SI KWELI PreGE2025 Sugu amelalamikia kutengwa na kamati kuu ya CHADEMA

SI KWELI PreGE2025 Sugu amelalamikia kutengwa na kamati kuu ya CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
kumekuwa na chapisho linalo sambaa kwenye mitandao ya kijamii likionesha ukurasa wa joseph mbilinyi umeweka chapisho la kutokuwa na imani dhidi ya uongozi uliopo madarakani "Nukuu ya chapisho hil o inadai kuwa nimekuwa nikihisi haklli ya kutengwa mara baada ya kuhusishwa kujiunga na chama cha CHAUMA
1749874849286.png
 
Tunachokijua
Joseph Mbilinyi ni mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa lakini pia amewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi tofauti kupitia jimbo la Mbeya Mjini.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo facebook Juni 13, 2025 wamekuwa wakisambaza inayoonekana kuwa ni screenshor kutokea kwenye mtandao wa X ikidaiwa kuwa imechapishwa na Joseph Mbilinyi “Sugu” akidai kuwa anajihisi kutengwa na kamati kuuu ya chama hiko.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa maneno hayo ni ya kughushi na hayajachapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa X wa Sugu.

Aliyetengeneza andiko hilo amefanya kwa lengo la kupotosha umma kwa manufaa yake binafsi aliyo nayo. JamiiCheck ilifanya ufuatiliaji kwa njia ya utafutaji maneno muhimu “Keyword search na kubaini kuwa maneno hayo hayajawahi kuchapishwa katika ukurasa rasmi wa Sugu.

Aidha Sugu kupiti ukurasa wake wa X amekanusha taarifa hiyo ya kuhusu kutengwa na kamati kuu ya chama kwa kuandika kuwa;

“Hakuna wa Kunitenga kwenye kamati kuu ya chama changu… Im a RANKING MEMBER”
Muda ni mwalimu na hakimu wa haki.. Hebu tuupe wakati
 
Huyo siyo mamluki wa G55 kweli?
 
Habari hiyo si kweli nipo sugu hapa tunakunywa 🍻 nimemuonesha kacheka sana
 
Back
Top Bottom