Kwenda mahakamani huo ni mtazamo wako.
Yeye ameamua kutumia njia nyingine ya kuwaeleza wadau wa muziki na taifa kwa ujumla kwamba kuna kitu hakiko sawa. Sasa ni juu yetu wananchi kuona ni kwa namna gani tunaweza kusaidiana nae kulimaliza hili tatizo.
Si kila mara unaweza kuiambia kitu serikali ikatekeleza wakati huo huo. Hata EPA ilipotajwa kwa mara ya kwanza serikali iliziba masikio, lakini watu walivyoendelea kukomaa, hatimaye ilisikia.
Na hapa nikukumbushe kuwa watuhumiwa wamekuwa wakimuandalia sherehe ya "birthday" mwenye serikali, kwahiyo unaweza kuona ugumu wa serikali kuchukua hatua kwa haraka, inabidi kelele ziendelee kupigwa hadi isikie, bila kujali ni redioni, JF, Facebook ama twitter!!