Suala la posho za wabunge

Unless and until the current ruling guys are forcibly thrown out we'll always witness the shocking, horrifying and terrifying events in our country.

MP's sitting allowance has shot up from Tzs 70,000 to 330,000 in the midst of hiked electricity bill per unit; the costs which no normal citizen wil comfortably afford.

Let the doctors lead the way to the battle front-line.
 
Mh pinda ameambiwa na mama spika kuwa maisha yamepanda dodoma tu, lakini inauma kumlipa mbunge laki 3 kwa siku kama posho alafu anaonyeshwa kwenye tv amesinzia!! au kipindi chote cha bunge hachangii chochote,

Pia kinachonikasirisha zaidi mapendekezo wanayopitisha mengi serikali haiyatekelezi.
 
CCM ni laana kubwa na mwenye kuimaliza hii laana ni wapiga kura .Lakini wapiga kura wa Lindi , Mtwara , Pwani , Tanga , Morogoro, Dodoma sina hakika kama wanaijua na kuiona hii laana .Lakini kuna siku CCM hawataamini kilio kimeongezeka ma CCM yamejawa na kiburi cha kutisha na hawajali tena ustawi wa jamii wao ni madaraka tu .
 
Ivi si ata chama CCM walisema posho hakuna kupanda,na CCM hao hao waliponda ongezeko la bei ya Kerosene.
Ivi chama tawala ni CCM au CDM mbona hawakiishi wanachokizungumza?
 
mimi Gang Chomba, nikiwa na akili timamu pasipo kushinikizwa na mtu nasema wazi bila kujiuma uma kuwa waziri mkuu pekee ambaye mwenyezi Mungu alitupa kama zawadi basi alikuwa EDWARD wa pekee, hapa namzungumzia Hayati Sokoine.
 
Hawa viongozi wa Tanzania ,pamoja na na mapungufu yake wakati mwingine namuona JK afadhali kuliko Pinda
 
mimi Gang Chomba, nikiwa na akili timamu pasipo kushinikizwa na mtu nasema wazi bila kujiuma uma kuwa waziri mkuu pekee ambaye mwenyezi Mungu alitupa kama zawadi basi alikuwa EDWARD wa pekee, hapa namzungumzia Hayati Sokoine.
Ahhaa! maana nilianza kukunja ngumi nikidhani unamtaja haka kabepari kasikotosheka na kitu!
 
kumbe lengo la kulazimisha kukutana na waganga siku ya jumapili , ilikuwa kuwadanganya warudi kazini halafu jumatatu ukawatangazie wabunge nyongeza ya posho, kwani ulijua ukikutana nao baada ya nyongeza ya posho kwa wabunge hoja yako ya serikali kutokuwa na pesa ingekuwa kichekesho! haya sasa rudi kwa meza ya mazungumzo au lete askari wako waje kutibu!

Pinda ataanza kulia sasaivi
 
Eti ''mtoto wa mkulima" Astaghfirullah, Astaghfirullah, Astaghfirullah.... Ni mroho tu kama waroho wengine, ni fisadi tu kama mafisadi wengine, ni mwizi tu kama wezi wengine, na ni mnafiki kuliko hata hao wanafiki wengine na wanaomtetea wote wako kundi hilohilo, ina maana yupo nchi gani?? kiongozi gani asiyejua vipaumbele katika nchi yake?? Ningekuwa Daktari ningegoma hadi nukta ya mwisho, ningekuwa mwalimu, Askari ningeuwasha moto usiozimika!! Nadhani wanayataka ya Misri........ Mnzxxxxxnxzxxxzyyy, sonyo hilo...
 
Bado kidogo tu kitaeleweka, hapa bila kuumizana tutaendelea kuchezewa na hawa majizi ya magamba.
 
  1. Rais ameshaidhinisha posho za wabunge na leo wameshaingiza siku kwa kukaa masaa 2 tu!!!...kodi zetu zinakwenda kwa wachache ambao ndio inasemekana wenye haki zaidi kuliko wengine (hata madaktari wanaoshughulika na Roho zao
  2. Mafisadi wanaendelea kupeta tena wakitaka kuja kula zaidi kwa mgongo mwingine na huiku wakikumbatia na kivuli cha makanisa
  3. Migomo ya madaktari inaendela bila kujulikana hatma yake
  4. Watu wanaendelea kujimegea nchi kwa kusaini mikataba ya kupeana ardhi na malighafi
  5. Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu, huku mfumuko wa bei ukishika kasi
  6. wenye dhamana wanaendelea kupigana vikumbo kwa urais wa 2015................badala yakushughulikia matatizo yetu
  7. Nchi haina uhakika kama itaendelea kuwa nuruni maana umeme haueleweki kabisa...
  8. ....................................................................
  9. ......................................................................
  10. ......................................................................
  11. Kila mtu anaendelea kulalamika tu.......

