Suala la Vyeti Feki ni Mbwa kala Mbwa

Kichuya

Member
Jul 9, 2016
55
30
Ukweli ni kwamba hata wenye vyeti halisi utendaji wao hautofautiani na hao wenye vyeti feki, na huenda hata wanawazidi wengine

Nimefanya kazi na wanaojiita wasomi tena wa haja kwa kiwango cha changarawe lakini kwa kweli nimeishia machungu sana mtu ana Masters ya kitu hicho hicho alichosomea lakini inabidi tena ubebe kichwa chake yaani kazi yake ufanye wewe .....................

Nikisema mbwa kala mbwa, nina maana ya kwamba huenda hata huko vyuoni tuseme basi wamefundishwa na waalimu FEKI?

Tusilaumu dobi ilihali kaniki ndio rangi yake

Mh waziri kwanza nikupongeze kwa kuiongoza wizara yenye changamoto nyingi na inayo simamia shughuli nyingi na nyeti kwa taifa letu,hasa ikiwemo idara ya elimu.

Tumeshuhudia matokeo ya mitihani mbalimbali ikiwemo ya darasa la saba wanafunzi wanafanya vibaya na lawama zinaiendea serikali, lkn ukitaka kujua nini chanzo cha wanafunzi kufanya kufanya vibaya utagundua ni walimu wao kutokuwa na sifa za kufundisha.

Sasa tunakuomba utuwekee namba yako maalum hewani ili tukutajie walimu wenye vyeti vya kugushi na ukiwaondoa hao wakabakia wenye sifa tunaamini elimu yetu itapanda ubora wake.
 
Uwe na cheti tu suala la ujuzi ni jambo jingine
Kweli kabisa knowledge na skills ni vitu tofauti ingawa vinaendana nina maana unaweza ukawa na maarifa ya kitu fulani lkn huna ujuzi wa kukifanya mf daktari aliyetoka shule ana knowledge ya oparesheni lkn hawezi kufanya na hatuwezi kumuita feki na nesi mfagizi wa wodi ya wazazi anaweza kuzalisha (skill)lkn hana knowledge!
 
nikitafakari Zaidi nagundua kwamba hawa makenika wa mitaani wanajua sana kuliko hata wahandisi wa vyuo vikuu ima hata wajenzi waliobobea wanajua sana ...................nk
 
Kwah
Ukweli ni kwamba hata wenye vyeti halisi utendaji wao hautofautiani na hao wenye vyeti feki, na huenda hata wanawazidi wengine

nimefanya kazi na wanaojiita wasomi tena wa haja kwa kiwango cha changarawe lakini kwa kweli nimeishia machungu sana mtu ana Masters ya kitu hicho hicho alichosomea lakini inabidi tena ubebe kichwa chake yaani kazi yake ufanye wewe .....................

nikisema mbwa kala mbwa kwa ninmaana ya kwamba huenda hata huko vyuoni tuseme basi wamefundishwa na waalimu FEKI?

tusilaumu dobi ilihali kaniki ndio rangi yake
Kwahiyo unatetea uwepo wa vyeti feki?Kama wewe unacheti feki mmeambiwa mjislaimishe,kiama kinawatembelewa
 
Ukweli ni kwamba hata wenye vyeti halisi utendaji wao hautofautiani na hao wenye vyeti feki, na huenda hata wanawazidi wengine

nimefanya kazi na wanaojiita wasomi tena wa haja kwa kiwango cha changarawe lakini kwa kweli nimeishia machungu sana mtu ana Masters ya kitu hicho hicho alichosomea lakini inabidi tena ubebe kichwa chake yaani kazi yake ufanye wewe .....................

nikisema mbwa kala mbwa kwa ninmaana ya kwamba huenda hata huko vyuoni tuseme basi wamefundishwa na waalimu FEKI?

tusilaumu dobi ilihali kaniki ndio rangi yake
Hizo zote ni porojo. Tunaanzia kwanza na cheti, halafu baada ya hapo tutaangalia utendaji kazi wako. Sidhani kama waweza mpa mtu kazi ya udaktari wa binadamu kama hakusomea; hata awe mchapakazi namna gani humpi ng'o.
 
Ukweli ni kwamba kama huna cheti feki basi angalau kuna somo umefundishwa na mwalimu feki, ndo ilivyo kwa hapa bongo.
 
Back
Top Bottom