Suala la posho za wabunge

Tatizo Jk anaona kazi ya Urais ni wito,hivyo anaogopa asipigiwe kura ya kuto kuwa na imani naye bungeni.
 
Bad timing, watu wanakufa kutokana na mgomo wa madaktari Pinda akisema serikali haina pesa na huku wakishangilia kupewa posho za malaki na kuwazomea wanaopinga, laana gani hii, nasi watanzania tulirogwa na siasa za ujamaa, kipindi hiki kilikuwa cha wafanyakazi wote kuungana pamoja dhidi ya hawa mafisadi kwa sekta zote kugoma. Namshangaa mbayuwayu wa TUCTA Nicholaus Mgaya kutamka kuwa mgomo haujafuata taratibu. TUCTA wapo kwa ajili ya propaganda za kupoza wafanyakazi kwa maneno matamu yasiyokuwa na vitendo, shame on u.
 
Si vema kuchanganya mambo na kuongelea jambo muhimu lenye maslahi kwa taifa kishabiki,kwamba chadema wamemuachia Zito pekee si sahihi,kama shibuda na selasini wanaunga mkono posho ni wao kwani wana utashi wao,ila kumbuka wabunge karibu wote wa chadema wako pamoja ukiondoa hao wachache ambao wapo kimaslai zaidi.
 
Hivi hawa CCM -- kwa nini wanahangaika sana kutafuta sababu ya kukimbiwa kwa chama chao? nani atakipenda tena chama hicho? sasa hivi tutaanza kushuhudia siyo tena wizi wa kura, bali unyang'anyi wa kura!
Kupitia ongezeko hili la Posho leo nimeitumbukiza chooni kadi yangu ya CCM yani naona 2015 mbali kwa nn tusifanye kama Tunisia!!
 
serikali yetu imeshajua kuwa sisi ni waoga wa mabomu hivyo inafanya chochote inachotaka bila shida yoyote.nadhani sasa hata wale wanaowapinga madaktari juu ya mgomo wao watawaunga mkono.
 
nasubiri jioni nimsikilize kibonde ataongea nini...kuhusu hili jana alini boa kweli ...

Kibonde jana aliboa kishenzi. Huyu mweshimiwa ukimsikiliza ni kama msemaji wa serikali - tena siyefikiri. Tumezoea anaitetea serikali hata pale inapokosea, na tumemsamehe kwa hilo tukijua anatetea ugali wa watoto. Lakini hii ya jana ya kusifia kitendo cha kufukuza kazi madaktari, amepitiliza.

Japo yeye anajifanya anapinga waTz kujifunza kiengereza, najua yeye anakifahamu. Na si ajabu anasoma gazeti la Citizen. Namsihi aangalie ile picha kwenye Citizen ya leo, inayomuonesha mama kakaa chini na kachanga chake.
 
kumbe lengo la kulazimisha kukutana na waganga siku ya jumapili , ilikuwa kuwadanganya warudi kazini halafu jumatatu ukawatangazie wabunge nyongeza ya posho, kwani ulijua ukikutana nao baada ya nyongeza ya posho kwa wabunge hoja yako ya serikali kutokuwa na pesa ingekuwa kichekesho! haya sasa rudi kwa meza ya mazungumzo au lete askari wako waje kutibu!
 
Kweli watawala wetu wameamua hasa kujipendelea wao tu kwa vile wao ndiyo walioshika kisu cha kukatia keki, wameamua kukata mipande mikubwa mikubwa na kugawana wenyewe na vile vipande vidogo vidogo kuwapa wengine tena kwa mikiki, maandamana na migomo. Ili kunyang'anya zaidi kodi za "Wanyang'anyika" mngejitengenezea posho nyingine inayofanana sana na hiyo mnayolipwa sasa ya "Kukaa-kwenye-kiti allowance" ya shs 200,000.00. Ongezeni na: 1.Kusimama allowance=100,000. (Spika anapoingia ukumbini na kutoka huwa mnasimama) 2.Kushangilia allowance=100,000. (Ikitolewa hoja ambayo mbunge ameipenda, posho hii itamsidia kuondoa maumivu ya kupiga meza) 3.Pipi allowance=50,000 (mh atahitaji kitu cha kuchangamsha mdomo awapo ukumbini) 4.Chooni allowance=50,000 ( Hii itamsidia mbunge kama usafiri kutoka kwanye kiti alipoketi hadi chooni) Kama kuna allowance niliyoisahau mnaweza kuongezea ili mfanye kazi zenu kwa ufanisi kabisa ya kunyang'anya kodi ya wanyonge. Lakini ipo siku moja Mungu atakifanyia kazi kilio cha walala hoi kwa dhulma muwatendeazo.
 
kwa Taarifa zisizo na shaka toka chanzo maalumu, suala la posho za wabunge limeleta mtafaruku katika kikao cha wabunge kupata muhutasari wa kitakachojadiliwa bungeni.kikao hicho kinaendelea sasa hivi. Muda huu wabunge wote wameungana kumtukana ZITTO ambaye ametoa hoja posho zifutwe madaktari walipwe, kuanzia SPIKA hadi PINDA wote wanamuattack ZITTO na wengine kadhaa wanamtukana JANUARI MAKAMBA.

nitawapasha kitakachoendelea, ZITTO kawaambia hamnifanyi lolote na ukweli ndo nishawaambia hivyo.

Kwenye hili suala kwa taarifa zaidi ni kuwa hata wabunge wa CDM nao walimpinga Zitto kuwa anajitafutia umaarufu. Kweli kwenye hili hata wabunge wapinga posho wamekula matapishi yao wenyewe

 
Honestly, kuitetea CCM mbele ya maskini wengi wa Tanzania unahitaji kuwa na "kichwa cha Mwendawazimu".

How do you justify paying someone 330,000/day.
 
Nilisema juzi kuw a Pinda Pinda Pinda, ulimi kitu kidogo, lakini madhara yake ni hatari. Tayari Pinda na wenzake wameshaingia ktk mauaji ya halaiki. Na hili swala bado, suburini muone mwisho wake. Hata aibu hamna, Posho posho posho, madaktari unajifanya unawakemea. Hivi umelewa madaraka?? Ngoja uone moto wake sasa, manesi ndio hao hawataki kuwaona wanajeshi wako pale Muhimbili.....wengi wao ni wa kutibu First AID. H
 
Alikuwa anajua kuwa tayri posho zao zimeshabalikiwa na JK sasa kwa ujumla wake kwa siku wanakunja laki 3 na ushehe hivi.watanzania njia imeshafunguliwa itafaa sasa tuunge mkono kuikomboa hii nchi,hasa kujikomboa wenyewe
 
Hakuna kitu muhimu katika maisha kama BUSARA NA UADILIFU, kwa bahati mbaya ni vitu ambavyo viongozi wetu hawana.
 
Back
Top Bottom