 
Jamani hivi hakunawaa Wachawi wanaoweza kuwaloga hawa watu wakawa Mataila wote?????? Maana unasoma mambo hapa mpaka unashindwa kuelewa hivi Tunaongozwa na Mashetani??
 
Jamani hivi hakunawaa Wachawi wanaoweza kuwaloga hawa watu wakawa Mataila wote?????? Maana unasoma mambo hapa mpaka unashindwa kuelewa hivi Tunaongozwa na Mashetani??

Wabunge wetu mbona ni mataila, sasa ikiwaloga itakuwa nini tena????
 
Ndugu wanajamii forum, hivi sasa tupo ndani ya nchi yetu ya Tanzania kama hatupo, maana viongozi tuliowaweka madarakani wanfanya watakacho nasi tumebaki tukilalama bila mafanikio. Kwani hatuna cha kuwafanya maana teyari wameshashikiria mpini nasi tupo kwenye makali. Nayasema haya kutokana na matukio ya hivi karibuni au yanaendelea mpaka sasa ndani ya hii nchi yetu. Yapo matukio kadhaa lakini naomba nielezee haya;

Posho za wabunge

Licha ya wanachi waliowengi kulalamikia kitendo cha wabunge kujiongezea posho, lakini wawakilishi hao wa wananchi bado wameweka pamba masikoni bila aibu wameshikilia tama zao za fedha bila kuwajali waliowachagua na jana 31 jan 2012 Waziri Mkuu mh Mizengo Pinda akatangaza kuwa posho hizo zimeongezeka naye Spika wa bunge akathibitisha kuwa rais Jakaya Kikwete ameshasaini muswada wa posho na sasa ni sheria kuwa wabunge walipwe posho hizo mpya wanazodai. Kwa hesabu za haraka haraka kwa mwaka mmoja tu posho za wabunge (ukiondoa mishahara yao, posho za vikao vya kamati, posho za semina wakati wa wikiend, gharama za mafuta, mchango wa maedeleo ya jimbo) zinafika karibu bil. 12,474,000,000/=. Hapa nimechukua wastani wa siku mia moja wanazotakiwa kukaa bungeni kwa mwaka mzima( wiki 3 mwezi February, wiki 3 mwezi April, wiki 3 mwezi October na siku 72 kwenye bunge la bageti mwezi June ukatoa wikiendi zote). Hizi ni gharama za vivuko viwili kama cha mv. Magogoni. Hapa najiuliza hawa wabunge wanania ya kweli kumtetea mwananchi?

Utetezi wa posho

Kwa kuzitetea posho hizi walijitokeza Spika na naibu wake pamoja na waziri mkuu ayejiita motto wa mkulima.
Katika utetezi wake Spika wa bunge Mh. Anne Makinda alisema poshohizo zimeongezwa kutokana na gharama za maisha pale Dodoma kupanda ikiwamo gharama za hotel, hata hivyo wamiliki wa hotel hizo wakajitokeza na kukanusha gharama hizo lakini bado spika akang'ang'ania msimamo wake.

Waziri Mkuu Mh. Pinda nae aksema wabunge huwapa wapiga kura wao fedha mara waendapo kuwalilia shida zao na hivyo haoni kama kuna ubaya wakipandishiwa posho hizo, kwangu mimi huu ni utetezi wa motto wa darasa la pili au la tatu maana sizani kama wabunge huchaguliwa ili wawe wasamalia wema kwa kugawa hela kwa walio na shida.

Naibu Spika yeye ndo alitoa mpya pale alipotetea posho hizo kwa kuzilinganisha na wafanyakazi wa idara nyingine kama uhamiaji, mahakama, TANAPA na TRA. Hapa napo nilibaki hoi maana njuavyo wabunge si wafanyakazi mpaka walipwe sawa au zaidi ya wafanyakazi. Ubunge ni wito (Sio kama wa waalimu, wauguzi au wanajeshi) hivyo sioni sababu ya wabunge kujilinganisha na wafanyakazi wakati ubunge sio ajira, Kwa wbunge wetu wa leo ubunge wanaona kama ajira wakati sio kweli. Na wala hawalazimishwi kuwa wabunge wakitaka waache kama gharama za kuutumikia ubunge ni kubwa. Hivi bila wabunge hatuwezi kuishi?Utetezi huu kwangu ni dhaifu kiasi kwamba inaonekana kama matusi kwa wananchi, kwani tunapewa sababu yoyote ilimradi kuna ufafanuzi kwani hatuna cha kuwafanya hata wakitekeleza matakwa yao.

