Suala la posho za wabunge

Kama hatuta gomea haya mabadiliko sasa, hatutakaa tuwawajibishe hawa wanasiasa
 
Kunaumuhimu wa kujilipua kwa petroli pale mjengoni pale hawa jamaa wanapokuwa break kuonesha kwamba sie hatuyaoni maisha kuwa magum bali wao pekee!
 
Hivi hawa CCM -- kwa nini wanahangaika sana kutafuta sababu ya kukimbiwa kwa chama chao? nani atakipenda tena chama hicho? sasa hivi tutaanza kushuhudia siyo tena wizi wa kura, bali unyang'anyi wa kura!
 
KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGA

Waandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku. Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.

Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani. Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta umaarufu wa kisiasa.

"Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga posho," chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho. Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. "Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama," kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.

Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili kutoka nchi za nje. "Shelukindo anasema amefanya ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo," chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo wake kwamba ongezeko hilo halina ‘mashiko' na haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka kukaa chini.

Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu, kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi kuwa amewatukana. "Zitto ametumia Kiingereza kuwa tatizo la wabunge ‘we think small', Shelukindo na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana," chanzo chetu kilieleza. Zitto anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alinukuliwa akisema matatizo ya posho yamefikia hapo baada ya kuonekana ni ya watu binafsi siyo mfumo hivyo, wanaopinga wanaonekana kama wanatafuta umaarufu na wana vipato vya fedha, akaitaka kamati ya uongozi ijadili na kupata mwafaka badala ya wajumbe kutofautiana mbele ya umma. Wabunge wengine wanaodaiwa kutetea posho hizo ni Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na Jenister Mhagama (Peramiho CCM).

Msimamo wa January
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Makamba alijibu: "Si sahihi kwangu kutoa taarifa za kikao cha ndani. Lakini msimamo wangu kwenye suala hilo unajulikana na haujabadilika. Msimamo wa CCM ulishawekwa wazi na sote tunaujua. Nitalizungumzia suala hili kwa kirefu katika siku zijazo."

Kuhusu taarifa kwamba anagharamiwa na CCM, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka kiulizwe chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu taratibu za kuwagharamia viongozi wa chama chake ambao ni wabunge alisema: "Mbunge au kiongozi yeyote wa chama mwenye nafasi nyingine anagharamiwa na chama pale anapokwenda kufanya shughuli za chama tu na si vinginevyo."

"Kwa hiyo kama ni mbunge suala la mafuta, dereva, mahali pa kulala na mahitaji mengine anagharamiwa na taasisi anayoifanyia kazi na siyo chama."

"Kwa mfano, mimi kwenye sekretarieti hata posho za vikao huwa sichukui, nadhani na mwenzangu January naye sidhani kama huwa anachukua posho, kwa sababu tukifanya hivyo ni kama tunakiumiza chama, huo ndiyo msimamo wetu na uko wazi wala siyo kificho."

Kwa upande wake, Zitto alisema jana kwamba hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia suala hilo na badala yake kuahidi kwamba atalizungumza leo atakapokutana na waandishi wa habari.

Wabunge walia njaa
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema wabunge hao walilalamikia kucheleweshwa kulipwa posho zao za wiki mbili walizokaa Dar es Salaam wakati wa vikao vya kamati.

Walidai hivi sasa wanaishi kwa shida huku wakihoji sababu za
kucheleweshewa.

Imeelezwa kwamba Spika Makinda alidai kuwa fedha hizo zipo na kwamba kilichochelewesha ni uhakiki wa wabunge waliohudhuria vikao.

Makinda alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakilipwa posho za vikao bila kuhudhuria, hatua ambayo imesababisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), kuhoji maswali mengi.
 
Hii serikali inabidi kuibana zaidi, et nini! JK mnafikihuyu, Pinda Mnafiki huyu, Mibunge ya CCm Minafiki hiii!!!

Tunahitaji migomo zaidi, poli nao wajianda kwa mgomo mkubwa lazima kieleweke!
 
JK abariki posho mpya za wabunge

KILA MMOJA KULIPWA
330,000 KWA SIKU, ZITTO,
MAKAMBA, KIGWANGALA
WASULUBISHWA KWA
KUZIPINGA,

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda
amesema tayari Rais Jakaya
Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa
wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.

Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa
mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa
mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000
zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi
cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa
taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa
Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama
na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais
Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini,
Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto
ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda
kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo
akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa

Serikali
wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia
baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais,
angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge. Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa
kuwashambulia Zitto,

Mbunge wa Bumbuli (CCM),
January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk
Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa
mbele kupinga posho hizo hadharani. Spika wa Bunge,
Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete
ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia
wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta
umaarufu wa kisiasa. “Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi
ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya
kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga
posho,” chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa
anadaiwa kwamba alitumia mafumbo
kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza
kupinga nyongeza hiyo ya posho. Kauli hiyo inadaiwa
kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said
Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini
akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba
ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM.

“Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa
gari, nyumba na analipwa na chama,” kilisema chanzo
chetu kikimkariri Nkumba. Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM),
anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge
posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili
kutoka nchi za nje. “Shelukindo anasema amefanya
ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili
Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo,” chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo. Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi
hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo
wake kwamba ongezeko hilo halina ‘mashiko’ na
haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini
alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka
kukaa chini.

Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza
kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu,
kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi
kuwa amewatukana. “Zitto ametumia Kiingereza
kuwa tatizo la wabunge ‘we think small’, Shelukindo
na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana,” chanzo chetu kilieleza. Zitto
anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja
ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa
hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na
kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika
alinukuliwa akisema matatizo ya posho yamefikia
hapo baada ya kuonekana ni ya watu binafsi siyo
mfumo hivyo, wanaopinga wanaonekana kama
wanatafuta umaarufu na wana vipato vya fedha,
akaitaka kamati ya uongozi ijadili na kupata mwafaka badala ya wajumbe kutofautiana mbele ya umma.
Wabunge wengine wanaodaiwa kutetea posho hizo ni
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na
Jenister Mhagama (Peramiho CCM). Msimamo wa January
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Makamba alijibu: “Si
sahihi kwangu kutoa taarifa za kikao cha ndani. Lakini
msimamo wangu kwenye suala hilo unajulikana na
haujabadilika. Msimamo wa CCM ulishawekwa wazi
na sote tunaujua.

Nitalizungumzia suala hili kwa kirefu katika siku zijazo.” Kuhusu taarifa kwamba anagharamiwa na CCM,
alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na badala
yake kutaka kiulizwe chama hicho. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alipoulizwa kuhusu taratibu za kuwagharamia
viongozi wa chama chake ambao ni wabunge alisema:
“Mbunge au kiongozi yeyote wa chama mwenye
nafasi nyingine anagharamiwa na chama pale
anapokwenda kufanya shughuli za chama tu na si vinginevyo.” “Kwa hiyo kama ni mbunge suala la mafuta, dereva,
mahali pa kulala na mahitaji mengine anagharamiwa
na taasisi anayoifanyia kazi na siyo chama.” “Kwa mfano, mimi kwenye sekretarieti hata posho za
vikao huwa sichukui, nadhani na mwenzangu January
naye sidhani kama huwa anachukua posho, kwa
sababu tukifanya hivyo ni kama tunakiumiza chama,
huo ndiyo msimamo wetu na uko wazi wala siyo
kificho.” Kwa upande wake, Zitto alisema jana kwamba
hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia suala hilo na
badala yake kuahidi kwamba atalizungumza leo
atakapokutana na waandishi wa habari.

Wabunge walia njaa
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema wabunge
hao walilalamikia kucheleweshwa kulipwa posho zao
za wiki mbili walizokaa Dar es Salaam wakati wa
vikao vya kamati. Walidai hivi sasa wanaishi kwa shida huku wakihoji
sababu za
kucheleweshewa. Imeelezwa kwamba Spika Makinda alidai kuwa fedha
hizo zipo na kwamba kilichochelewesha ni uhakiki
wa wabunge waliohudhuria vikao.

Makinda alisema baadhi ya wabunge wamekuwa
wakilipwa posho za vikao bila kuhudhuria, hatua
ambayo imesababisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Serikali (CAG), kuhoji maswali mengi.

Source:mwananchi.
 
Ndani ya siku 10 kila mbunge ataondoka na mil 3.3, hivi inakuwaje watanzania tunaachia haya yaendelee? Mbona sheikh Yahya mlinzi wa Vasco alishakufa, nini kinafanya watanzania tusiingie barabarani na kupinga dhuluma hii ya hawa watawala wetu (maana hawa si viongozi).
 
Duh kweli ccm ni wasikivu! rais ni msikivu! serikali ni sikivu! na watanzania ni wavumilivu! Period!
 
Eti nini vile? Kwa mtindo huu mtu kusema eti CCM yatumainiwa kutujengea uchumi unaopaa yote ni ndoto tupu. Kuna kila ishar chama hiki kimeshakata tamaa hivyo kimeamua kwamba sasa liwalo na liwe tukose sote na kuchukua kinachowezekana leo hii hii kabla ya 2015.
 
hii nch watu hatuna msimamo kabisa, madkatari wenyewe wanahujumiana wao kwa wao, kama madkatari wengine wanagoma na wengine wanaendelea na kazi unategemea nini?

Watanzania sisi ni waoga kama wahindi, make tanzania na india ndo nchi zenye wanachi waoga sana, tuna baki kulalamikia kwenye vujiwe vya kahawa na kwenye vijiwe vya wabrush viatu, wanatumia muanya wa sisi kuwa waoga kufanya hayo yote, wanajua hakuna wakugoma, madaktari ndo hao wameshindwa, ni wafanya kazi gani wataweza?

-tutalalamika sana lakini mwisho wa siku hakuna tutakacho fanya, ok tuendelee kulalamika
 
Kweli Jey Key Tikitimaji. Yaani na mateso yote wananch wanayopata na wafanyakaz wanaolipwa kiduchu bado kapitisha posho!?. Hakika walisema aliyeshiba...........
 
duh kweli ccm ni wasikivu! Rais ni msikivu! Serikali ni sikivu! Na watanzania ni wavumilivu! Period!

ccm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.........ccm juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...........! Kidumu chama cha mapinduzi.....!
 
Tanzania nchi ya posho. Wabunge wanapigania posho, madaktari posho, kila mtu posho!
 
Back
Top Bottom