BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Mayiik Ayii Deng amefutwa kazi kupitia tangazo lilitolewa kupitia Runinga ya Taifa bila kuwepo kwa taarifa zaidi za sababu ya kuondolewa kwake. Waziri huyo ni mtu wa karibu wa Rais Kiir na amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais.
Kiir amechukua uamuzi huo ikiwa ni Wiki moja tangu amfute kazi Waziri wa Ulinzi ambaye ni mke wa Makamu wa Rais wa Kwanza, #RiekMachar, uamuzi ambao umetajwa kutishia makubaliano ya amani baina ya Serikali Kuu na Upinzani unaoongozwa na Machar.
Umoja wa Mataifa (UN) umetoa wito kwa pande zote kuepusha hisia zinazoweza kuhatarisha hali ya ushirikiano uliorudisha amani kati ya Serikali na waasi kutoka upande wa Makamu wa Kwanza wa Rais.
================
South Sudanese President Salva Kiir has sacked his foreign minister, less than a week after dismissing the defence and interior ministers.
No explanation was given for the dismissal of Mayiik Ayii Deng, which was announced in a decree on the state television.
The sacked minister is an ally of Mr Kiir, and previously served as the minister in the president's office.
Last week’s sackings have threatened to derail a peace deal with opposition leader First Vice-President Riek Machar.
The opposition called for the reinstatement of Angelina Teny, who Mr Kiir dismissed as defence minister and handed the position to his party. Mrs Teny is also Mr Machar’s wife.
The UN called for the parties to "exercise restraint and engage in a collegial spirit in order to resolve such sensitive national issues”.
BBC