimi napafahamu vema Oman mbona vumbi lao bado wana safari ndefu sana ya kulipoteza? Au watatoa kipaumbele Kwa Vumbi la Zanzibar?
Mkuu, issue siyo negative thinking! hell No! issue ni akili mgando za baadhi ya watu wanaotaka kutuaminisha kuwa ujumbe kutoka Oman umeleta baraka Tanzania na Commander in chief anaamini hivyo. kweli nchi imejaa wajinga. hivi ni wapi nchi ya Oman imewekeza kwenye Gas nje ya mipaka yake. Remember, mafuta yanayochimbwa Oman ni technology ya Mzungu na si vinginevyo!
Hata hizo Nchi za magharibi wenye Technology wanategemea sana watu wenye Fedha, wao hio Technology yao hawatoi bure . Ukiwa na Fedha mtu yoyote na Pahala popote duniani ataekeza,hakuna cha kujivunia hapo. Oman licha ya kwamba ina mafuta siyo tajiri kivile na hata wao wanategemea western countries in term of technology. sasa huo uwekezaji kwenye gas utawezekanaje? nachoona ni kwamba wamekuja kama watalii kwa ticket ya kidiplomasia na si vinginevyo. harafu Rais naye anasema eti sisi ni ndugu, kweli? WTF...Hakuna undugu wowote wa mwarabu na mswahili...and that's the bottom line! inakera na inaudhi..
Prof labda ungeisoma tena historia ya Oman na Zanzibar halafu ndiyo ungetoa maoni yako, naomba pitia katika hii link ili upate kujua japo kidogo uhusiano wa kirafiki au uliyochanganya damu? History of the Oman and Zanzibar SultanateMkuu, hao ni waarabu/Arabs na sisi ni waafrika/blacks. Ratio ya kuwa ndugu ni (1/billion). bora Rais angesema kuwa ni Rafiki zetu due to long history and diplomatic ties kati yetu na wao. mkuu, i have nothing against whoever..ila ni ajabu kuwachukulia Oman kama big deal kwetu na kuona tumepata wakombozi/wawekezaji kama mkuu wenu wa nchi alivyokuwa anajitapa. sometimes nashindwa kuelewa akili ya waafrika wenzangu...
Hata kama sio uchumi mkubwa ,bado hutoweza kuilinganisha na huku bara.Hizo no ndoto za mchana mchana zenji hata ikijitenga haitaweza kuwa na uchumi Mkubwa Kama unavyofikilia wewe
We are planted this issue in our mind so it's Ok but I am not seeing any changes through Arabia
Qaboos bin Said Al Said alizaliwa tarehe 18 Novemba mwaka 1940 katika mji wa Salala ulio kusini mwa Oman.Ndiye mtoto pekee wa Sultan Said bin Taimur.Mama yake ni malkia Mazoon al-Mashani.
Elimu ya msingi aliipata mjini Salala na baadae Pune nchini India.Alipofika miaka 16 alipelekwa kwa masomo ya juu nchini Uiengereza.Alipofika miaka 20 aliingia kwenye kikosi cha kijeshi cha kifalme kinachoitwa sandhurst. Baada ya kufaulu mafunzo katika chuo hicho alijiunga na jeshi la kiiengereza na kupangiwa shughuli za kijeshi kwenye bataliani ya 1 nchini Ujerumani ambako alikaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na hata kushika nafasi za unadhimu kwenye jeshi hilo la kiiengereza.
Sultan Qaboos baadae aliacha shughuli za kijeshi na  akaanza kuchukua mafunzo ya namna ya kuendesha serikali za kiraia.Baada ya hapo alifanya ziara ndefu ya kuizunguka dunia kabla kurudi nyumbani kwao  Salalah.Alipofika Salala aliisoma dini yake ya kiislamu na historia ya nchi yake ya Oman.
Mwaka 1976 mfalme Qaboos alimuoa bint Ami yake, bi Kamila,nee sayyida Nawwal bint Tariq.Hata hivyo ndoa hiyo haikudumu na tangu aachane na mkewe huyo hajaoa tena na wala hana mtoto.
Mnamo mwezi Julai mwaka 1970 kikosi cha jeshi kilichomuunga mkono Qaboos kilipambana na kikosi cha jeshi cha mfame Said bin Taimur  na kufanikiwa kumpindua baba yake huyo.Serikali ya Uiengereza ilisaidia kuimarisha utawala wa mfalme Qaboos baada ya mapinduzi hayo.
Tangu mfalme Qaboos atawale Oman amefanikiwa kubadili hali za kiuchumi za raia wake na kuleta maendeleo makubwa nchini humo.
Ukoo wa mfalme Qaboos wa Abusaidy ndio uliokuwa na mahusiano makubwa na ukanda wote wa pwani ya mashariki ya Afrika na hata kuwa na utawala wa pamoja ambapo ulijenga makao makuu ya utawala wake nchini Zanzibar ambayo sasa ni nchi ndugu waTanganyika ambazo kwa pamoja zinaunda jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa zaidi ya karne moja raia wa ufalme huo waliweza kupenya kibiashara na kusambaa kote mashariki na kati ya Afrika.
Kutokana na ukweli huo wa kihistoria na mafungamano kati ya Oman na Tanzania zipo kila sababu kwa mfalme Qaboos bin Said kuja kutembelea Tanzania akianzia Zanzibar.
Kutokana na mapenzi makubwa ya wengi wetu kwake siku atakapofika tutajitokeza kwa wingi kwenye mitaa ya Shangani mjini Zanzibar au Kariakoo jijini Dar es salaam kujipanga barabarani kumpokea na kusalimiana nae.
Moja ya maeneo ambayo yanaweza kuwa kivutio na mapumziko ya sultan huyo wa Oman ni mbuga za wanyama za Serengeti,Loliondo na Ngorongoro. Kwa heshima na taadhima na kwa niaba ya wapenzi wa utawala wa Sultanate of Oman nachukua fursa hii kumkaribisha his majesty Sultan Qaboos bin Said aje kuitembelea Tanzania.