Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani

Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Yaani wewe ndio inabidi tukufundishe sasa kiswahili aisee, kwenye kiswahili lipo neno samani (means furnitures) na neno thamani (means value). Haya ni maneno mawili tofauti kabisa hayashabihiani.
 
CCM wanachakachua hadi samani??
jana tumesikia Masha kang'oa vitasa...
Kweli hii ni aibu ya taifa
MBUNGE wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, ameanza kukumbana na machungu ya uongozi baada ya kukabidhiwa ofisi ambayo haina samani ndani yake.
Ofisi hiyo imebainika kukosa samani zinazotakiwa baada ya mbunge huyo kwenda kwa Mkurugenzi wa Jiji, Juma Rashid Idd, kwa lengo la kukabidhiwa rasmi ili aanze kazi za kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi, majira ya saa 3.30 kati ya Mkurugenzi wa Jiji Idd na mbunge huyo, lakini lilikwama kutokana na mazingira ya uchafu yaliyo mithili ya ofisi iliyotelekezwa na haikuwa na samani ndani yake.

Baadhi ya maofisa wa jiji la Mbeya ambao walishuhudia tukio la kukabidhiana ofisi, waliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa kutokana na kukosekana kwa samani katika ofisi hiyo, Mbunge huyo hakuweza kukabidhiwa hadi hapo zitakaponunuliwa nyingine.

“Ni kweli Mbunge kashindwa kukabidhiwa ofisi hiyo maana hali ya ofisi ni mbaya, ukiangalia kwa haraka utagundua kabisa kuwa jamaa…(akimaanisha mbunge aliyepita Benson Mpesya CCM) hakuwa akiitumia kwa muda mrefu,” alisema mmoja wa maafisa jiji ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Mbali ya kutokuwa na samani, ofisi hiyo pia haikuwa na mafaili yoyote yanayotumika kuhifadhia nyaraka mbalimbali za kiofisi ikiwemo mipango iliyotekelezwa na inayotarajia kutekelezwa na mbunge.

Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, kila mwezi mbunge hupokea sh 500,000 kwa ajili ya shughuli za jimbo, ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ofisi.

Source: Tanzania Daima 01/12/2010

Hivi huu ndo mpango wa CCM au ni utashi mdogo wa viongozi wa siasa?
 
...blah blah nyiiiingi hazitusaidii, tungekuwa tunaanzia hapa kwenye 'accountability' kuwapeleka hao wabunge waliomaliza muda wao polisi kisha mahakamani. Kila senti 'inayofujwa' inatokana na kodi yangu mimi na wewe mwananchi. Tuna kila sababu ya kuhoji matumizi yake. Laki tano kwa mwezi nyingi, ni sawa na 6,000,000/= kwa mwaka, au...30m/= kwa miaka mitano!

Naunga mkono hoja!!!!!!
 
Kaka kweli wewe kihiyo maana nina kila sabaubu ya wasiwasi na uraia wako kisha elimu baadaye kazi yako Samani ni furniture &fixtures, kama meza viti kabati na vitendea kazi vinavyohitajika,

Anyway nimekusamehe bure ama kwa moyo mweupe kabisaaa, Mpesya atakaaje ofisini wakati alihamia Dar na Dom akajenga kilabu kijijini alipotokea kisha akaenda kujenga shule Dom kweli Msafa sijui msafwa awezi kuendelea kama mchaga maana aliona home wanahitaji pombe zaidi
 
Kaza mkanda Mr Sugu ndo ukubwa huo , baadaye utakula matunda ya machungu yako maana matunda yake ndo matamu
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Haya ndio matokeo ya Shule za kata. Kutojua hata kutofautisha SAMANI na THAMANI. Mungu tuhurumie.
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Acha kukurupuka kama mwehu, hili ni jukwaa la wasomi wa kila taaluma, neno samani ni neno fasaha linalomaanisha furnitures kwa lugha ya kiingereza. Rudi shule kama unahitaji kufundisha kiswahili zuzu wewe.
 
Nadhani samani ingekuwa inawekwa na mbunge mwenyewe au chama chake. Hii itaepusha malalamiko kama haya na kuondoa uwezekano wa kuwekeana vitega sauti kwenye hizo samani. Serikali itoe nafasi ambayo ni safi, salama ( madirisha na milango inayofungika) na ina huduma kama maji, umeme basi. Hayo ya ma-filing cabinet na picha za mheshimiwa Rais wanunue wenyewe. Wakiondoka, waondoke na vitu vyao.

Amandla......
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Ndiyo matatizo ya elimu iliyochakachuliwa na MUNGAI. kasome kamusi.
 
Jamani muiteni Mh.Mbilinyi kwa sasa....Sugu ni yule ndugu yetu wa humu....nilistuka kudhania ndiye yeye
 
nani kakuambia kabla ya sugu kulikuweko na mmbunge mbeya mjini? popote walipochukua jimbo chadema hakukuwahi kuwa na mmbunge ndo wamepatikana wabunge sasa hivi kwnye majimbo husika hvo hvo na TZ hatuna RAIS nimpaka SLAA atakapochukua ndo tanzania itakuwa na RAIS.kwa hyo kwanza wajenge offce zao waweke hzo SAMANI sijui wengine wanaita thamani humo humo but habari ndo hyo!!
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Matunda ya shule za kata
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
wewe ndio bomu kabla hujafundisha watu kiswahili jifunze wewe kwanza.

Samani ni furniture na thamani ni value
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
Kama vile maneno Malazi na Maradhi,kidogo kama sawa ila maana tofauti kabisa.
 
Aibu kwa CAG anafanya kazi gani? huu ni ubadhilifu wa wazi wazi, kweli nchi haina mwenyewe
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
Mwalimu pompopo, umeshaeleweshwa vya kutosha maana ya maneno samani na thamani. Naamini hata matumizi ya neno "nawakilisha" siyo kuteleza kwa vidole kwenye keyboard ni kwamba hujui. Neno sahihi ulilopaswa kulitumia hapo ni "kuwasilisha"
 
Sugu aanze kazi bila tatizo lolote kukiwa hamna kitu wananchi wa jiji la Mbeya watamuelewa tuu
 
Hapa kweli wanastahili kushtakiwa. Kinachonichanganya pia ni kuwa kwa hawa wapya wasiokuwa na fenicha, wanasubiri wakurugenzi waweke fenicha ndo wakabidhiwe ofisi, issue hapa ni kuwa, kama wanapokea hela kwa kazi hiyo Je? Watazirudisha kwa Halmashauri husika pesa zilizotumika kununua hizo fenicha?
Hapa tuwekane sawa wana JF, nadhani 500,000/- ni Petty Cash kwa ajili ya ofisi ya mbunge na sio kwa ajili ya fixtures, furnitures, renovations and so on. Hizo major office exps zinachukuliwa na mwenye ofisi na si mtumia ofisi. Ingawa ndugu yetu nyamagana kaamua kung'oa hadi vitasa vya milango. Hapo hamkomoi mbunge mpya ila anaitia hasara serikali ambayo aliwahi kuwa waziri wake.
 
Back
Top Bottom