Source:
Fanack.com, m.foreignaffairs.com , theeconomist.com
1. Sultan Qaboos hawapi nafasi wananchi wake kuwa na sauti katika siasa. Wananchi wakiandamana kama miaka ya 2011 na 2013, anawakandamiza na kuwatia ndani.
Yeye pekee ndio anachagua wanasiasa na mawaziri kuendesha nchi.
2. Raia wengi waliotoka Zanzibar wanaoishi Oman hawana haki ya uraia wao. Wanaishi na viza kama wageni wengine japokuwa kwa kuwa wana uhusiano wa kidamu, ni rahisi kupata viza za kufanya kazi.
3. Chuo cha Kifalme cha Sandhurst ni Chuo kikuu Waingereza wanatumia kuwapa masomo ya kijeshi kwa "marafiki" zake, kwa manufaa yake.
Bila kusaidiwa na jeshi la Uiingereza, Sultan Qaboos asingeweza kumpindua baba yake mzazi wala kukaa madarakani mpaka leo. Mpaka miaka ya 1990, wanajeshi wa Kiingereza walikuwa kwenye madaraka ya juu katika jeshi lake. Na Mpaka leo wana kambi na vifaa vyao hapo.
4. Oman ni nchi tulivu na imeendelea vizuri. Lakini mafuta yanakwisha muda si mrefu na kizazi kipya kinaomba sauti kubwa zaidi kisiasa. Pia, ajira ni ndogo kwa vijana wao na ufisadi serikali upo japokuwa sio mkubwa kama wa kwetu.
Nategemea wananchi wao watabanwa kisiasa madamu Sultan yupo hai. Uiingereza na Marekani imewekeza sana katika sekta ya Mafuta na haitataka wananchi wa Oman kutaifisha au kuvuruga biashara yao ya mauzo ya vifaa vya kijeshi. Watakuwa tayari kupinga mapinduzi yoyote yatayoharibu biashara zao.
Hatuwezi kuongelea mada ya Sultan Qaboos bila ya kuzungumzia maswala ya siasa za nchi yake. Sio tu upendo wake ambao ni mkubwa na sifa zake za kuoongoza
A pack of Lies lets ask Lukuvi, Makinda and Mbowe who had recently been there!!