Mgomo wa madaktari

Mwanzoni nilikuwa nasita kuunga mkono kwa umesababisha madhara makubwa kwa wananchi na niliona madaktari wanawatumia wananchi kama chambo ya kupata mahitaji yao! Lakini kwa hili la wabunge na madaktari nao walistahili kugoma. Serikali kila siku haina hela lakini ikifika kwa wabunge hela zinapatikana hapa nashangaa, kwa madaktari haina hela kwa wabunge zipo! Haya ni mambo ya firauni kabisa kabisa.
Mgomo huu navyoona hautafanikiwa kwani serikali kwa kujikosha itawapa nyongeza kidogo na sio kama walivyoomba mshahara wa mil 3.5 kwani inaonekana wananchi tumegawanyika wapo wanouunga mkono na wapo wanaoupinga kwani wanaonakama wametolewa kafara kwa madai ya wengine.

Maslahi ya wafanyakazi

Kwa mtazamo wangu wafanyakazi karibu wote wanamadai yanayofanana sijui wa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama maana hawa ndo huwalinda hawa viongozi serikalini na wala hawajawai kugoma wala kulalamika inaonekana kwao mambo ni mtelemko, lakini kwa kada zingine kama waalimu, manesi, madaktair,mahakama, TRL na wengineo wote madai ya mishahara na posho ni yaleyale. Kinachowashinda mpaka kila siku wanalialia ni utengano wao katika kudai hizo stahiki zao, mara utasikia leo waalimu, kesho TRL( ingawa siku hizi siwasikii tangu katibu wao Sylvesta Rwegasira afariki), kesho kutwa utaskia madaktari. Hivyo utengano wenu ndiyo unawanyima haki zenu. Siku zote najiuliza je hawa wafanyakazi hawana chama kinachowaunganisha? Na kama kudai kwanini wasidai kwa pamoja? Hebu tujiulize kama mahakama,walimu, madaktari na wengine wote wagome kwa pamoja serikali haitatikisika na kuwasikiliza? Lakini mkigoma madaktari tena wa muhimbili wataletwa wanajeshi kama kawaida.

Yangu ni hayo kwa leo hebu tujadili kidogo kwa hili wanajamvi.
 
Nimefuatilia hii ishu ya posho, hasa pale ilipoonekana wazi kuwa Spika na Waziri Mkuu wametudanganya.
Ivi kweli tunawezaje kuwasamehe? Upinzani bungeni upo wapi kuwasulubisha hawa waongo?
Ni kweli hii ishu inaishia kujibiwa kwenye magazeti na press releases tu? Tunakuwa na bunge la kazi gani?
It is time wananchi tudai bunge la kweli.
By the way...tusisahau ile ishu ya kuwa na bajeti mbili ambayo nayo haikuzungumziwa bungeni ikaishia kwenye magazeti.

Hapa nimeweka mfano wa bunge linalokaa kiukweli na hata likidai posho ya laki 2 itakuwa sawa.
Na huu ndio upinzani haswa. Hakuna kuogopa mtu, heshima inaachwa mlangoni, kazi inafanyika.
Maoni yangu: Kama hatuwezi kuwa na bunge la namna hii, ni bora tuache kuwa na bunge.

<font size="3">
 
Last edited by a moderator:
Nimefuatilia hii ishu ya posho, hasa pale ilipoonekana wazi kuwa Spika na Waziri Mkuu wametudanganya.
Ivi kweli tunawezaje kuwasamehe? Upinzani bungeni upo wapi kuwasulubisha hawa waongo?
Ni kweli hii ishu inaishia kujibiwa kwenye magazeti na press releases tu? Tunakuwa na bunge la kazi gani?
It is time wananchi tudai bunge la kweli.
By the way...tusisahau ile ishu ya kuwa na bajeti mbili ambayo nayo haikuzungumziwa bungeni ikaishia kwenye magazeti.

Hapa nimeweka mfano wa bunge linalokaa kiukweli na hata likidai posho ya laki 2 itakuwa sawa.
Na huu ndio upinzani haswa. Hakuna kuogopa mtu, heshima inaachwa mlangoni, kazi inafanyika.
Maoni yangu: Kama hatuwezi kuwa na bunge la namna hii, ni bora tuache kuwa na bunge.

<font size="3">


Bunge letu kuna wabunge kibao ambao wapo pale lakini hawajui kazi yao ni nini. Sasa inapofikia MP anasema pesa wanazopata ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kutoka majimboni wanapokuja Dom then ujuwe ni tatizo ta Kitaifa. The Other thing, wabunge wetu wakiwa Dom kazi yao kubwa ni kujirusha kwa sana usiku kucha halafu kesho yake wanakuwa wamechoka hivyo wanalala ovyoovyo!!
 
Last edited by a moderator:
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom