Posho ya Vikao vya Bunge na Ziara za Kamati zifutwe

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Sitting allowance ya wabunge zifutwe na kubakia na mshahara tu! Hela ya dereva sijui msaidizi zote ziondolewe! Malipo ya vikao vya kamati zifutwe. Mfuko wa Jimbo ufutwe, Safari za Ulaya za kamati vibali kwa Rais. Wabunge walipwe mishahara tu na magari wakopeshwe. Ni maoni yangu tu ila kwakuwa Rais alikuwa Mbunge najua gharama halisi anazijua.

La mwisho ni I LOVE MY PRESIDENT! Najisikia raha kusema huyu ni Rais wangu.

Huu ndio wakati wa kuzitupulia mbali posho za wabunge (posho za kukalia kiti cha bunge) , posho hizi hazina tija zipingwe kwa nguvu zote.

Tumemuagiza mbunge wetu Mteule Zittokabwe asichukue posho, tunawaomba wabunge wote mzitupilie mbali posho zikasaidie maskini huko vijijini.

Pia tunategemea na kuamini Rais John Pombe Magufuli ukiisoma Ilani yetu utakubaliana nasi kuwa kuna umuhimu wa kuzifutilia mbali posho za Wabunge. Posho za wabunge ni sehemu mojawapo ya upendeleo na unyonyaji unaendelea nchini kwetu, huu ni wakati Wa mabadiliko sasa ukomeshwe kabisa.

Kama posho zisizokuwa na tija zitasitishwa na kukomeshwa zisiishie taasisi ya bunge tu iwe Taasisi zote zilizopo hapa nchini ili tujenge nchi yetu upya.

#PoshoSasaBasi

ACT-Wazalendo Taifa Kwanza
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kuwa Kamati ya Bunge imeenda nchi kadhaa kujifunza mambo yanayofanyika katika nchi hiyo kwa lengo la kutoa ushauri katika nchi yetu. Hata hivyo, wabunge wamekuwa wakitumia vibaya ziara hizo na wengi wameishia kwenda kujivinjari na mahawara zao tu. aidha, ziara hizo zimekuwa zikigharimu mabilioni ya shilingi ilhali ufanisi wake hauonekani.

Kutokana na hali hiyo, ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya Hapa Kazi Tu, nashauri ziara hizo zifutwe kabisa. Najua Rais Magufuli amefuta safari za nje ya nchi kwa watendaji na viongozi wa Serikali. Hata hivyo, zuio hilo halijahusu muhimili mwingine wa Dola ambao ni Bunge. Hivyo ili kuweka mkakati wa pamoja, Spika wa Bunge akishachaguliwa naye atangaze kusitisha ziara hizo ili wabunge wabaki majimboni kusaidiana na wananchi kutatua kero zinazowakabili.

Nawasilisha.
 
Mi napendekeza allowance ziwepo ila zisiwe sasa ndo mpunga mwiiingiii.....

Kazi kama zile za siasa bila allowance nazo zinachosha.
 
mengine umepatia ,,ila kuusu mfuko wa jimbo umebugi mkuu.
bila mfuko wa jimbo sasa maendeleo ya jimbo yataendaje???
 
Kuna kipindi Nilikuwa natamani sana Rais wa Kenya UHURU KENYATA kutokana na tabia yake ya kupeleka maslahi ya Kenya Mbele! ILA KWA SPEED HII. TANZANIA tunae Rais! Najitokeza Kuwaambia I LOVE MY PRESIDENT. This is our president of all time!

Kama unamkubali THE PRESIDENT karibu.
 
Daaaah ni noumah babake...

Kama ataendelea hivi hakika 2020 Tanzania tutakuwa tunafukuzana na Ujerumani kwa maendeleo.......hahaa Prank''
 
Kuna kipindi Nilikuwa natamani sana Rais wa Kenya UHURU KENYATA kutokana na tabia yake ya kupeleka maslahi ya Kenya Mbele! ILA KWA SPEED HII. TANZANIA tunae Rais! Najitokeza Kuwaambia I LOVE MY PRESIDENT. This is our president of all time!

Kama unamkubali THE PRESIDENT karibu.

Naona kuna haja ya elimu juu ya spelling za jina la mh. rais wetu maana hapo juu umeandika kikurya (R) badala ya kisukuma (L)
 
Hzo ni ndoto kwa siasa zetu mbofu mbofu hzi. Watawala wa CCM wanalitumia bunge letu kufunika na kufanikisha maovu na madili yao kwa hiyo kuwaminya wabunge hasa wa ccm ambao ndio wengi ni sawa na kuiweka serikali hatarini kukwama mambo yake hasa bajeti na mengineyo kupita bungeni. Na hii ndio simple logic ya wabunge kupewa mishahara mikubwa na marupurupu kibao wakati walimu na madaktari na watumishi wengine wa umma wakiendelea kuuumia kwa kisingizio cha serikali haina fedha!
 
Back
Top Bottom